Fahamu kuhusu supercomputer na jinsi inavyofanya kazi


Super Computer ni kompyuta zenye kiwango cha juu cha utendaji ukilinganisha na kompyuta za kawaida. Utendaji kazi wa kompyuta hizi unapimwa kwa uwezo wake wa kushughulikia kazi zilizosubirishwa kwa sekunde (FLOPS).


Kompyuta hizi huwa na maelfu ya prosesa ndani yake na zina uwezo wa kukokotoa mabilioni ya mahesabu ndani ya sekunde. Hutumika kuendesha programu zinazofanya kazi kwa muda halisi. 



Na nchi zinazoongoza kwa kuwa na kompyuta nyingi za aina hii ni Marekani, China na Ujerumani.

Related Article

Super Computer hutumika kwenye madhumuni ya kisayansi na kihandisi yanayohitaji taarifa za kina na ukokotoaji mzito kama vile Quantum mechanics, utabiri wa hali ya hewa, uchunguzi wa mafuta na gesi, aerodynamics (Elimu ya Anga), utafiti wa nyuklia na uchanganuzi wa crypto (Sarafu za Kidigitali). Programu endeshi inayotumika sana kwenye kompyuta hizi ni Linux.


Aina za Super Computer hutofautiana kutokana na matumizi yake pamoja na kampuni iliyotengeneza. 


Makampuni na mashirika yenye kompyuta hizi ni pamoja na IBM, HP, Fujitsu, SGI na Dell. IBM wametengeneza aina ya IBM Roadrunner, IBM Sequoia, IBM Blue Gene na IBM Power 775 .

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa