TRENDING NOW

As salaam aleikumndugu zangu kutokana na kila mmoja anakuwa na sheria zake kwaajili yake na watu wake binafsi nimeanzisha blog hii kwaajili ya kuwasaidia watu wa aina zote zaidi blogger's hasa wanaotumia lugha ya kiswahili lakini kwa masikitiko makubwa nimeona sheria zangu zikivunjwa wazi kabisa jambo ambalo likanatisha tamaa kuendelea kufanya mambo makubwa zaidi, nimeweka sheria kwa wale wanao kopi makala zangu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html nimeweka masharti rahisi sana katika sheria hiyo lakini watu wamekuwa wagumu kuelewa.

mpaka umeamua kukopi makala kutoka sehemu moja kupeleka kwako bila shaka umefahamu ni ugumu kiasi gani kuandaa makala mpaka ikiwa na msaada kwa watu wengine hivyo ili tusivunjane moyo katika kusaidiana naomba tujitahidi kufuata sheria za blog hii kwani sifanyi ili kupata pesa lakini nafanya hapa ili kuwasaidia watu wengine kama unahitaji kukopi makala kutoka katika blog hii soma hapa kabla ya kukopi https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html soma sheria za huduma zangu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/terms-of-service.html soma sheria mama za mtandao huu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/privacy-policy.html kama unamalalamiko soma hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/blog-page_29.html kama utakubaliana na sheria hizo basi wasiliana nami hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/contact.html
Kampuni ya Simu ya Airtel Afrika pamoja na kampuni ya kuwezesha kutuma na kupokea pesa nje na ndani ya nchi ya Western Union, hivi karibuni zimetangaza ushirikiano wa pamoja ambao utawawezesha wateja wa Airtel Money kuweza kutuma na kupokea pesa kutoka nje ya nchi kwa kutumia huduma za Western Union.

Huduma hiyo itawaruhusu watumiaji kutuma na kupokea fedha kutoka akaunti zao za Western Union kwa kutumia akaunti zao za Airtel Money. Mbali na hayo wateja wa Airtel Money wataweza kutumia pesa hizo kulipa bili, kununua muda wa juu wa maongezi, na kutuma pesa ndani na nje ya nchi kwa urahisi.

Pia watumiaji wa huduma za Western Union kote duniani, wataweza kutuma pesa moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mtumiaji wa huduma za Airtel Money kupitia huduma za kidigital za Western Union ambazo zinapatikana kwenye nchi zaidi ya 75, kupitia kwa mawakala zaidi ya 200 ambao wanapatikana kwenye nchi hizo.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini huduma hii itanza kufanya kazi rasmi kwa hapa Tanzania, lakini kwa mujibu wa tovuti ya Twistarticle ni moja kati ya nchi zitakazopata huduma hiyo ikiwa pamoja na nchi nyingine za Afrika kama vile Nigeria, Uganda, Gabon, Zambia, DRC, Malawi, Madagascar, Kenya, Congo, Niger, Chad, Rwanda pamoja na Visiwa vya Shelisheli.

Airtel Tanzania itakuwa ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano kwa hapa Tanzania, kuungana na Western Union kwa ajili ya kurahisisha kutuma na kupokea pesa kutoka nje ya nchi kwa gharama nafuu na kwa urahisi zaidi kwa kutumia simu za mkononi. Ili kujua jinsi ya kujiunga na huduma hii endelea kutembelea Tovuti ya Swahili Tech kila siku tuta kuhabarisha zaidi.


Kuanzia tarehe 8/4-14/4 2019 simu za Infinix zitakuwa katika punguzo la bei kupitia soko la mtandaoni lifahamikalo kama Jumia na punguzo hili kufanyika kwa wiki moja ya JUMIA MOBILE WEEK. JUMIA MOBILE WEEK ni wiki madhubuti kwajili ya kuuza simu kwa bei ya punguzo, na safari hii simu za Infinix ikiwamo Infinix ZERO 6 na Infinix HOT 7 ni miongoni mwa simu zitakazopatikana kwa bei ya punguzo. Jumia mobile week imeanza rasmi tarehe 8/4-14/4 2019.
Infinix Mobile Tanzania inatumia nafasi hii kuingiza simu za Infinix katika JUMIA MOBILE WEEK ikiwamo simu zilizoingia sokoni mwishoni mwa mwezi wa tatu kwa dhumuni la kufanya kila mtanzania aweze kuhamia katika ulimwengu wa kidijitali, ulimwengu unaoaminika kuwa suluhisho hata kwa yale yanavyoshindikana kufanyika kwa muda mfupi. 
Na ukiondoa matumizi ya simu kuwa kwajili ya mawasiliano tu lakini Infinix inatambua umuhimu wa simu hasa kwa matumizi ya kujiongezea kipata mfano Infinix ZERO 6 kupitia uwezo wake wa kamera unapata picha sasa hii kuwa ni chombo cha biashara.  sifa kuu ya Infinix ZERO 6 ni kamera, Infinix ZERO 6 imewekwa nguvu nyingi upande wa kamera  nyuma ikiwa na MP 12+MP 24 zenye kupiga picha/picha jongefu na mng’ao  wa hali ya juu sana, na kamera ya mbele ni MP 20. Katika kuhakikisha Infinix ZERO 6 inakupa picha yenye uhalisia ya mazingira husika ndipo teknolojia ya Artifficial Intelligence inapofanya kazi yake.Kwa asilimia 100% Infinix ni kampuni yenye kujali wateja wake pamoja yakuwa Infinix HOT7 inapatikana kwa bei chee katika maduka ya Infinix lakini bado ni miongoni mwa simu zilizopo katika jumia mobile week. Infinix HOT 7 inasifika kwa kupiga muziki mzuri na hii ni kutoka na DIRAC MODE iliyopo ndani ya Infinix HOT 7. 
Na kwa simu yoyote ya Infinix utakayonunua ndani ya mobile week itakuwa na warranty ya mwaka mmoja. 


As salaam aleikum mpendwa msomaji wa ukumbi huu makini kuhusu uchambuzi wa masuala ya Tech, wenda ilishawahi kukutokea unahitaji kununua simu lakini haujui ni vitu gani vya kuzingatia basi leo Riyadi Bhai nimekuwekea vitu vya msingi ambavyo unatakiwa kuvizingatia kabla ya kununua simu mpya
● Battery
Fikiria: Wewe ni mtumiaji ambaye una apps nyingi na kuzifungua wakati huo huo? Je! Unajiona kuwa mtumiaji mkubwa wa apps za video au kucheza games? Matumizi makubwa kwenye mtandao hufanya kupunguza betri kwa kasi. Ikiwa wewe ni wa mtumiaji mkubwa, basi ni bora kwenda kwenye simu yenye battery yenye kutunza chaji.

● Memory
Simu za mkononi zina aina mbili za memory - Random Access Memory(RAM) na Read Only Memory (ROM). RAM, pamoja na processor ya simu yako (angalia chini), huamua kasi ya simu na urahisi wa kuitumia. ROM kama watu wengi tunavyojua kuwa uwezo wa kuhifadhi. Hii ni memory ambayo hutumiwa kuhifadhi programu za OS, apps na video zote, picha na nyimbo ambazo unataka kuhifadhi kwenye simu.Hivyo, nasisitiza kuwa simu zenye RAM kubwa zitakuwa na kasi zaidi na wale walio na ROM kubwa watahifadhi vitu vingi zaidi. Mtumiaji wa wastani hili kufurahia simu yako unapaswa kuwa na 2 GB RAM na 16 GB ROM. Lakini kama wewe ni mtumiaji mkubwa, nenda kwenye simu yenye angalau 3-4 GB RAM na 64GB ROM. Kuongeza ROM yako unaweza kutumia micro SD, lakini kumbuka, sio simu zote unaweza kuweka micro SD.

● Camera
Kuna aina nyingi za vitu vinavyozunguka camera na kufanya iwe bora. Kuna kampuni za simu zinazojaribu kutoa megapixels zaidi mfano kwasasa simu nyingi wanaweka 20MP - 48 MP wakati inaweza pitwa na simu yenye 16 MP kwa ubora wa picha. Usiruhusu hii iwe sababu ya wewe kuwa mjinga. Kwani kamera yenye megapixels zaidi haina matokeo ya picha bora kama tunavyodhani. Mbali na megapixels, picha nzuri ni kazi ya vitu kama ISO standard, kasi ya autofocus. Ukiwa ni mpenzi wa kupiga picha nyingi, inakupasa uende kwenye simu yenye kamera ya 12 au 16 MP ambayo ina aperture ya f / 2.0 au chini, kwa picha bora hata kwenye mwanga mdogo. Ikiwa matumizi yako ya kamera hayawezi kuwa makubwa, simu yenye kamera ya 8-12 MP na aperture f / 2.2 itafaa kwa matumizi yako.

● Processor
Kama vile kwenye upande wa kamera za simu,kuna vitu vingi vinachangia processor iwe na nguvu. Simu nyingi zina Snapdragon, MediaTek nk. Angalia kasi ya processor ambayo imeelezwa kwa GigaHertz (GHz) simu ikiwa na processor nzuri utaweza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.

● Display
Simu iliyo na display ya 5.5 - 6-inch HD au QHD ni chaguo bora. Hii itakuwezesha kufurahia ubora wa muonekano wa screen pia inakuwa rahisi kuishika na kuiweka katika mfuko wako.

● Operating System
Hapa napendelea Android, pia angalia UI na hiyo Based Android OS. Kama haupendi mbwembwe nyingi chukua Android Stock (Android One). Pia kuna baadhi ya hizi Stock firmware zinazokuja na simu zinakuwa na bloatware, na hivyo kupunguza ROM na RAM ya simu. Kwa hiyo, jaribu kuangalia hili kabla ya kufanya uamuzi.

● Cost
smartphones huja kwa bei ambazo hutofautiana sana. Ni wazi, bei zinatokana na specs, simu yenye specs za juu thamani yake huwa juu pia kwa mfano: processor, memory, camera na display.Lakini usiruhusu bajeti yako ikuzuie kununua smartphone bora unayotaka, unaweza kujichanga hata miezi mitatu upate kitu bora zaidi.

Kwa uelewa wangu hivyo ndio vitu muhimu vya kuzingatia.
As salaam aleikum ndugu msomaji wa ukumbi huu bila shaka kama wewe ni mtumiaji wa computer utakuwa ushawahi kukutana na hadha kama hii ya kutaka software fulani lakini hauna pesa hivyo ukaamua kuingia google lakini ukaishia kukutana na Trial version
Basi leo nikupe ujanja wa kumalizana na issue hiyo Njia moja unaweza kulikwepa hili ni kuacha kusearch free software kwenye google na badala yake search open source

Mfano kama unahitaji internet downloader manager


Usitafute “Free internet downloader manager” kwenye google search, na badala yake tafuta  “Open source Internet downloader manager”.

hapo utakutana na kile unachokitaka hii ni njia rahisi sana je unanjia nyingine unayoijua funguka nasi katika sanduku la maoni


Njia gani wewe unatumia kupata free softwares?
As salaam aleikum ndugu wapendwa wasomaji wa Jukwaa hili ni wakati mwingine tena wa kupeana mawili matatu, wenda imeshawahi kukutokea katika pitapita zako katika mitandao ya kijamii ghafla ukatua facebook ukakutana na video ambayo imekuvutia kisha ukashindwa kuipata kutoka na kutokufahamu jinsi ya kuipakua video hiyo, basi leo nimekuletea njia ya kukuwezesha kuishusha video yeyote kutoka facebook bila usumbufu wowote twende sawa hapa chini nimekuwekea maelezo kamili.

kwanza kabisa pakua App ya Fb Video Downloder hapa

kisha fuata hatua hizi ili kushusha video yeyote
fungua app yako ya Fb video downloder kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa GO TO FB Kisha log in katika facebook akaunti yako
kisha tafuta video unayihitaji kuishusha kutoka facebook kisha iguse au ibonyeze hiyo video
utaona option kama inavyoonekana pichani hapo juu kama unahitaji kuiangalia kabla ya kuishusha bonyeza sehemu iliyoandikwa Stream kama unahitaji kudownload bonyeza sehemu iliyoandikwa download
kama utahitaji kuona idadi ya video ulizopakua kupitia app ya Fb Video Downloader bonyeza sehemu iliyoandikwa Gallery
hapo utaona video zako zote pia zitakuwa zimehifadhiwa katika memory ya simu 
Mpaka hapa utakuwa umeshafahamu jinsi ya kupakua video za facebook kama unaswahili kuhusu makala hii unaweza kuniuliza katika sanduku la maoni nami nitakujibu kwa haraka zaidi Enjoy
As salaam aleikum Yawezekana umewahi kusikia kuhusu teknolojia ya Wi-Fi na pengine na wewe ni miongoni mwa wanaotumia teknolojia hii. Kama hujui, hii ni teknolojia inayokuwezesha kupata intaneti kwenye simu yako ya mkononi, tablet, kompyuta au vifaa vingine vyote vinavyotumia intaneti.

Kwa kutumia Wi-Fi, unaweza kutazama video mtandaoni, unaweza kusikiliza muziki, kuingia kwenye mitandao ya kijamii, Instagram, Facebook, WhatsApp, Snapchat na mitandao mingine kibao. Kwa kifupi, unaweza kufanya kila kitu kinachohusianana intaneti bila kuwasha ‘data’ kwenye simu yako.

Unachotakiwa ni kuwa tu sehemu yenye Wi-Fi, kisha unaji-connect kwa kupitia simu yako au kifaa chochote kinachotumia intaneti na unaendelea kuperuzi kwenye mitandao kwa kasi kubwa pengine kuliko ukitumia ‘data’, kutegemea na uimara wa Wi-Fi mahali ulipo.

Wakati Wabongo wengi ndiyo kwanza wameanza kuishtukia teknolojia hii na kuanza kuitumia kwa kasi, kwenye maofisi mengi kukiwa kumefungwa vifaa maalum vya kukuwezesha kupata Wi-Fi bila chenga, nchi za wenzetu tayari kilishakuwa kitu cha kawaida sana na yapo baadhi ya majiji ambayo unapata Wi-Fi ya bure popote ulipo!

Kwa jinsi dunia inavyokwenda kasi, wakati sisi ‘tukihangaika’ na Wi-Fi, tayari wanasayansi kwenye nchi zilizoendelea, wamegundua teknolojia mpya, yenye kasi ya zaidi ya mara mia moja ya Wi-Fi ya kawaida.

Teknolojia hii inaitwa Li-Fi (Light Fidelity) na tofauti na Wi-Fi inayotumia mawimbi ya radio (radio waves), Li-Fi inatumia mawimbi ya mwanga (Light Waves).

Kinachofanyika ni kwamba, taa maalum (LED Light) ndizo zinazotumika kusambaza mawimbi ya Li-Fi na watu waliopo ndani ya eneo ambalo mwanga wa taa hiyo unafika, wanakuwa na uwezo wa kupata intaneti yenye kasi kama ya mwanga! Yaani hata kama video ni kubwa kiasi gani, ukitaka kudownload, unagusa tu na ndani ya sekunde chache kazi inakuwa imeshakwisha.

Taa hizo huwa zinaunganishwa na kifaa maalum ambacho ndicho kinachopokea intaneti kutoka kwenye satelite, kisha kinaibadilisha kwenda kwenye mawimbi ya mwanga na kuisambaza kupitia taa hizo, ambazo zinatakiwa kuwashwa muda wote ili kupata intaneti. 
Kasi ya Li-Fi, ni 224 gigabits/seconds na kama nilivyokueleza, ni zaidi ya mara 100 ya Wi-Fi ya kawaida. Mgunduzi wa teknolojia hii ni Profesa Harald Haas wa Chuo Kikuu cha Edinburgh nchini Uingereza na tayari imeshafanyiwa majaribio nchini Uingereza, Marekani, Dubai na maeneo mengine duniani.

Changamoto kubwa ni kwamba, ili kuwahudumia watu wengi zaidi, taa zinatakiwa kuwa nyingi na zinatakiwa kuwashwa muda wote, hata mchana. Pia Li-Fi haina uwezo wa kuvuka ukuta, taa ikiwashwa ni wale tu waliopo ndani ya eneo mwanga unapofika ndiyo watakaopata intaneti.

Ili kukabiliana na tishio la Li-Fi inayoonekana kama itakuja kuliua soko la Wi-Fi, Kampuni inayotoa huduma za Wi-Fi ipo mbioni kuanza kutumia teknolojia mpya iitwayo Wi-Fi HaLow ambayo nayo itakuwa na kasi kubwa zaidi ambayo hata hivyo, bado haitaifikia Li-Fi.

Tayari makampuni makubwa kama PureLiFi, Lucibel, Icade na Phillips pamoja na Jeshi la Marekani yameongeza nguvu na kuanza katika project hiyo kubwa na kuanza kutengeneza vifaa vyenye uwezo wa kupokea mawimbi ya Li-Fi na matarajio ni kwamba mpaka ikifika 2020, Li-Fi itakuwa imesambaa dunia nzima.
As salaam aleikum wapendwa baada ya kupotea kutokana na maswala ya kujitafutia mkate wa siku leo nimerudi tena kwaajili yako karibu sana katika blog inayojaribu kukutatulia mambo yako ya kiteknolojia kwa mapana zaidi leo tugusie suala zima la kuwepesisha kupakua file za torent kwa speed kubwa zaidi kwa kutumia IDM yaani Internet Download Manager 

Watu wengi wamekuwa wakitumia torrent clients ( kama u-torrent, bittorrent, vuze etc) kwa ajili ya kupakua movies na apps zenye file kubwa kutoka kwenye torrents sites mbalimbali lakini huwa kunakua na changamoto ya speed kuwa ndogo unapokua unapakua file hasa lenye seeders wachache ....ili kuepukana na changamoto hyo leo ntakujuza njia ya kupakua files kwa kasi zaidi;

1. kwanza kabisa  unatakiwa uwe na internet download manager (IDM) kama hauna download hapa bure kabisa DOWNLOAD

2. Link internet download manager na browser unayotumia mimi huwa natumia chrome unaweza kupakua chrome browser hapa DOWNLOAD

3.Unatakiwa ufungue account kwenye website inayoitwa www.seedr.cc ambako utapewa disk kama 2gb ( ila inaweza kufikia 5GB ukifanya sharing na rafiki zako kupitia referral code yako) 4.Ukishafungua hiyo account utakwenda kwenye torrent site unayopendelea either rarbg.to , katcr.co , limetorrent.cc 13377x.to etc5 . Copy magnet link ya file kama unavyoona katika picha hapo juu unalotaka kudownload na paste kwenye seedr.cc 


account kuna sehemu imeandikwa paste, kisha bofya kitufe cha jumlisha 

na file lako litaundwa na utaona mshale wa kupakua ukiweka mouse yako katika folder lililoundwa angalia picha hapa chini
na utaweza download kwa kasi nzuri sana ambayo ni tofauti kabisa kama ungetumia utorent

asante kwa kusoma makala hii sambaza upendo kwa washkaji kwa kushare makala hii karibu tena
UKIANGALIA katika simu yako ni dhahiri Application nyingi ulizopakua ni za bure. Wote tunapenda App za bure.

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako.

Wengi wetu tumekuwa hatusomi vigezo wakati tunapoingiza App hizo ndani ya simu zetu, huwa tunabonyeza tu ‘agree to continue’ bila kusoma.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUS aina ya TROJAN

Virusi hao ambao hutumia majina tofauti-tofauti wana uwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa hackers (wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zina uwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing) ambapo ukijichanganya tu, basi taarifa zako za siri kama bank details, email, password (nywila au neno la siri) zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa wadukuzi.

Credit : JF