Articles by "Computer"
Showing posts with label Computer. Show all posts
Kampuni ya Dell hivi karibuni imerudi tena na laptop yake mpya ya Dell Inspiron 7572, laptop hii inakuja na kioo cha inch 15.6 kilichotengenezwa kwa teknolojia ya FHD chenye resolution ya 1920 x 1080 ambacho pia ni InfinityEdge IPS display.

Kava la laptop hii limetengenezwa kwa ubora kwa kutumia Aluminum pamoja na Magnesium alloy, ambayo kwa pamoja inafanya laptop hii kuwa na kava lenye ubora zaidi. Kwa ndani Dell Inspiron 7572 inakuja na processor ya Intel Core i5-8250U processor yenye speed ya 3.4GHz ambayo inasaidiwa na RAM ya DDR4 yenye uwezo wa GB 8. Vilevile laptop hii inakuja na toleo lingine lenye processor ya Intel Core i7-8550U processor yenye speed ya 4.0GHz.

Kwa upande wa Graphics, laptop hii inakuja na GPU ya NVIDIA GeForce MX150 yenye uwezo wa GB 4 GDDR5 graphics memory. Mbali na hayo Dell Inspiron 7572 inakuja na ukubwa wa kuchagua kati ya SSD yenye ukubwa wa GB 128 au HDD yenye ukubwa wa TB 1, sifa kamili za Dell Inspiron 15 7572 ni kama zifuatazo.
JinaDell Inspiron 7572
Ukubwa19.5 x 358.16 x 246.95mm
Uzito2.00kg
Kioo15.6-inch FHD (1920 x 1080)
CPU8th Generation Intel Core i5-8250U/ i7-8550U
GPUNVIDIA GeForce MX150
RAM8GB – expandable upto 16GB
Ukubwa wa ndani128GB SSD + 1TB
Sehemu za kuchomeka1 HDMI, 1 USB 3.0, 1 USB 3.0 with PowerShare , 1 USB 2.0, 1 Noble lock slot, 1 SD card
Battery42 WHr
Mfumo wa uendeshajiWindows 10 Home/Pro
Bei ya Dell Inspiron 7572
Kwa upande wa bei ya Dell Inspiron 7572 inatarajiwa kuuzwa kwa nchini india na itakuwa inapatikiana rasmi kwa matoleo manne tofauti ambapo toleo la chini litapatina kwa rupee ya india RS 54990 ambayo ni sawa na Tsh 1,715,000 bila kodi.
Kutengeneza Bootable USB katika Windows 10 bila ya kutumia Software ndio njia pekee rahisi na  ya usalama zaidi ya kuinstall Windows kwa sasa.

Siku hizi watu wachache sana wanaochoma (burn) ISO ya Windows  kwenye cd na kuitumia katika installation, wengi wanatumia usb flash sababu ni njia ya haraka na rahisi zaidi katika kufanya zoezi hilo. Kuna tools nyingi zinazosaidia katika zoezi hilo na kufurahisha zaidi mpaka Microsoft wenyewe wametengeneza baadhi ya tools za kusaidia zoezi hilo, ila kuna njia rahisi na ya haraka ya kufanya flash yako iwe bootable bila ya kutumia software yoyote ile.
Hebu tuangalie zoezi hilo:

Njia za kufuata ili kutengeneza Bootable USB katika Windows 10 bila software yoyote ile

 • Chomeka flash yako unayokusudia kuifanya kuwa bootable, Angalizo: zingatia ukubwa wa flash na ukubwa wa faili lako.
 • Fungua ukurasa wa komandi (Command Prompt) kwa kutafuta Command Prompt katika Task bar, au unaweza ukabonyeza Windows+R kwa wakati mmoja na sehemu ya kuandika itatokea, andika cmd katika sehemu hiyo alafu bonyeza Enter
 • Kama utajaribu kufungua Command Prompt kwa kutumia Task bar chagua Run as administrator
 • Window mpya nyeusi (Command Prompt) itatokea, hiyo ndio sehemu ya kuandika komandi, andika disk part na bonyeza Enter, subiri kwa muda Diskpart itafunguka katika Windows nyingine.
 • Baada ya window ya diskpart kufunguka, andika list disk na diski zote zilizopo kwenye kompyuta wako kwa muda huo zitafunguka, na zitakuwa na herufi na zimepangwa kwa namba kuelekea chini.
Mara nyingi utakutana na aina mbili za diski, Disk 0 kwa hard disk na Disk 1 kwa flash na ukubwa wake.
Kwa kuwa tunaenda kutengeneza Bootable ISO kwenye flash hivyo tutadili na Disk 1
 • Andika select disk 1 alafu bonyeza enter. Utapata ujumbe unaosema Disk 1 is now the selected disk. Hii inamaanisha chochote utakchokuwa unafanya hapa kitaathiri diski hii moja kwa moja.
 • andika clean alafu bonyeza enter, clean command itafuta kila kitu kilichopo katika diski yako. ikmaliza ujumbe Diskpart succeeded in cleaning the disk utatokea.
 • Andika create partition primary alafu bonyeza enter utapata ujumbe Diskpart succeeded in creating the specified partition
 • Andika select partition 1 alafu bonyeza enter, itachagua partition 1 kama active partion.
 • Bonyeza active alafu bonyeza enter , hii itaactivate partition hiyo
 • Andika format fs=ntfs quick alafu bonyeza enter . Komandi hii itaifanya flash hiyo kuwa na format ya ntfs file system kwa haraka zaidi.
 • Andika exit alafu bonyeza enter, hii itaifunga Diskpart program, ila usiifunge window ya command prompt.
 • Hapa kabla hatujaendelea  hebu tuangalie baadhi ya vitu kwa uangalifu zaidi, angalia flash yako imepewa herufi gani, katika kesi yetu ina herufi drive G: na file lako la Windows unalotaka kulikopi lipo kwenye drive E:.
 • Kwa kawaida Command Prompt’s active directory for Administrator permission lipo kwenye C:\Windows\System32>. Hapa tunatakiwa kuielekeza Command Prompt ichukue mafile kutoka katika drive E:
 • Andika E: alafu bonyeza enter alafu active directory litabadilika lenyewe na kuwa katika E:
 • Andika cd boot alafu bonyeza enter . Hapa active directory litabadilika na kuwa E:\boot>
 • Andika bootsect /nt60 g: alafu bonyeza enter itatengeneza boot sector katika G: drive (USB Flash drive)
 • Andika exit alafu bonyeza enter kufunga command prompt.
Mpaka hapa utakuwa tayari umeshatengeneza bootable USB na flash drive ipo tayari kwa zoezi zima la kuinstal windows.
Ili kuinstall windows katika USB Drive tunatakiwa kuhamisha (kucopy) file zima la windows kutoka katika drive E: na kulipeleka katika Flash Drive.
 • Kufanya hivi kirahisi na kwa uhakika, fungua tena command prompt, baada ya kuifungua andika xcopy e: \ *. * G: \ / E / H / F alafu bonyeza enter. Subiri mpaka mafaili yote yahamie kwenye flash drive.
Baada ya hapo Flash itakuwa tayari kwa zoezi zima la kuinstall Windows kwenye Kompyuta nyingine.
Nadhani utakuwa umefurahia makala hii, kama unaswali lolote tafadhali uliza katika sehemu ya maoni hapo chini.
Katika kufuatilia utumiaji wa data katika Windows 10 wengi tunatumia “Windows Task Manager”, lakini ukweli ni kwamba Windows Task Manager inaonyesha matumizi ya data ya application za msingi za Windows. Fahamu jinsi ya kufuatilia utumiaji wa data wa programu zote katika Windows 10.
Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Windows 10 utakuwa umegundua ni kwa jinsi gani programu hii endeshi kutoka Microsoft inavyokula kiwango kikubwa cha data au MB kama tunavyoita tulio wengi. Wengi huwa wanalalamika watoa huduma za kimtandao wao (ISPs)  wanawaibia kwa sababu tu kifurushi alichojiunga kimeisha mapema wakati hajafanya chochote.
Katika kompyuta zetu kuna programu mbalimbali zinazofanya kazi kwa kutumia mtandao bila ya sisi kufahamu na wengi wetu tumekuwa tukijaribu kuangalia ulaji wa data kwa kutumia Windows Task Manager,  lakini ukweli ni kwamba sio matumizi yote ya data katika kompyuta yako yanaoenekana katika Task manager.
Mfano mimi huwa natumia Skype, Mozilla,Games na kuangalia Movies mtandaoni na hapa ndipo napoona umuhimu wa kufuatilia utumiaji wa data katika kompyuta yangu. Hebu tuangalie njia rahisi za kujua kiwango gani cha data unatumia katika kompyuta yako na jinsi ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya data.

Njia za kufuatulia utumiaji wa data katika Windows 10

Kuna njia kuu mbili,
 • Kwa kutumia application za bure za kufuatilia matumizi ya data
 • Kwa kutumia Windows Task manager

Tumia application ya bure ya Free Network Usage katika Windows 10

 • Fungua sehemu ya kutafuta (Search) katika windows 10 na tafuta neno “Network Usage” katika sehemu ya kutafuta.
 • Fungua tokeo la juu kabisa lililoandikwa Network Usage kama inavyoonekana katika picha na windows itakupeleka katika ukurasa wa kupakua programu hii, bonyeza kitufe cha free kilichopo chini ili kushusha programu hii.
 • Mara baada ya kupakua programu hii itafunguka kama inavyoonekana katika picha chini na kuanza kufuatilia matumizi yako ya mtandao
 • Upande wa juu kushoto kuna kitufe cha Settings na utaweza kupangilia jinsi programu hii itavyokuwa inafanya kazi.
Programu hii ni nzuri kwa wale wanaotaka kujua kiwango cha data alichotumia mwezi uliopita au mwezi uliopo ili uweze kulipa na kupanga bajeti zako, ila kama unataka kufuatilia kiwango cha data katika kila programu ndani ya windows 10 tafadhali fuata njia ifuatayo.

Jinsi ya kuangalia matumizi ya data kwa kutumia Task Manager

 • Kufungua Task Manager kiurahisi bonyeza Ctrl+Shift+Esc, au unaweza ukaright click kwenye Taskbar na chagua Task Manager
 • Bonyeza sehemu iliyoandikwa Application History katika vitufe vya juu vya Task Manager
Hapo utaweza kuona matumizi ya data kwa application za msingi za windows lakini applications kama Kivinjari chako (Web Browser), Skype na Games hutoweza ziona hapo. Haileweki kwa nini Microsoft aliamua kufanya hivyo, usihuzunike ngoja tuangalie njia mbadala ya kufanya hivyo.
 • Fungua Windows 10 Settings na chagua Network and Internet
 • Baada ya kufunguka chagua Data Usage katika kipengere cha Network and Internet, alafu fungua Usage Details
Baada tu ya kufungua, kidirisha kingine cha windows kitafunguka na hapo ndipo utaweza kuona applications nyingine tofauti na zile za msingui za windows. Kama unavyoona katika picha Chrome imetumia kiasi kikubwa zaidi zha mtandao wangu 36.6GB kuliko programu nyingine yoyote.
Nadhani mada hii ilikuwa nzuri kwako, kama una njia nyingine ya kufuatilia utumiaji wa data katika Windows 10 tafadhali unaweza ukaiandika kwenye maoni hapo chini. Ahsante.
Ni wazi matumizi ya simu janja yameongezeka kwa kasi sana na kusababisha matumizi ya kompyuta kupungua kwa kiasi flani, lakini pia ni wazi kuwa kompyuta bado zinayo nafasi yake kubwa sana kwenye maisha ya kila siku hii ni kutokana na kuwa bado kuna mambo ambayo ni vigumu kuyafanya kwa kupitia kwenye simu zetu za mkononi. Ndio maana leo tumekuletea makala hii ya sheria ya 20 20 20 ambayo ni muhimu sana kwa afya yako kwa wewe mtumiaji wa kompyuta.

Wote tunajua matumizi ya kompyuta ya muda mrefu kuna wakati haya epukiki, iwe umeajiriwa au wewe ni mwanafunzi ni lazima utatumia kompyuta kwa muda mrefu kwa namna moja ama nyingine. Sasa matumizi haya ya muda mrefu husababisha matatizo mbalimbali kwenye mwili wetu kuanzia kwenye macho hadi sehemu nyingine za mwili kutokana na kukaa sana.

Baadhi ya matatizo au dalili zinazo patikana kwa kutumia kompyuta kwa muda mrefu ni pamoja na macho kuwa kama yanawaka moto au kuwasha, kichwa kuuma, kutokuona vizuri au kuona ukungu pamoja na matatizo mengine ya muda mfupi ambayo kwa ujumla wake  yamepewa jina la kitaalam la Computer Vision Syndrome, Kwa mujibu wa mtandao wa WebMD bado hakuna ushahidi kwamba utumiaji wa kompyuta kwa muda mrefu unaweza kusababisha upofu badala yake watafiti hao wamegundua kuwa unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ambayo ndio kwa ujumla wake yanaitwa Computer Vision Syndrome.

Lakini pamoja na hayo kuna njia za kujilinda usipate matatizo hayo, njia moja muhimu na inayo shauriwa na wataalamu wengi ni pamoja na sheria ya 20 20 20. Hii sio sheria mpya bali ni sheria inayotumiwa na watu wengi sana kwa sasa japo kwa hapa kwetu sidhani kama inatumika kwa upana wake kama inavyotakiwa. Sasa ili uweze kuelewa nitatumia mchoro hapo chini kuweza kukuelewesha na natumaini utaweza kufuata sheria hiyo rahisi itakayo saidia macho yako kuwa salama pamoja na kujilinda na Computer Vision Syndrome.

Sasa basi maana ya Sheria ya 20 20 20 ni kuwa, endapo una angalia kompyuta kwa muda mrefu, unatakiwa kupumzisha macho yako kila baada ya dakika 20 (ishirini) na wakati huo unatakiwa kuangalia kitu kilichopo umbali wa futi 20 (ishirini) kutoka mahali ulipo na unatakiwa kuangalia kitu hicho kwa sekunde 20 (ishirini). Hiyo ndio maana ya 20 20 20.

Sasa najua utaniuliza kwanini sekunde 20..? Kwa mujibu wa tovuti ya Healthline, macho hutumua sekunde 20 kuweza kupumzika kikamilifu hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unafuata sheria hii. Watalamu mbalimbali wa maswala ya macho duniani wana shauri sana sheria hii na ni muhimu sana kuhakikisha unaifuta pamoja na kupumzisha mara kwa mara macho yako hasa kwa wale wafanyakazi wa maofisini ambao huangalia karatasi nyeupe na baadae kuangalia kioo cha kompyuta.

Mpaka hapo natumaini utakuwa umefahamu sheria ya 20 20 20, hakikisha unatumia sheria hii maana ni kweli inasaidia sana na pia hakikisha unapata muda wa kupumzika au kumpizisha macho yako hii itakusaidia kiafya na pia kiutendaji.
As salaam aleikum mpendwa karibu tena, hapa huwa tunakutaka na Mkanganyiko mkubwa pale tunapotaka kuchagua kati ya aina hizi mbili za Windows 32-Bit au 64-Bit kwa sababu wengi wetu hatujui nini hasa tofauti zao. Baada ya kusoma makala hii utafahamu na utachagua chaguo sahihi kwa ajili ya kompyuta yako.


Mfumo endeshi wa Microsoft Windows unakuja katika matoleo tofauti tofauti na kila moja likiwa na kitu cha ziada zaidi ya mwenzi wake, na muda mwingine inakuwa ngumu sana kuona tofauti hizi. Mfano mzuri ni huu wa aina hizi mbili za Windows kati ya 32-Bit OS na 64-Bit OS inakuwa ngumu sana kwa mtumiaji wa kawaida kufahamu tofauti zake.
Microsoft walianza kuachia toleo la 64-Bit katika mfumo wao endeshi uliopendwa zaidi duniani na uliohudumu kwa zaidi ya miaka 14 Windows XP. Kwa mara ya kwanza 64-Bit ilianza kutumika katika mifumo endeshi na kampuni ya Cray mwaka 1985 ikiwa na mfumo endeshi unaofanana kabisa na UNIX – UNICOS. Baada ya hapo aina hiyo ya mifumo endeshi ilitapakaa katika Windows, Mac OS X, Solaris pamoja na Android kwa sasa.
Mifumo endeshi hii ya 32-Bit na 64-Bit inatengenezwa ili kuendana na aina ya Processor inayopatikana katika kompyuta husika, kwa maana hiyo inategemea na aina gani ya processor unatumia ili kuweza kutumia mifumo hii. 32-Bit Windows ilitengenezwa ili kuendana na 32-Bit Processor na 64-Bit hivyo hivyo ili kuendana na 64-Bit Processor. Kwa hiyo kabla ya kufanya chochote ni muhimu kufahamu tofauti kati ya aina hizi mbili za processor.

‘bit’ ni nini

Sehumu ndogo kabisa ya data katika kompyuta hufahamika kama ‘bit’ au kwa kirefu ‘binary digit’. Inafahamika kuwa kompyuta inaelewa lugha ya binary tu (lugha ya uwili) yaani ya  0 na 1 kwa hiyo kila bit inaweza ikawa na thamani ya 0 au 1. Kwa hiyo kompyuta huwa inahifadhi data katika makundi ya bit nane nane yanafahamika kama Byte au Octet, na makundi haya kadri yanavyozidi kuwa makubwa ndipo tunapopata Kilobyte, Megabyte, Gigabyte pamoja na Telabyte.

Processor ni nini

Processor au CPU ndio ubongo wa kompyuta, kwa maana nyingine processor ndio inafanya kila kitu katika kompyuta kuanzia kupiga muziki, kuangalia picha, kuvinjari katika mtandao pamoja na kazi zote za kompyuta kwa kutumia mahesabu ya 0 na 1 kama tulivyoona katika bit. Wengine huwa wanachanganya CPU na lile jumba linalobeba kompyuta (Computer case).
Ndani ya processor kuna vitu vinavyoitwa Regista na Logical sakiti, sasa hizi regista ndizo zinazosaidia katika kutunza data za ndani ya processor wakati processor ikiendelea na mahesabu ili kufanya shughuli fulani ya kompyuta. Kwa hiyo kuna ukubwa wa regista katika mfumo wa processor wa 32-bit ni 32-bit na hivyo kwa 64-bit ni 64-bit. Kwa hiyo kinachofanya tupate aina hizi mbili za processor ni Regista zilizomo ndani yake.
Kwa hiyo unaona kabisa 64-bit processor inaipa uwezo kompyuta wa kufanya mambo makubwa kwa sababu ina hifadhi kubwa katika ubongo wake (CPU) ukilinganisha na 32-bit processor.

Tofauti kati ya 32-Bit OS na 64-Bit OS

Mifumo endeshi ya Windows yenye 64-Bit ilitengenezwa ili kusapoti kiwango kikubwa cha RAM ukilinganisha na ile ya 32-Bit. Software kubwa kama Autocard, Photoshop, Cinema 4D pamoja na Magemu yanahitaji kiwango kikubwa cha cha RAM hasa inayotolewa na mfumo endeshi mpaka kufikia 16 exabytes. Kiwango cha RAM za kupachika kinachohitajika hutegemea sana na aina ya motherboard unayotumia.
Kiwango kidogo cha RAM kinachohitajika ili mfumo wa 32-Bit ufanye kazi vizuri ni 1GB wakati ule wa 64-Bit unahitaji 2GB na kuendelea.  Hii ipo wazi kwani 64-Bit ina regista kubwa hivyo kiwango kikubwa cha RAM kitahitajika. Kama unahitaji kupata matokeo mazuri kutoka kwenye kompyuta ya 64-Bit ni bora uwe na RAM inayoanzia 4GB na kuendelea na kwa wale wa 32-Bit ni bora uwe na RAM inayoanzia 2GB na kuendelea.
Kitu cha msingi unachotakiwa kufahamu ni kwamba 32-Bit Processor inafanya kazi vizuri tu katika kompyuta ya 64-Bit processor ila hautofurahia uzuri wa processor hii. Unachotakiwa kufanya ni kuweka 64-bit OS. Pia software na Drivers zinahitajika kuwa za 64-bit ili kupata kasi nzuri.
Tatizo kubwa la 64-Bit OS ni kwamba software nyingi zinagoma kufanya kazi na mifumo endeshi hii kwa sababu bado madeveloper hawajatengeneza software za kutosha katika soko zinazoendana na mfumo huu, lakini usihofu kwa sasa utapata software zote za muhimu za 64-bit, mfano Mozila Firefox wameanza kutengeneza kiinjari cha 64-bit hapo Desemba mwaka juzi.
Kwa ushauri, kama unaenda kununua kompyuta kwa sasa ni bora ukanunua ya 64-Bit ili kuendana na mazingira ya teknolojia yanayobadilika kwa kasi hivi sasa na ili kupata faida zaidi ya kile unacholipia.
K 
atika vitu vinavyokera zaidi kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta ni kitendo
cha PC yako kuwa slow. Kuna sababu nyingi zinasababisha kompyuta kuwa slow kama virusi, hardware specification pamoja na RAM kuzidiwa mzigo.Matumizi ya kompyuta hotofautiana sana kutoka mtumiaji mmoja mpaka mwingine kulingana na aina na shughuli inayofanyiwa. Kompyuta kwa matumizi ya kuchapa, kusikiliza muziki pamoja na kuangalizia muvi huwa hazihitaji hardware specifications kubwa ukilinganisha na kompyuta za kufanyia graphics na kuchezea games.
Mara nyingi watumiaji wengi wa kompyuta hulalamika kuwa kompyuta zao zimekuwa slow sana tofauti na hapo awali wakati wanazinunua. Kuna sababu nyingi zinazofanya kompyuta kuwa slow kama nilivyoeleza hapo juu inategemea sana na matumizi ya kompyuta husika.

Njia 7 za kuifuata kama kompyuta yako ipo slow sana

1. Weka Anti Virus
Moja ya sababu kubwa ya kompyuta kuwa slow ni uwepo wa virusi vya kompyuta. Virusi vya kompyuta vitatumia sehemu kubwa ya RAM na HDD katika kutekeleza majukumu yake. Hivyo ni muhimu kuweka anti virusi nzuri na nyepesi ambayo haitatumia kiasi kikubwa cha RAM.
2. Futa Temporary Files
Kwa watumiaji wa Windows unaweza ukafungua my computer=>Nenda local disk C: au disk yenye Windows=> Fungua Users => Chagua User kama jina la mtumiaji lipo => AppData=> Local=>Temp
Hapo unaweza ukafuta mafaili yote yaliyomo kwenye hilo folder la temp, kisha restart kompyuta yako.
3. Punguza vitu katika Hard Drive yako
Kujaa kwa Hard drive kunachangia sana kompyuta kuwa slow. Windows inatoa taarifa ya kukaribia kujaa kwa hard drive yako mapema sana pale tu inapokaribia kujaa na kuibadilisha rangi na kuwa nyekundu. Futa au hamisha baadhi ya vitu ili kuiacha kompyuta yako ikiwa na nafasi ya kutosha.
4. RAM ya kompyuta yako ni ndogo, ongeza RAM
RAM ni kiungo cha muhimu sana linapokuja suala la speed (kasi) ya kompyuta husika. Kiasi cha RAM hotofautiana kulingana na bei ya kompyuta. Angalia mwongozo wa RAM kulingana na mfumo endeshi wa kompyuta yako;
 • Windows XP kiasi kidogo cha RAM kiwe 1GB
 • Windows 7 kiasi kidogo cha RAM kiwe 2GB
 • Windows 8, 8.1 na 10 kiasi kidogo cha RAM kiwe 4GB
Ukiachana na RAM bado kuna vitu vingi vya kuzingatia hapa kama processor
5. Funga baadhi ya Programs kama unarun Programs nyingi kwa pamoja
Kama umefungua programu nyingi kwa pamoja katika kompyuta yako ni vyema ukafunga baadhi ya programu ili kuipunguzia mzigo kompyuta.
6. Update Windows yako (Mfumo endeshi)
Ni muhimu sana kuupdate windows yako kila updates zinapotoka sababu updates zinakuja na maboresho mengi hasa ya kuisalama katika kompyuta yako.
7. Punguza Add-Ons kwenye browser (kivinjari) yako
Wingi wa Add-on kam vile youtube downloader, ruler, games, znet hupunguza ufanisi wa kompyuta kwa kiasi kikubwa sana, hivyo hakikisha unaunistall baadhi ya add-on ambazo huzitumii mara kwa mara.
Ni muhimu sana kununua kompyuta inayoendana na shughuli zako ili kuepusha uzumbufu usio wa lazima.
Zipo sababu nyingi zinazoweza kupelekea computer kuwa slow Chache kati ya nyingi ni.

1. Udogo wa RAM

2. Udogo wa Processor

3. Ku-run program nying kwa pamoja

4. Ku-install program nyingi kwenye PC

5. Temporary files

JINSI YA KUTATUA TATIZO HILO.

1. Bonyeza windows button+R (kwa pamoja) then andika
%temp% then bonyeza ENTER. Yatakuja mafile na mafolder mengi bonyeza
CTRL+A then Bonyeza delete (del)

2. Bonyeza windows button+R (kwa pamoja) then andika temp
then bonyeza ENTER. Yatakuja mafile na mafolder mengi bonyeza CTRL+A then Bonyeza delete (del)

3. Nenda kweny my computer then local disk C then right click then chagua properties, then disk cleanup then iache icalculate kitafunguka ki-page kidogo weka tick upande wa kushoto then bonyeza ok. Itakuuliza are you sure you want to delete? Click yes then iache icalculate mpaka imalize then
funga.

4. Nenda kweny my computer then properties then advanced setting then advanced then setting (ya kwanza) then Advanced then change then utaona tick hapo kwenye automatically.

Toa hiyo tick then shuka chini kwenye custom then kwenye initial weka ukubwa wa ram yako mfano RAM yako ni 2 GB ichukue hiyo zidisha na 1024. (Hii inamaana GB1 ni MB1024) jibu utakalopata jaza hapo.

Then kwenye maximum chukua jibu ulilopatahapo juu lizidishe mara 2 then jaza hapo.(hapa unachokifanya ni kuifanya RAM yako itumike yote) Then bonyeza SET Then bonyeza apply then ok.

Itakuomba kurestat. Accept then bonyeza ok itazima itawaka tena kama hujui jinsi ya kuipata RAM yako nenda kwenye my computer then properties then angalia sehem wameandika

RANDOM ACCESS MEMORY(RAM) utaweza kuiona]
5. Epuka kujaza program nyingi ambazo huzitumii. Unistall
program ambazo hazina kazi.