FAHAMU JINSI YA KUTAMBUA KIWANGO CHA DATA KINACHOTUMIKA KATIKA WINDOWS 10

Katika kufuatilia utumiaji wa data katika Windows 10 wengi tunatumia “Windows Task Manager”, lakini ukweli ni kwamba Windows Task Manager inaonyesha matumizi ya data ya application za msingi za Windows. Fahamu jinsi ya kufuatilia utumiaji wa data wa programu zote katika Windows 10.
Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Windows 10 utakuwa umegundua ni kwa jinsi gani programu hii endeshi kutoka Microsoft inavyokula kiwango kikubwa cha data au MB kama tunavyoita tulio wengi. Wengi huwa wanalalamika watoa huduma za kimtandao wao (ISPs)  wanawaibia kwa sababu tu kifurushi alichojiunga kimeisha mapema wakati hajafanya chochote.
Katika kompyuta zetu kuna programu mbalimbali zinazofanya kazi kwa kutumia mtandao bila ya sisi kufahamu na wengi wetu tumekuwa tukijaribu kuangalia ulaji wa data kwa kutumia Windows Task Manager,  lakini ukweli ni kwamba sio matumizi yote ya data katika kompyuta yako yanaoenekana katika Task manager.
Mfano mimi huwa natumia Skype, Mozilla,Games na kuangalia Movies mtandaoni na hapa ndipo napoona umuhimu wa kufuatilia utumiaji wa data katika kompyuta yangu. Hebu tuangalie njia rahisi za kujua kiwango gani cha data unatumia katika kompyuta yako na jinsi ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya data.

Njia za kufuatulia utumiaji wa data katika Windows 10

Kuna njia kuu mbili,
  • Kwa kutumia application za bure za kufuatilia matumizi ya data
  • Kwa kutumia Windows Task manager

Tumia application ya bure ya Free Network Usage katika Windows 10

  • Fungua sehemu ya kutafuta (Search) katika windows 10 na tafuta neno “Network Usage” katika sehemu ya kutafuta.
  • Fungua tokeo la juu kabisa lililoandikwa Network Usage kama inavyoonekana katika picha na windows itakupeleka katika ukurasa wa kupakua programu hii, bonyeza kitufe cha free kilichopo chini ili kushusha programu hii.
  • Mara baada ya kupakua programu hii itafunguka kama inavyoonekana katika picha chini na kuanza kufuatilia matumizi yako ya mtandao
  • Upande wa juu kushoto kuna kitufe cha Settings na utaweza kupangilia jinsi programu hii itavyokuwa inafanya kazi.
Programu hii ni nzuri kwa wale wanaotaka kujua kiwango cha data alichotumia mwezi uliopita au mwezi uliopo ili uweze kulipa na kupanga bajeti zako, ila kama unataka kufuatilia kiwango cha data katika kila programu ndani ya windows 10 tafadhali fuata njia ifuatayo.

Jinsi ya kuangalia matumizi ya data kwa kutumia Task Manager

  • Kufungua Task Manager kiurahisi bonyeza Ctrl+Shift+Esc, au unaweza ukaright click kwenye Taskbar na chagua Task Manager
  • Bonyeza sehemu iliyoandikwa Application History katika vitufe vya juu vya Task Manager
Hapo utaweza kuona matumizi ya data kwa application za msingi za windows lakini applications kama Kivinjari chako (Web Browser), Skype na Games hutoweza ziona hapo. Haileweki kwa nini Microsoft aliamua kufanya hivyo, usihuzunike ngoja tuangalie njia mbadala ya kufanya hivyo.
  • Fungua Windows 10 Settings na chagua Network and Internet
  • Baada ya kufunguka chagua Data Usage katika kipengere cha Network and Internet, alafu fungua Usage Details
Baada tu ya kufungua, kidirisha kingine cha windows kitafunguka na hapo ndipo utaweza kuona applications nyingine tofauti na zile za msingui za windows. Kama unavyoona katika picha Chrome imetumia kiasi kikubwa zaidi zha mtandao wangu 36.6GB kuliko programu nyingine yoyote.
Nadhani mada hii ilikuwa nzuri kwako, kama una njia nyingine ya kufuatilia utumiaji wa data katika Windows 10 tafadhali unaweza ukaiandika kwenye maoni hapo chini. Ahsante.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa