JINSI YA KUPOKEA PESA ZAKO KUTOKA ADSENSE KWA KUTUMIA WESTERN UNION

As salaam aleikum wapendwa karibuni tena katika blog yetu tuendelee kupeana maujuzi ya kuturahisishia mambo yetu, kipindi cha nyuma niliandika makala jinsi ya kupokea pesa zako kutoka adsense kupitia wire transifer ( njia ya kibenki) unaweza kuisoma hapa :[ Jinsi ya kupokea pesa zako kutoka adsense kupitia bank] leo tuangalie njia hii ya pili ambayo baada ya kuitumia nimegundua kuwa ni bora na ni nafuu zaidi ya bank.

kabla hatujaendelea wenda kuna ndugu zetu wengine hawajui hata Adsense yenyewe ni nini soma hapa [ Jinsi ya kupata pesa kupitia Adsense ]

haya sasa tuendelee na mada yetu hii kwanza kabisa fahamu jinsi ya kuweka namna ya kupokea mapato yako kupitia Western Union ingia katika akaunti yako ya adsense
upande wa kushoto wa dashibodi ya adsense bonyeza sehemu iliyoandika setting kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Payment
kisha utabonyeza sehemu imeandikwa manager payment kisha ongeza au chagua western union kisha ifanye kuwa ndio Primary sasa rudi katika payment

Kama utaona muonekano kama huo pichani basi umefaulu sasa tuangalie vipi utaweza kuzishika pesa zako mikononi baada ya kufikia U$D 100 ambacho ndio kiwango cha adsense kuwalipa watumiaji wake.
Bonyeza hiyo sehemu iliyoandikwa View Transactions kisha tazama muamala wako kisha ubonyeze itafunguka new Tab itakuonesha kila kitu 
hapo ndio ilipokuwa pesa yako hizo ndio vitu vya kuandika sehemu au kama utaenda na kifaa chako katika bank/ofisi inayotoa huduma za western union

vitu vya kuzingatia wakati unaenda katika ofisi za western union kuchukua pesa yako ni lazima uende na na moja kati ya hivi: Passport ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha kitaifa au cha mpiga kura na lazima kiwe chako wewe mwenyewe.

ukifika kuna karatasi utatakiwa kujaza majina yako ya utakayoyajaza lazima yafanane na ya katika kitambulisho chako na akaunti yako ya adsense, sehemu ya swali jaza namba zilizopo katika ID Billing tazama hapo pichani utaziona katika sehemu ya mtu anayekutumia jaza Google Ireland Limited.

Ukishafika kwa mtoa huduma mpe hiyo karatasi na kitambulisho chako kati ya ivo nilivyokuorodheshea hapo kwenye maandishi mekundu.

mpaka hapo utakuwa umekamilisha kuchukua pesa yako sasa furahiya, bila shaka umepata mwangaza kidogo kama sio sana lakini kama kuna sehemu hujaelewa niachie swali lako katika sehemu ya maoni nami nitakujibu kwa kadri nitakavyokuelewa. shukrani kwa kuwa nami mwanzo mpaka mwisho sambaza makala hii kwa ndugu na jamaa ili nao wafaidike

NB
Kwa wale wazee wa kukopi na kupaste naomba usome hapa kabla hujakopi makala za kwenye blog hii 

12 Comments

  1. Hi Bro , My Blogger Comment System Not Working On Savida 2.5
    How i can fix it. Website www.webdevo.tk

    ReplyDelete
    Replies
    1. Add this in gadget of comment system [blogged] then save

      Delete
    2. sorry bro typing error not blogged but is [blogger]

      Delete
    3. Thanks But Its Not Working For Me.

      Delete
    4. Hey bro I found so;ution for your problem today alhamdulillah, Goto Blogger Dashboard >> Template >> Edit HTML
      Search and find this code :

      [hidden],template,.blogpost-setting{display:none}
      Replace it with the following code :

      [hidden],template {display: none;}

      then save your theme

      Delete
  2. Nimefanikiwa kupata matangazo ya AdSense changamoto yangu kujua mfumo gani rahisi Wa kupokea pesa AdSense?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Western union ni mfumo rahisi na waharaka zaidi

      Delete
  3. Kama Sina kitambulisho chochote
    Ila Nina namba ya kitambulisho changu cha taifa ninaweza kupata pesa zangu?

    ReplyDelete
  4. Asante Sana mkuu kwa somo hili.
    Ila saivi AdSense naskia wameiondoa Western Union kwenye njia za malipo.
    Je Kuna mbadala wake au! Ndo mpaka wire transfer

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwasasa wanatumia njia mbili tu wire na check

      Delete

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa