As salaam aleikum ndugu zangu wasomaji wa blog hii, kutokana na ombi la ndugu yetu Mfangavo kuhusu kujua jinsi ya kuweka sticky Ads basi nimeonelea niandae makala kamili ili tunufaike sote kwa pamoja wenda na wewe ulikuwa mmoja miongoni mwa watu waliohangaika kujaribu kufahamu jambo hili ila jitihada zako zikagonga ukuta, basi leo wacha nikupe suluhisho la jambo lako hilo kuwa makini katika usomaji wako ili upate kunielewa vema.

Hapa chini nimekuwekea code ambazo utaziweka katika blog yako katika upande wa Layout




<div style="left:0;position: fixed;text-align:center;bottom: 0px;width:100%;z-index:9999;"><center><a href="weka link ya tangazo lako">
<img src="weka code ya adsense hapa/ weka link ya picha ya tangazo lako">
</a></center></div>



Twende sawa sasa hizo code unazoziona hapo juu ndio code tutacazo zitumia katika kukamilisha jambo letu hili copy code hizo  kisha nenda katika Layout ya blog yako kisha bonyeza Add a Gadget kama uovyoona katika picha hapo chini
 Kisha chagua Gadget iliyoandikwa HTML/JavaScript kama unavyoona pichani hapo chini, hapo ndio tutakapozikweka code zetu
 Kisha utaona uwanja ambao hauna kitu pacte/pachika code zako ulizozikopi hapo juu kwenye sehemu ya Title usiandike kitu, edit/rekebisha code zako kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa save
 Shabbash mpaka kufikia hapo utakuwa umefanikiwa kuweka Tangazo mnato/mgando katika blog yako hata kama mtu atafungua post ataliona tangazo hilo kama unavyoona pichani hapa chini


Bila shaka nimejitahidi kurahisisha katika kuelezea Jambo letu hili kama utakuwa kuna sehemu hujaelewa basi unaweza kuniachia maoni yako hapo chini nami nitajitahidi kukusaidia kadri nitakavyoelewa

makala hii Imeandikwa na Riyadi Bhai Sambaza kama Ilivyo kama unahitaji kukopi makala zetu zilizopo katika blog hii wasiliana nami kwa email RiyadiBhai@gmail.com