JINSI YA KUJIUNGA NA SEEBAIT NA KUJIPATIA KIPATO KUPITIA BLOG/WEBSITE

Habari ndugu zangu katika tech leo tutazungumzia kuhusu kujiinua kiuchumi sisi kama blogger's, nalizungumzia hili baada ya kupata maswali na maoni kuhusu seebait kutoka kwa blogger's wenzangu hivyo tunatimiza Ahadi kama kawaida yetu, naam nisikupotezee wakati twende kwenye mada moja kwa moja.

Jinsi ya kujiunga na seebait hatua kwa hatua hatua ya kwanza ingia kwenye site ya Seebait.com kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Login/SignUp 
Itaonekana muonekano kama huu pichani
Itakuletea muonekano huo pichani , kwasababu sisi ndio tunahitaji kujipatia pesa kupitia Seebait.com basi tutaenda sehemu iliyoandikwa Select option you want to use kisha chagua mtandao unaohitaji kujisajili seebait kupitia mtandao ulioidhinishwa na seebai ambao ni Facebook, twitter na google+ hivyo nitakuonyesha kupitia google+ kwasababu bloggers wengi tunatumia google+
ukibonyeza google+ itakuomba idhini hivyo bonyeza Allow, 
Itakuwezesha kuingia katika dashibodi ya seebait kama inavyoonekana pichani kisha utucopy hizo code na kwenda kuzipaste kwenye blog yako
Katika dashibodi ya seebait walishakuelekeza sehemu ya kuweka , hivyo ingia kwenye blog yako bonyeza theme kisha edit Html, kisha search maneno haya <head> [ jinsi ya kutafuta code kwenye HTML bonyeza mouse yako mara moja kwenye code za templete yako kisha bonyeza Ctrl+F utaona sehemu ya kusearch  kisha paste code za seebait chini ya code hii <head>.  save tempalte yako.

kisha rudi kwenye website ya seebait.com bonyeza sehemu inayosomeka Properties , kisha bonyeza Add Property 

Utaona fomu kama hiyo hapo juu pichani jaza fomu hiyo kama hapa chini pichani
Hiyo picha hapo juu ni mfano hivyo jaza kutokana na mahitaji ya blog yako hakikisha hauvunji sheria za seebait.com, kisha ukimaliza bonyeza Submit
Ukisha submit itakuletea muonekano huo hapo juu kama umekidhi mahitaji ya seebait , lakini kuna vitu vitapungua kutokana na picha yangu ipo aproved lakini yako haitakuwa aproved kwasababu bado hajakubaliwa na kwenye status itakuonyesha not verify hivyo tumalizie hivi bonyeza sehemu yenye alama ya mshale ulioelekea chini unapatinaka upande wa kulia wa properties yako , utaidownload properties yako kupitia mshale huo, kisha ifungue kwa ku doble-click , itafunguka kupitia browser yako mimi nimetumia Chrome pichani hapa chini
Utaona code mfano wa hizo hapo juu sasa andaa code zako kwaajili ya ku verify akaunti yako ya seebait , pia seebait wameelekeza kuhusu kukamilisha hilo nenda juu kabisa kulia kwenye dashibodi ya seebait utaona alama ya magazine bonyeza hapo kisha tafuta Property Activation 
Utaona makala hiyo ya msaada wako imekuwa nambari moja bonyeza neno Read itafunguka makala kisha copy code hii <meta name="seebait" content="ACTIVATION CODE HERE" /> Kisha paste sehemu unayodhani utaweza kuiedit mimi huwa natumia notepad kisha irekebishe hapo kwenye neno ACTIVATION CODE HERE paste zile code za kwenye file ulilodownload kwenye properties hivyo code zako zitakuwa hivi <meta name="seebait" content="ryyady-bhay49d26e96ac7ebfc7c9t.html" /> Chukua code zako hizo ulizozitengeneza vema kisha nenda kapaste chini ya kwenye code hii <head> hii tulishazungumzia sehemu ya kuipata kwenye maelezo yetu hapo juu.

kisha rudi tena kwenye dashibodi ya seebait.com nenda kwenye properties kulia bonyeza alama ya TIKI au Nike utaona mabadiliko sehemu ya status itaandika Active. 

kufikia hapo umefanikiwa kuwa na akaunti ya seebait malizia kuweka matangazo kisha subiri seebait.com waipitie fomu yako ya maombi kama umekamilisha utakuta notification kwenye dashibodi yako ya seebait.com
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa sasa jitahidi kutafuta Traffic kwa nguvu ili upate pesa zaidi

Kidokezo

Jinsi ya kuweka tangazo ingia kwenye dashbbodi ya seebait kisha bonyeza Ad Spaces kisha bonyeza Add Ad Space 
Andika jina la tangazo, kwenye category chagua ukubwa unao uhitaji kisha bonyeza submit

kisha copy code sehemu iliyoandikwa space code kisha ka paste sehemu unayotaka tangazo lako lionekane kwenye blog yako. HONGERA UMEFANIKIWA

Bila shaka umefanikiwa kama umezingatia vema maelezo hayo, lakini kama hujaelewa usisite kuniachia maoni yako hapo chini wapi hujaelewa nami nitakusaidia haraka iwezekanavyo, maoni yako sio lazima yawe kuhusu swali kama umeelewa unaweza kuacha mtazamo wako hapo chini maoni yote ninayapenda muhimu usitumie lugha chafu. sambaza makala hii kwa marafiki ili tupate mwangaza wa mafanikio pamoja karibu sana

kama utahitaji kufanyiwa wasiliana nami whatsapp/call/sms namba 0717 101 085 nami nitakusaidia kukufanyia ila utachangia 10000

38 Comments

  1. Asante sana kaka makala iko poa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante pia kwa kutembelea matandao huu karibu

      Delete
  2. nice article,ipo very clear

    ReplyDelete
  3. aisee mi nafeli kwenye kutafuta neno property Activation haiji kitu zaid ya kuleta notification ya not verified. naomba msaada zaid

    ReplyDelete
  4. soma vema kwenye maelezo haya hapo juu >>> copy code hii meta name="seebait" content="ACTIVATION CODE HERE" Kisha paste sehemu unayodhani utaweza kuiedit mimi huwa natumia notepad kisha irekebishe hapo kwenye neno ACTIVATION CODE HERE paste zile code za kwenye file ulilodownload kwenye properties hivyo code zako Chukua code zako hizo ulizozitengeneza vema kisha nenda kapaste chini ya kwenye code hii head hii tulishazungumzia sehemu ya kuipata kwenye maelezo yetu hapo juu.

    ReplyDelete
  5. Hi nimeshafanya kila kitu na tayari bunner ya seebait inaonekana kwenye blog yangu ila kwenye acount yangu bado katika dashboard inasoma 0 impressions na kwenye notification ya kuwa approved kwenye status inaonesha not read.Je kuna shiada yoyote au iko sawa. Lakini pia mbadiliko ya kutoka kwenye bunner mpakwa kwenye matangazo mengine seebait ndio wanohusika na hayo mabadiliko au mmiriki wa blog?
    Nimekuwa Approved tangu 05/03/2017.Naomba msaada.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwanza hongera kwa kufanikisha kupata seebait kwa masaada wa makala hii. kuhusu kubadilika kwa ads ni kazi yao seebai pia kuhusu 0 impressions hii ndio itakayo kusaidia wewe kupata pesa jitahidi kutafuta watembeleaji zaidi kwaajili ya blog yako, na kwenye notification ya kuwa approved kwenye status inaonesha not read. hili wasiliana na seebait kupitia email yao hii support@seebait.com watakupa maelezo vema, Asante kwa kutembelea blog yetu washirikishe na marafiki

      Delete
    2. Me napenda kujua malipo yake ni kwa njia gn

      Delete
  6. Ahsante sana kwa msaada wenu

    ReplyDelete
  7. Nashukuru pia nimepata msaada kwa hiyo concern nyingine.

    ReplyDelete
  8. asante kwa msaada lkn nimejaribu account iko proved na matangazo hayaonekani kwenye blog nimewauliza wanasema' you have an error in your js. the meta tag should be out the scrip tag, sasa sielewi hapo nirekebishe vip ? naomba msaada plz

    ReplyDelete
  9. nenda katika pofile yako cpoy code kapachike katika html ya template yako kwenye code Head kisha download propeties yako kisha weka katika mfumo wa code ya activition kama nilivyoeleza hapo juu kisha kaweke code zako katika html kwenye Head kisha save template yako, refresh blog yako matangazo yataanza kuonekana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimefanya kama ulivyo eleza apo kwnye hii coments ila bado

      Delete
    2. Wenda ikawa ni template yako ndio tatizo ila kwa msaada zaidi wasiliana na seebait wenyewe kwa email yao support@seebait.com

      Delete
  10. inachukua muda gani mpaka kua approved

    ReplyDelete
  11. Kuhusu approval process inachukua kuanzia siku 1 mpaka 14 zakazi kutegemea na blog yenyewe ilivyo na idadi ya blog zinazohitaji msaada.

    ReplyDelete
  12. kuhusu ku verify inabidi uweke code ya activation vema kwa kuichanganya na property uliyodownload pasi na hivyo haiwezi kufanikiwa. na ukiiweka vema haiwezi kukataa ukiona imegoma ujue umekosea kuweka

    ReplyDelete
  13. nimejiunga frsh, baada ya fallback period tangazo halionekani tena .nimejaribu kila mbinu . nifanyeje?

    ReplyDelete
  14. Ahsante nimeweka code lakin banner inayotokea ni kama hii hapo juu yako ?

    ReplyDelete
  15. mm nimeshindwa kuzipaste hzo code kwenye html, kila nkipaste hazikubali.
    hv unapaste ndani ya kile kijumba cha head au wapi? na ni lazima upaste hapo tu?
    msaada tafadhali.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio ni lazima uweke katika sehemu ya head iweke mbele yake au chini yake

      Delete
  16. Not approved lakn status approved na nimepitia hatua zote hizi ads wanaanza kuweka siku hyo hyo au baada ya kuaprove

    ReplyDelete
    Replies
    1. matangazo yataanza kuonekana punde tu baada ya akaunti yako kuwa approved na status iwe active basi matangazo yataanza kuonekana

      Delete
  17. matangazo yataanza kuonekana punde tu baada ya akaunti yako kuwa approved na status iwe active basi matangazo yataanza kuonekana

    ReplyDelete
  18. Asante ndugu status hipo active bro kwa hivyo mpaka waipitie ndo inakua approve

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio mpaka waipitie, wakijiridhisha watai approve

      Delete
  19. Nashukuru kwa kuwa unajibu comments

    ReplyDelete
  20. kaka nimefanikiwa kuweka matangazo,lakin tangazo linaonekana tuu ninapoliweka kwenye ad banner ya headleft tena linaonekana kwa watumiaji wa desk top tuu, halionekan kwa watumiaji wa simu,, nikiweka sehemu nyingine hayaonekani kabisa, je tatzo ninni??

    ReplyDelete
    Replies
    1. blog yangu n www.mfangavo.tk

      Delete
    2. Shukrani kwa kuwa mwana familia wa swahili Tech, kuhusu jambo lako hilo hapo tatizo ni muonekano (template) wa blogger yako mfumo wa seebait haukubaliani na kila muonekano wa blogger ili kuonuesha matangazo ya aina mbili kwa wakati mmoja. Ivo jaribu kubadilisha template bila shaka itakubali

      Delete
  21. asante sana nimefanikiwa kujiunga na huu mfumo je tangazo ili lionekane mpaka seebait wenyewe waikague form

    ReplyDelete
  22. Asante sana Riyadi kwa maelezo mazuri,nimefanikiwa kuwa approved lakini ninajaribu kuweka matangazo kwenye blog lakini hayaoneshi tatizo linaweza kuwa ni nini? au kwa sababu nina matangazo mengine ya adsense? Msaada please

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wenda inaweza ikawa template yako haisapoti kuna baadhi ya template kama mageone toleo la 6 halisapoti jaribu kubadili muonekano kama hali itakuwa bado wasiliana na seebait support@seebait.com kwa msaada zaidi

      Delete
  23. blog yangu ina wiki moja tu je naweza kujiunga seebait?

    ReplyDelete
  24. kupanda kwa impression ya seebait ndi kwa shida sana mdau una impress 200 una vistor 500 unakuta visstors 1000 lakini impr bado hipo pale pale 200 kwanini mdau

    ReplyDelete
  25. Kaka kuna ani ya matangazo inaitwa 1×bet naiona kw baadhi ya mablogger wa tanzania cjuiii unaweza kutusaidi jinsi ya kujiunga nao, nakutueleza uzuri wake ukilinganisha na aina zingine za adsnetwork zilizopo bongo kama seebait

    ReplyDelete

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa