Articles by "Adsense"
Showing posts with label Adsense. Show all posts
As salaam aleikum ndugu zangu kwa wale blogger wa kongwe na wale wachanga ni kipindi kirefu tumesikia kuhusu neno adsense lakini kumekuwa hakuna Tija ya kulisikia tu neno Adsense, sababu hata baada ya kulisikia na kulijua kumekuwa ni vigumu kunufaika nalo kutokana na masharti yao.
Leo katika uchambuzi huu tuelewe kwanini Tunafikiri adsense wanaweza kukiweka kiswahili kati ya lugha zinazosapoti katika matangazo yao? 

Katika masiku ya hizi karibuni kampuni ya google imeboresha mtandao wake na huduma zake zote kwa ujumla kama kubadilisha muonekano wa dashbodi ya blogger.com, adword, adsense, youtube, google map, na hata adsense pamoja na mfumo wa upakiaji app wa google console, Lakini ukiangalia kipaumbele walichokipa kiswahili katika program zao ni kubwa mno kwa wale watumiaji wa google translate watakuwa wameona hili.

Kwa sasa lugha ya  Kiswahili imepata pendeleo la kutafsiriwa bila hata kuwa na muunganisho  wa data,hii ni fursa nzuri hasa pale utakapokuwa huna kifurushi.

Na kwa upande wa adsense ilikuwa kipindi cha nyuma ukifungua blog kisha kabla hujaifikia dashbodi ya blog ukachagua lugha ya kiswahili ndio iwe lugha mama ya blog yako google walikuwa wanakiondosha kipengele cha mapato katika blog yako.
 Lakini kwasasa kipengele hicho kinawekwa na google wenyewe hata kama utafungua blog yako kwa lugha ya kiswahili mwanzo mwisho, hii ni wazi siku za usoni blogger wanaotumia lugha ya kiswahili katika kuendesha blog zao wataanza kunufaika na adsense.

Hayo ndio machache kati ya mengi tuliyokuandalia siku ya leo endelea kuwa nasi ili kufahamu zaidi kuhusu ADSENSE
As salaam aleikum wapendwa karibuni tena katika blog yetu tuendelee kupeana maujuzi ya kuturahisishia mambo yetu, kipindi cha nyuma niliandika makala jinsi ya kupokea pesa zako kutoka adsense kupitia wire transifer ( njia ya kibenki) unaweza kuisoma hapa :[ Jinsi ya kupokea pesa zako kutoka adsense kupitia bank] leo tuangalie njia hii ya pili ambayo baada ya kuitumia nimegundua kuwa ni bora na ni nafuu zaidi ya bank.

kabla hatujaendelea wenda kuna ndugu zetu wengine hawajui hata Adsense yenyewe ni nini soma hapa [ Jinsi ya kupata pesa kupitia Adsense ]

haya sasa tuendelee na mada yetu hii kwanza kabisa fahamu jinsi ya kuweka namna ya kupokea mapato yako kupitia Western Union ingia katika akaunti yako ya adsense
upande wa kushoto wa dashibodi ya adsense bonyeza sehemu iliyoandika setting kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Payment
kisha utabonyeza sehemu imeandikwa manager payment kisha ongeza au chagua western union kisha ifanye kuwa ndio Primary sasa rudi katika payment

Kama utaona muonekano kama huo pichani basi umefaulu sasa tuangalie vipi utaweza kuzishika pesa zako mikononi baada ya kufikia U$D 100 ambacho ndio kiwango cha adsense kuwalipa watumiaji wake.
Bonyeza hiyo sehemu iliyoandikwa View Transactions kisha tazama muamala wako kisha ubonyeze itafunguka new Tab itakuonesha kila kitu 
hapo ndio ilipokuwa pesa yako hizo ndio vitu vya kuandika sehemu au kama utaenda na kifaa chako katika bank/ofisi inayotoa huduma za western union

vitu vya kuzingatia wakati unaenda katika ofisi za western union kuchukua pesa yako ni lazima uende na na moja kati ya hivi: Passport ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha kitaifa au cha mpiga kura na lazima kiwe chako wewe mwenyewe.

ukifika kuna karatasi utatakiwa kujaza majina yako ya utakayoyajaza lazima yafanane na ya katika kitambulisho chako na akaunti yako ya adsense, sehemu ya swali jaza namba zilizopo katika ID Billing tazama hapo pichani utaziona katika sehemu ya mtu anayekutumia jaza Google Ireland Limited.

Ukishafika kwa mtoa huduma mpe hiyo karatasi na kitambulisho chako kati ya ivo nilivyokuorodheshea hapo kwenye maandishi mekundu.

mpaka hapo utakuwa umekamilisha kuchukua pesa yako sasa furahiya, bila shaka umepata mwangaza kidogo kama sio sana lakini kama kuna sehemu hujaelewa niachie swali lako katika sehemu ya maoni nami nitakujibu kwa kadri nitakavyokuelewa. shukrani kwa kuwa nami mwanzo mpaka mwisho sambaza makala hii kwa ndugu na jamaa ili nao wafaidike

NB
Kwa wale wazee wa kukopi na kupaste naomba usome hapa kabla hujakopi makala za kwenye blog hii 
Habari tena karibu hapa tujuzane haya na yale baada ya kufahamu jinsi ya kujiunga na seebait kama ulipitwa soma hapa Jinsi ya kujiunga na seebait kutokana na maoni na maombi ya wasomaji wangu nimeona nitimize haja za wasomaji wangu kwa kuwafahamisha kuhusu kujisajili na adsense je unajua adsense ni nini soma hapa jinsi ya kupata pesa kupitia adsense 

Tukumbuke kila kitu kina sheria zake na utaratibu wake hivyo ni vema kufamu kuhusu sheria na sera za google , kwanza fahamu ya kuwa adsense hawasapoti lugha ya kiswahili kufahamu zaidi soma hapa sababu za kiswahili kutokubaliwa katika mfumo wa adsense hivyo ikiwa unaweka machapisho kwa lugha ya kiswahili katika blog yako ni vigumu kukubaliwa.

baada ya kufahamu hayo machache nafikiri tuanze lakini unaweza kuniachia maoni yako kama hujaelewa maelezo yanguIngia katika blog yako kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa ernings
Utaona sehemu imeandikwa Sign Up for adsense kama huoni na unatumia domain kama SwahiliTech.Net ingia hapa https://www.google.com/adsense/signup watakuletea chagua hili 
bonyeza sign in kama umetumia link watakuletea sehemu ya kujaza website yako na lugha lakini kama umetumia blogger moja kwa moja sehemu ya website watakujazia kisha wewe utajaza lugha
lugha zote watakazokuletea hapo zinasapoti mfumo wao kwahiyo ni chaguo lako hapo ila mimi huwa nachagua kiingereza baada ya kuchagua lugha bonyeza Accept association watakuletea muonekano huu
utajaza form hiyo kama wanavyokuomba namba ya simu time zone sehemu ulipo yaani nchi na mkoa jina n.k kisha utasubmit chini kabisa ya hiyo fomu kisha watakuletea muonekano kama huu chini pichani
Bonyeza hapo Continue watakurudisha kwenye dashibodi ya blog yako sehemu ya ernings utaona ujumbe kuwa adsense yako ipo kwenye mchakato itakuwa aproved baada ya muda kidogo, hivyo wataiangalia kama umekidhi vigezo na mashariti yao watakukubalia ndani ya siku tatu na utaona muonekano huu kama utakuwa umekubaliwa
mpaka hapo utakuwa umefanikiwa na kuhusu kupokea pesa zako soma hapa Jinsi ya kupokea pesa yako kutoka adsense mpaka hapo nafikiri utakua umepata muangaza japo kidogo natumaini makala yangu haijakamilika ila wewe  unaweza kuikamilisha kwa kuniuliza swali hapo kwenye coment nami nitakujibu ili tukamilishe makala hii, pia sambaza upendo kwa blogger wenzetu kwa kusambaza makala hii nao wajipatie ujuzi huu bure, nimekufahmisha bure basi nawe toa bure
Habari na karibu katika ukumbi huu maridhawa kwaajili yako , kutokana na maombi ya baadhi ya wasomaji wangu kuhitaji kufahamu jinsi ya kupokea pesa zao kutoka adsense leo nimeonelea wacha tujuzane kuhusu hili, ispokuwa nitaeleza kwa upande wa bank tu hizi njia nyingine tutaelezana wakati mwingine au hata kwa kupitia maoni.

kwanza fahamu jambo muhimu kuwa adsense wanawatumia pesa zao wateja wake kuanzia dola 100, pia ili kujua jinsi ya kurekebisha mambo mpaka pesa yako itumwe kwenye bank akaunti yako lazima ufikishe dola 10 na google watakutumia (PIN) Kupitia sanduku lako la barua ulilojaza wakati unajiunga nao,
mfano wa PIN utakayotumiwa na google
Ukiingia katika akaunti yako ya adsense kama umeshafikisha dola 10 utaona sehemu wanakuomba ujaze PIN yako waliyokutumia , fanya kama walivyokwambia jaza PIN yako kutoka katika barua hio uliokwenda kupokea posta, ukisha jaza nenda sehemu iliyoandikwa payment setting
Hapo katika setiing kuna vipengele vingi ila sisi tutazungumzia kuhusu kujaza data zako za bank basi, bonyeza new form of payment kisha chagua wire transfer to bank account kisha jaza form utakayopewa ila kabla ya kujaza lazima ujue SWIFF za bank yako kwa hiyo lazima uwasiliane na bank yako ila kama unatumia equity swif zao ni hizi ( $ : EQBLTZTZ, na kwa pesa tofauti na $ ni hii,  EQBLKENA) 
Picha hii kwa hisani ya ndugu yetu Harsh kumar


baada ya kujaza form yao hiyo baasi utakuwa umeshamaliza kila kitu pindi pesa yako itakapotumwa utajulishwa kupitia email yako na kama unatumia sim banking utajulishwa na sms kutoka bank

Share na marafiki kama makala hii itakuwa imekusaidia au kama umeipenda Riyadi Bhai hapa fanya kuniachia maoni yako ili nikusaidie zaidi unaweza kunitumia maombi yako kuwa kitu gani nikifafanue kuhusu Adsense kupitia riyadibhai@gmail.com
Kumekuwa na changamoto sana kwa wamiliki wa blog za kiswahili kupata akaunti ya Adsense kutokana na taarifa zinazowekwa katika blog zao kuwa na lugha kuu ya kiswahili.Tumekuwa na website au blog nyingi za kiswahili zenye watembeleaji zaidi ya 50,000 kwa siku na zingine hadi100,000 kwa siku lakini hazikubaliwi katika programu hii.

[soma 
Njia za kupata pesa kupitia adsense kwenye blog/website yako]

Jambo la msingi ambalo tunapaswa kufahamu ni kuwa Google Adsense ni programu ya kibiashara zaidi kwa maana google wanaangalia zaidi maslahi yao kutoka kwa makampuni na wafanyabiashara wanaohitaji matangazo yao yaonekane mtandaoni.

Je umewahi kujua kwamba nyuma ya Google Adsense kuna programu inayohusu wamiliki wa matangazo iitwayo Google Adwords.Programu hii inawapa wamiliki wa matangazo uwanja wa kuchagua aina ya website au blog ambazo wangependa matangazo yao yaonekane.

Miongoni mwa vigezo ambavyo wamiliki wa matangazo huangalia katika kuomba kutangaziwa bidhaa au huduma zao kupitia google ni:

  • Maneno ya msingi (Targeted Keywords)
  • Eneo au Nchi (Geographical Location)
  • Lugha itumiwayo katika Website (Language)
[soma Jinsi ya kuweka matangazo ya adsense katika blog ya kiswahili]

HIVI NDIVYO VIKWAZO VYA LUGHA YA KISWAHILI
1.wamiliki wa matangazo

Ikiwa umefanya uchunguzi wa kina katika matangazo ya Adsense yanayomilikiwa na makampuni ya tanzania,ASILIMIA 90utagundua kuwa ni wamIliki wa mitandao ya simu….FANYA UCHUNGUZI.Hii ni kutokana na makampuni haya huchagua eneo au nchi ambazo wanataka matangazo yao yaonekane “geographical location” na sio “targeted keywords”

Ukiwa kama blogger mwenzangu nikupe siri ya kuwa wanaokiangusha kiswahili katika programu ya adsense ni wamiliki wa matangazo.Hii ni kutokana na Programu ya Google Adwords inawapasa wamiliki wa matangazo kuchagua maneno ya msingi “keywords” ambayo matangazo yao yataonekana katika blog zilizobeba hizo “keywords”

2.“Target keyword”

Katika programu ya google Adsense tunapoongelea “Keyword” tunamaanisha yale maneno ya msingi yanayopatikana katika utafutaji ndani yagoogle.com.Ukilinganisha takwimu za utafutaji wa “keywords” ndani ya google.com utaona utofauti mkubwa wa lugha ya kiswahili na lugha nyingine.
Mfano mtu anayeandika kwa lugha ya kiingereza kupitia google “how to get diabetes treatment” hapa utaona “keywords” ni “diabetes” na “treatment” ambapo kwa lugha ya kiswahili mtu anayetafuta jambo lile lile angeandika “namna ya kupata matibabu ya ugonjwa wa kisukari” hivyo hivyo pia utaona “keywords” hapa ni neno “matibabu” na “ugonjwa wa kisukari“.

Kwa mfano mdogo hapo juu utaona ya kuwa hakuna kampuni nchini Tanzania au hata duniani itakayo iomba google iweke matangazo yake katika blog zinazozungumzia “ugonjwa wa kisukari” ukilinganisha na “keyword” kama “diabetes” ambayo ina maana sawa na ugonjwa wa kisukari.

Makampuni mengi makubwa yanatarajia wanapoweka matangazo yao katika “targeted keywords” ni rahisi kumshawishi mtumiaji ku bofya “click” tangazo lao kwa maana hiyo ujumbe wao utakuwa umemfikia mlengwa.

Kulingana na hili pia jaribu kufanya uchunguzi katika blog au website nyingi za kiswahili,wengi wao wanazungumzia habari ,matukio,udaku na michezon tu.Hivi ni kweli kuna kampuni gani ya nje itakayokubali kuweka tangazo lao katika blog yenye habari tu.Hii ni kutokana na kuwa hakuna kampuni inayouza bidhaa zinazohusiana na habari.
Kwa Hali ya Sasa Kumekuwa na Blogs nyingi za Kiswahili ambazo mbali na kujitahidi kupata Akaunti za Adsense bado wanakabiliwa na Changamoto Kubwa ya Matangazo yao Kutooneka, Hii Inatokana na Google Adsense Kuto Support Lugha yetu ya Kiswahili katika Kuratibu Uonekanaji wa Matangazo katika Site Husika. 

Leo Nitakupa Mbinu ambayo Itakufanya Ads ziendelee Kuonekana Japo Una Tumia Lugha ya Kiswahili katika Blog Yako. Binafsi sio Mtaalamu sana wa Mambo ya Codes, Ila nimekubali kujifunza na kujisomesha mtandaoni kwa kadri ya Uwezo wangu. Hivyo Nitakuomba Uridhike na hiki kidogo nitakachokupa leo nawe usisite kuitafuta elimu ya kujazia Sehemu Nyingine kwani ELIMU HAINA MWISHO. 

Japo kuwa sio lazima ujifunze kila kitu Tukirudi katika Mada yetu, Hatua za Kufuata ili Matangazo yaweze Kutokea Katika Site za Lugha ya Kiswahili:- 

1. Ingia kwenye Dashboard yako ya Blogger, Nenda Mpaka kwenye Template, Click Customize Ili Ikupeleke kwenye Edit Css
Baada ya Hapo Nenda Kwenye Tab ya Advanced halafu Add CSS, Hapo Utaingiza Codes za Design Hii kisha Una Apply to Template Halafu Unarudi Kwenye Blogger Template Tena. 

Weka Codes Hizi za Rangi Nyekundu{   </script>  google_language = "en";</script>  
    <meta content='Engish' name='language'/> }  hapo Juu.

2. Hatua ya Pili Unaenda kwenye Blog Dashboard yake unaingia Template halafu Unabonyeza Edit HTML, Ikifunguka Bonyeza mouse yako kwenye code za template kisha bonyeza CTRL+F (Amri ya Kutafuta) Ndani ya Kibox cha Kulia Juu kwenye Codes za HTML utaingiza Codes Hizi <head>  halafu Bonyeza Enter. Chini ya Head Utaingiza Codes Hizi Hapa { <meta content='Engish' name='language'/>  } Kisha Una Save.
Nia Na Madhumuni ni Kuilazimisha Site Yako Kwenye Meta Tags Iitambulishe Kama Ni Site.Blog inayotumia Lugha ya Kiingereza. N.B. Unaweza Ukaweka Mara nying hii Meta Tag kwenye Blog yako though Mimi nakushauri Usizidishe mara 3.

3. Hatua ya Tatu ni Kuandaa Page ya Privacy Policy.
Hapa Utaenda Kwenye Dashboard yako Kisha Utaingia Sehemu ya Pages, Uta Create Page ya Privacy Policy Kisha Utaandika Maneno angalau Paragraphs 4 kuhusiana na Site yako na Vile Ambavyo hautohusika n Comments mbaya kutoka kwako au Wasomoaji wako, Kisha Unai Publish.

Ukishai Publish Unaenda Kwenye Layout katika Dashboard yako Ili Uchague wapi Itakaa Hiyo Page ya Privacy Policy, Ingawa Ikakaa Juu Ni Bora Zaidi.

N.B Post za Nyuma kabla ya Kufanya Trick Hii zinaweza Zisioneshe Ads bali zitaanza Kuonesha zile zitakazokuja baada ya Trick Hii.

Kama Njia Hii Haitaleta Mafanikio Kwako, Ingia Kwenye Ku Edit HTML tena, Kisha Tafuta data:post.body, halafu tafuta Post Footer au Post Footer Line 1 Kisha Uingize yale maneno ya Privacy Policy Humo.


Thanks kwa Kuwa Nami, Kwa Maoni na Ushauri Usisite Kuwasiliana Nami.Niachie maoni yako hapo chini nami nitayafanyia kazi kwa kukupa majibu kadri nitakavyofahamu maswali yako.
Habari msomaji wa blog hii hapa leo nitakujuza kuhusu kupata pesa kupitia blog au website yako wengi hutumia mitandao bila mafanikio leo inabidi tujue kutumia kwa mafanikio yetu


kama unamiliki blog au website kuna kitu kinaitwa google adsense hii ni
program ambayo inatupatia pesa sisi wanablog wenda unaijua au ushawahi kuisikia mahali.

GOOGLE ADSENSE NI NINI ?

Ni mfumo wa Matangazo kwa njia ya mtandao unaihusisha matangazo kwenye kurasa za tovuti , programu , blogu , majukwaa na huduma zingine za mawasiliano haswa kwenye mtandao .

Google Adsense ina aina 2 za matangazo kuna yale ya maandishi pekee yaani Text na yanayotembelea kama picha na video yote ni mazuri na yote yana gharama zake .

GOOGLE ADSENSE NA MAISHA YAKO
Kwa kutumia Google Adsense unaweza kupata karibu laki 9 na zaidi kila mwezi na ukasahau kufanya shuguli zingine , Adsense inaweza kufunga Akaunti yako muda wowote au blogu yako muda wowote ule usipozingatia Masharti yao , kwahiyo usitegemee sana , Soma sheria za Adsense Hapa

GOOGLE ADSENSE INAFANYAJE KAZI
Kama unatovuti yako ukiweka matangazo ya mfumo wa adsense utalipwa kutokana na wingi wa watu wanaitembelea tovuti hiyo na jinsi watu watakavyo gonga click matangazo hayo.

Mfano mrahisi ni Bwana Riyad ana kampuni yake inaitwa Riyadi Bhai , badala ya kutengeneza matangazo makubwa kwenye magazeti pamoja na kufungua tovuti ataenda kuongea na google au wawakilishi wa google atatoa tangazo lake atasema jinsi anavyotaka liangaliwe kwa mfano idadi ya nchi au maeneo ndani ya nchi husika , Matangazo ya Riyadi Bhai yanaweza kuonekana kwenye blogu ya Zote kali inayoitwa www.zotekali.com na tovuti nyingi za watu mbalimbali zilizokuwa na huduma za Adsense .

Kwahiyo Riyad atafaidika kwa tovuti yake kutembelewa na watu wengi kutokana na kutangaza kupitia adsense na watu wanaotembelea Zote kali kuona kiunganishi cha tovuti yake.

NOTE > Kufuatilia masharti na maelezo mengine ni muhimu sana kwa mfano unatakiwa usiwaambie watu wagonge matangazo yako waache wa gonge click wenyewe ukifanya hivyo unaweza kufungiwa .

SWALI MUHIMU
Je ukubwa wa Tovuti au Blogu au umaarufu ndio kuongeza kipato cha Adsense ?

Jibu ni hapana utaweza kupata mapato zaidi kutokana na jinsi ulivyoweka matangazo yako na jinsi watu wanavyogonga matangazo hayo hapo ulipoweka kwenye kurasa za tovuti au blogu yako

USAJILI WA GOOGLE ADSENSE UKOJE
Wale wanaotumia huduma za Gmail ambayo ni mali ya Google ni rahisi kujisajili ili kutumia mfumo wa Adsense kwenye blogu na tovuti zao unaweza kutembelea www.google.com/adsense

NOTE>Kila mtu anahaki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kufuatilia malipo yake mwenyewe na kulipwa yeye.

KUKUBALIWA NA PIN NUMBER
Usajili wa Goolge Adsense hauwezi kukamilika kama huna PIN NUMBER na kujaza vitu vingine vya kuthibisha jinsi unavyolipa kodi , kama uko nchi za ulaya kuna namba unatakiwa kuandika ndio utapewa PIN NUMBER .

Kama ukiwa nje ya ulaya kama Tanzania , unaweza kutumiwa PIN NUMBER kutumia DHL ambapo utaingiza namba hiyo kukamilisha mfumo wa usajili au unaweza kuwatumia google kitambulisho au aina nyingine ya utambulisho kuthibitisha uwepo wapo kama kadi ya benki au passport.

NOTE> Bila pin Number hutoweza kutambulika kwenye mfumo wa google adsense na malipo yako hutopatiwa .

MALIPO YA GOOGLE ADSENSE
Google huwa inalipa wenye Adsense kwenye tovuti zao kila mwisho wa mwezi kwa mfumo wa cheki , benki au western Union kutegemea na nchi ambayo mtu yupo , malipo hulipwa pale kunapokuwa na kiasi cha pesa kuanzia dola 100 kwa mwezi ambapo dola 17 hutumika kama gharama za kusafirisha cheki kama uko nchi ambayo wanatuma cheki .

Kwahiyo unavyofanya kazi hii ya matangazo hakikisha unapata hela nyingi zaidi ili uweze kulipa gharama za benki na usafirishaji wa cheki yako , angalau uweze kuwa na dola za kimarekani 700 kila mwezi .

NOTE > Malipo ya kila mwezi hulipwa mwezi unaofuatia kama yalifikia zaidi ya dola 100 za kimarekani 

MALIPO YANAVYOTUMWA
Kwa nchi ya Tanzania malipo ya Google Adsene huja kwa njia ya DHL ambapo hufika kila tarehe 2 kila mwezi , malipo yakifika kwenye ofisi za DHL wateja hupigiwa simu na kupelekewa au kama unaweza kufuatilia mwenyewe kutumia tracking number ya DHL kujua kama mzigo umefika au la .

Jambo la kujua ni kwamba watu wengi hufikiri cheki zinatumwa kwa njia za posta za kawaida hapana ni DHL .

UTARATIBU WA KIBENKI
Unatakiwa uwe na Akaunti kwenye benki yoyote Tanzania kwa sababu cheki za google huandikwa jina la mtu au kampuni kwahiyo lazima uwe na Akaunti kama uko Tanzania .

Ukishaweka cheki kwenye Akaunti yako huchukuwa siku 21 za kazi ili kuweza kulipwa malipo kwenye Akaunti yako na gharama zingine za kibenki .
Kutokana na gharama nyingine za kibenki ina maanisha ukiwa na shilingi laki 5 kwa mwezi ujiandae kutoa elfu 70 kama gharama za kushugulikia Cheki yako kwenye benki yako.

NOTE > Watu wengi hukata tamaa mapema na huishia njiani kwahiyo wanapoteza hela zao nyingi na watu wanatangaza kwenye tovuti au blogu hizo bure .

Kumbuka unavyofungua blogu ukaweka adsense matangazo yataendelea kuwa hapo na watu wataona wanavyotafuta vitu mbalimbali kwenye mtandao kwahiyo usikate tamaa mapema .

ZINGATIA NA UWE MAKINI NA MATAPELI
Hapo juu nimesema kila mtu ana haki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kulipwa kwa jina lake hela yake mwenyewe , kuna watu wa nchi za nje haswa Uganda wanapenda kuwalaghai watu wa Kenya na Tanzania kwamba washirikiane kuendesha Mfumo wa Adsense kwenye tovuti zao na kugawana Hela nusu kila mwisho wa mwezi .

Usikubali kuingia kwenye mtego huu , unatakiwa uwe na Akaunti yako unayoweza kuitolea maelezo na inayolipwa kwa jina lako kwenye nchi yako unaporuhusu hivyo faida haiendi nchini mwako inaenda Uganda kwa jina la Raia wa Uganda ambaye atatumia jina bandia ili asimwone akisha kutapeli hela zako .
Hata kama unapata hela kidogo mfano dola 1 kwa siku usikate tama utaweza kuongeza vitu kwenye tovuti yako haswa kwa lugha ya kiingereza na kifaransa na kuweza kupata hata dola 50 kwa siku moja jinsi unavyoendelea kukuwa .

CHANGAMOTO ZA MFUMO HUU
Baadhi ya maeneo Adsense haifanyi kazi kutokana na aina ya matangazo yaliyofungiwa kutokana na mila na desturi za maeneo hayo .

Mfumo wa Adsense uko zaidi kwa lugha ya kiingereza na nyingine za kimataifa bado haijasambaa sana kwenye lugha zingine ndogo ndogo kama Kiswahili ingawa mtu anaweza kutangaza pia 

Benki nyingi haswa za afrika hazitambui mfumo wa google adsense kwahiyo baadhi ya watu wanapata tabu pale wanapoenda kuingiza cheki zao kwenye Akaunti na kudhani ni utapeli badala yake nyingi hutumwa kupitia CITIBANK ambayo huduma zake ziko juu sana .

Nchi nyingi hazina mfumo wa kulipa kodi kwa njia ya mtandao kwahiyo unakuta wanachama wote wa google adsense wanalipa kodi kwenye nchi ya marekani kwa kwa kila malipo ya adsense nchi nyingi zinapoteza malipo hayo kutokana na mifumo yao .

Kwa sasa nchi ya Kenya na Uganda wamefanya mazungumzo na google kwahiyo ukiwa nchi hizo malipo yako unapata baada ya siku 3 kila mwezi kwa njia ya western union au kuingiziwa fedha kwenye Akaunti yako moja kwa moja .

Nakaribisha maoni yako hapo chini kuhusu makala hii usisahau Kushare