Articles by "Android"
Showing posts with label Android. Show all posts
Kampuni ya Motorola hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Motorola One Power au P30 Note huko nchini India, simu hii inakuja na muonekano unaofanana sana na iPhone X huku ikiwa na ukingo wa juu maarufu kama top notch tofauti na simu nyingi kutoka kampuni hiyo.
Motorola One Power au (P30 Note) inakuja na Battery kubwa ya 5000mAh ambayo kwa mujibu wa kampuni hiyo inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku mbili kwa kuchaji mara moja tu, vilevile motorola inadai kuwa simu hii pia inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku moja na masaa kadhaa iwapo utakuwa unacheza game mfululizo kwenye simu hiyo.
Mbali na battery ambayo ndio maboresho makubwa ya simu hii, Motorola One Power (P30 Note) inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS display ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2246 pixels pamoja na uwiano wa 18.7:9 ratio.
Simu hii pia inakuja na mfumo wa Android 8.1 ambao unaweza ku-update hadi kwenye mfumo mpya wa Android 9 Pie. Simu hii inatumia processor ya Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 3, GB 4 na GB 6. Motorola One Power inakuja na kamera mbili za nyuma ambapo kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 5. Sifa nyingine za Motorola One Power ni kama zifuatazo.Sifa za Motorola One Power
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCS capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2246 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~402 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 32 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu tatu moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4 na ya mwisho ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 yenye f/2.0, 1.25µm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye ff/2.2, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (15W)
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa moja ya Midnight Black.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Motorola One Power
Kwa upande wa bei, simu hii imetangazwa hivi leo kuanza kupatikana huku inchini India ambapo itakuwa inaanzia kuuzwa kwa rupee ya india Rs 15,999 ambayo ni sawa na Tsh 503,000 bila kodi. Bado hakuna taarifa zaidi kuhusu ujio wa simu hii kwenye nchi nyingine mbalimbali hivyo endelea Kutembelea Swahili Tech kujua zaidi kuhusu simu hii.
Mfumo wa Android ni moja ya mfumo ambao unatumika kwenye simu nyingi sana kwasasa, mfumo huu kwa sasa unamilikiwa na kampuni ya Google na hapo siku ya jana mfumo huo umefikisha miaka 10 toka kuanzishwa kwake rasmi.
Sasa kwenye miaka 10 hii ya kuanzishwa kwa Android labda nikupe historia kidogo ya mfumo huu ambao sasa ndio unaonekana kutumiwa zaidi kwenye simu za mkononi maarufu kama smartphone. Kwa kuanza labda tuanzie mwaka 2005 ambapo mwaka huu kampuni ya Google ndio ilinunua kampuni ya Android Inc ambayo ndio ilikuwa mtengenezaji wa mfumo huo.
Kampuni hiyo ya Android Inc ilikuwa ikiongozwa na kumilikiwa na Andy Ruby, Rich Miner, pamoja na Nick Sears ambao ndio waanzilishi na wabunifu wa mfumo huu. Kampuni ya Google ilifanikiwa kununua kampuni ya Android Inc kwa makadirio ya dollar za marekani $50 Milioni ambayo ni sawa na Tsh Bilioni 1.14. Mbali na kiasi hicho, kwa mujibu wa tovuti ya venturebeat inasemekana kampuni ya Google ilitumia zaidi ya dollar za marekani $ 130 milioni kuweza kukamilisha ununuzi kamili wa kampuni ya Android Inc.
Baada ya Google kufanikiwa kununua kampuni hiyo inayochipukia ya Android Inc, Mwaka 2007 kampuni ya Google ilitangaza rasmi kuleta mfumo huo rasmi kwa watumiaji mbalimbali. Kufanikisha hayo simu ya kwanza yenye kutumia mfumo wa Android ilizinduliwa rasmi tarehe 23 mwezi September mwaka 2008 kwa ushirikiano wa kampuni tatu za Google, T-Mobile, pamoja na HTC.
HTC Dream au G1 ndio jina la simu hiyo ya kwanza iliyokuwa ikitumia mfumo huo wa Android kwa mara ya kwanza kabisa, simu hii kama wewe ni muhenga basi lazima kwa namna moja ama nyingine utaikumbuka simu hii. HTC Dream au G1 ilikuja ikiwa na mfumo wa Android 1.6 (Donut), simu hii ilikuwa inauzwa kwa kati ya dollar za marekani $179 hadi $399 na ilikuwa inauzwa rasmi na kampuni ya simu ya T Mobile.


Simu hii ya HTC Dream au G1 ilikuwa na kioo cha inch 3.2 ambacho kilikuwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya TFT capacitive touchscreen yenye uwezo wa kuonyesha rangi elfu 65.
Simu hii pia ilikuwa ikitumia processor ya Qualcomm MSM7201A ambayo ilikuwa na nguvu ya MHz 528 pamoja na GPU ya Adreno 130. Kwa upande wa ukubwa wa ndani simu hii ilikuwa na ukubwa wa ndani wa MB 256 huku ikisaidiwa na RAM ya MB 192. Mbali na hayo simu hii ilikuwa na uwezo wa kusoma memory card hadi ya GB 16.
Kwa upande wa kamera simu hii ilikuwa na kamera moja tu ya nyuma iliyokuwa na Megapixel 3.15 ambayo ilikuwa na teknolojia ya autofocus, pamoja na uwezo wa kurekodi video. Battery ya simu hii ilikuwa ni ndogo sana ikiwa na uwezo wa Li-Ion 1150 mAh huku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 5 pekee.
Baada ya kuzinduliwa kwa simu hii baadae ziliendelea kuja simu nyingine kama Motorola Droid, HTC Droid Eris, Samsung Behold II na HTC Nexus One ambayo ilizinduliwa mwaka 2010.
Kwa ufupi ni kuwa Android kwa sasa ni kubwa sana, hadi kufikia mwaka 2017 Android ilikuwa imeshikilia asilimia 87 ya mifumo ya uendeshaji ya simu janja. Bila shaka asilimia hizi zinaendelea kupanda kila siku huku ukizingatia sasa tuko kwenye mfumo wa Android 9 Pie ambao umezinduliwa hivi karibuni. Kwa sasa mfumo wa Android unaendesha vitu mbalimbali kama vile kompyuta, Radio za magari, TV, pamoja na vifaa mbalimbali vya kielektroniki.
credit : TanzaniaTech
Wengi tumekuwa na kiu ya ku root simu zetu ili tuweze kubadili muonekano mzima wa simu. Simu ikiwa rooted ina faida nyingi. Moja ya faida kubwa ni kuweza kuweka custom rom pamoja na exposed framework.

Swali linakuja kwamba utajuaje kama simu yako tayari imekuwa rooted au bado.Njia rahisi ya kujua kama simu yako ipo rooted au bado unatakiwa ku download ROOT CHECKER kutoka kwenye play store

STEP 1
Search for root checker kwenye play store kama picha inavyoonyesha chini kisha install kwenye simu yako


STEP 2
Baada ya kumaliza ku install root checker kwenye simu yako ifungue hiyo app kisha utaona muonekano kama kwenye picha chini

STEP 3
Bonyeza sehemu iliyoandikwa VERIFY ROOT. Endapo utaona muonekano kama huo hapo chini basi simu yako tayari ipo rooted kama utapata muonekano mwingine tofauti na huo hapo chini basi simu yako haipo rooted. Unapaswa ku root ili uweze kuweka custom rom

As salaam aleikum, Kuna matumizi mengi sana ya kamera ya simu janja zetu ukiachana na yale tuliyo yazoea ya kupiga picha tu

Unajua kama kamera ya simu janja yako inaweza ikawa na matumizi lukuki ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kurahisisha maisha yako

1. Scan Nyaraka

Kamera ya simu janja yako pia inaweza ikawa ina’scan’ nyaraka tofauti tofauti. Pata picha unakuwa na ‘scanner’ ambayo ipo mfukoni kwako. Unaweza uka ‘scan’ vitu kama vile mikataba,risiti au kitu chochote kilichopo katika karatasi na unataka ukifanye kiwe kidigitali

Baada ya hapo unaweza ukaamua kutuma vitu hivyo katika barua pepe au unaweza ukavihifadhi katika mfumo wa PDF au JPG
Unataka ku’scan’ vitu?

Kwa iOS shusha(download) Evernote

Kwa Android shusha Google Drive ndani yake kuna kipengele cha ku’Scan’

2. Tumia Kamera Ya Simu Janja Yako Kama Mkalimani Wako

Teknolojia inabadilisha dunia kwa kiasi kikubwa sana miaka kadhaa iliyopita ningebisha kata kata kama jambo hili lingeweza kutokea. Hivi unajua unaweza ukatumia kamera ya simu yako ili kutafsiri lugha Fulani?

Kumbuka kuna maandishi huwa yanaandikwa na mara nyingi tunakuwa hatuyaelewi kwa mfano ukiwa katika mgahawa ikaja menyu yenye maandishi ya kigeni hapo ndipo huduma hii utakapo ona ubora wake

Ukiwa na App ya Google Translate, ambayo inaweza kutafsiri lugha 29 utafanikisha hilo kwa kuweka kamera mbele ya maandishi yaliyoandikwa na hapo App itafanya zoezi zima la kutafsiri kwenda katika lugha unayotaka

3. Tumia Kama Kamera Ya Ulinzi

Hivi ulishawahi kuwa na hamu ya kutumia kamera ya simu yako kama njia ya ulinzi? Labda una kamzigo kako pale ndani na unataka ukachunge. Ondoa shaka kuna App maalum ambazo zinakuwezesha kufanya hayo yote. App hizi hutumia kamera ya simu janja ili kugundua mwondoko wa aina yeyote (motion) na kisha kukutaariffu kupitia barua pepe (e-mail) yako

Kwa Android shusha App ya Silent Eye

4. Fuatilia Barcodes Za UPC

Wakati mwingine wakati ukiwa unafanya manunuzi ya vitu na ukawa huna uhakika kama unanunua vitu imara achana na ku Google, tumia kamera ya simu janja yako kuweza kuichunguza bidhaa hiyo.

Zile App ambazo zinamsaidia mtu ku’scan code’ za UPC zinampatia mtu taarifa za bidhaa katika kiganja chake kabisa. Ukiachana na taarifa kuhusiana na bidhaa bado utaweza kufananisha bei tofauti tofauti ya bidhaa hizo ili kujua kama umepewa bei nzuri au la

Kwa Android shusha App ya ShopSavvy Barcode and QR Scanner

5. Shangaa Anga

Hivi ushawahi kukaa usiku na ukawa unashangaa anga na ukaanza kujiuliza maswali kama baadhi ya vitu unavyoviona ni nyota au ni sayari zingine?
Sasa App ya Skyview kwa Android na iOs itakupa majibu yote

App hii inatumia kamera ya simu yako katika kukuonyesha jinsi anga ilivyo cha kufanya hapa wewe elekeza kamera ya simu janja yako katika anga.

Pia kama remote ya Tv au kisimbusi inasumbua unaweza kutumia kamera ya simu kuona kama remote hiyo inatoa mionzi au la kabla ya kuchukua hatua nyingine kama kubadili betri au kuitengeneza.Washa kamera ya simu,nyoshea kile kitaa cha remote kwenye kamera huku ukiwa una bonyeza vitufe kwenye remote.Utaona mwanga unawaka kwenye screen ya simu endapo kama remote ni nzima
As salaam aleikum Mswahili mwenzangu matumaini yangu uko poa kama mimi Alhamdulillah, leo tuangalie jinsi ya kubadilisha Version ya simu yako ya android wenda ukajiuliza kwanini nibadilishe Version ya android yangu naam inabidi tubadilishe kwasababu kuna app za muhimu wakati mwingine tunazihitaji lakini kutokana na version za simu zetu kuwa ni toleo la zamani tujikuta tunakosa uhondo huo. twende kwenye mada moja kwa moja tusipoteze muda sana, kama utakuwa na swali utaniuliza katika sanduku la maoni


Hatua ya kwanza download app inaitwa Root browers kutoka playstor nenda moja kwa moja na link hiyo hapa Download.

Baada ya kuifungua utaona files zimetokea nyingi hapo teremka chini na tafuta /angalia file lililoandikwa *System*

Fungua humo na teremka chini utaona kiji file kimeandikwa Build.prop
Angalia hicho maana vipo viwili kengine kanaitwa Build.prop.bak

Bonyeza Build.prop kisha itafunguka na options tano hapo angalia palipo andikwa RB text Editor

Ukisha bonyeza hapo itafunguka na utaona detail zote za simu sasa hapo utafanya chaguo lako kama unataka kubadili builder number, manufactures,  na mengineyo kwa version utashuka chini 
 kisha utaangalia palipo andikwa ro.build.version.release=[hapa itakuwepo version original ya simu kisha utaifuta na kuweka mpya]


NOTE; Hakikisha unaweka version isiyo zidi 7 usidhidishe zaidi ya hapo ili kuweka simu yako katika Latest isiwe imepitiliza italeta shida

kisha ukimaliza kufanya mabadiliko hayo utasevu kwa kubonyeza icon ya sevu iliyopo juu kabisa mkono wa kulia kialama chake kipo kama mfano wa hichi ki emoj 🏥

 kisha restart simu yako na nenda kaanglie version mpya uliyoweka katika settings kisha about phone
 na utaweza kudownload app bila kikomo kwa kutokuwa na kizuizi cha version

Kuna apps ambazo zinarun kwenye version latest tu, kwahiyo ukiweka version latest apps latest zitakubali. 

Kwa mfano Recharge king haiwezi kurun kwenye W3 tecno ila inarun kwenye k7 na k9 lakini ukibadilisha version kwenye w3 na kuweka 7 itarun bila shida.

Imeandikwa na Riyadi Bhai Sambaza makala kama ilivyo kama unahitaji kukopi makala hii soma hapa Copyright Policy Zingatia sheria za Blog hii Ahsante kwa Kutembelea Swahili Tech

As salaam aleikum mpendwa kama kawaida msomaji wangu kutokana na kutokuwa hewani kwa muda mrefu sasa ni muda wa kuweka makala za kutosha hadi tuombane po, wacha tuendelee Kulinda simu yako au tablet yako ya Android hakuishii kwenye kuweka screen lock tu, la hasha kuna njia nyingine nyingi za kuifanya simu na data zako kuwa salama muda wote.
Leo tujaribu kuangalia njia 10 zitakazokusaidia kuifanya simu yako iwe salama muda wote. Tumeamua kuanza na simu na tablet za android kwa sababu asilimia kubwa simu zinazotumika hapa Tanzania kwa sasa ni za Android.

1. Weka Screenlock
Kuweka lock kwenye screen yako ni njia moja ya muhimu ya kuilinda simu yako hasa pale unapoipoteza au unapoiacha kwenye mikono isiyo salama. Katika mfumo endeshi wa android unaweza ukaweka screen lock tofauti kama PIN lock, Pattern lock, Password lock au Fingerprint scanner kama simu yako inauwezo huo. Kuna baadhi ya matoleo unaweza ukaweka voice lock au eye scanner lock. Hii inamzuia mtu mwingine asiyehusika na simu yako kuweza kuifungua bila ridhaa yako. Kuset screen lock fungua Settings–> Security–> Screen lock na hapo utachagua inayokufaa.

2. Lock Application zako za msingi, picha pamoja na video
Unaweza ukaongeza ulinzi katika application zako ambazo hutaki mtu mwingine aweze kuzitumia au kuzifungua kwa kuzilock kwa kutumia baadhi ya application za kulock mafail na application kama App Lock inayopatikana googe play store. Hii itakusaidia sana kulinda taarifa zako za ndani hata kama mtu amefanikiwa kutoa screen lock yako.

3. Hakikisha Mfumo Endeshi wako (OS) pamoja na Application zote unazotumia zipo Updated
Hii ni ya msingi zaidi kwani wengi wetu tumekuwa tukipuuzia kupdate application zetu hata pale zinapotuomba kuziupdate. Makampuni yanayotengeneza application husika huwa wanaziupdate sio tu kuongeza vitu vipya au kuongeza ufanisi, hapana bali kuziba mianya yote ya kiusalama iliyoachwa wazi hapo kabla. Unatakiwa kuset simu yako iwe inaupdate application zake automatically pale tu zinapotoka kwa kufungua Settings–> General –>Auto update application ( Hapa inategemea na toleo la android unalotumia).

4. Usidownload Application nje ya Googleplay store
Kwa kawaida simu yako huwa haikuruhusu kudownload application nje ya play store, ila unaweza kubadilisha hili kwenye settings–> security–>Device Administration –> Unknown sources kiurahisi. Sasa sio vizuri kabisa kupakua application nje ya play store kwa usalama wa simu yako. Wadukuzi wengi wamekuwa wakitumia mwanya huu kuiba data za mwenye simu au hata kuiharibu simu yenyewe (Kwa wenye tecno Y6 na H6 watakuwa mashuhuda wa simu zao inafikia kipindi huwezi kuicontrol) . Kwa hiyo unatakiwa kuzima hiyo kama unajua unachokifanya na unauhakika na application unayotaka kuinstal.

5. Kuwa makini na Application Permissions wakati unapoziinstal
Hii ni ya muhimu na kuzingatia sana, mara nyingi huwa tunapoinstal application kutoka Google Play huwa zinaomba ruhusa ya kutumia baadhi ya vitu katika simu yako. Kwa mfano punde tu unapoanza kuinstall Whatsapp huwa inaomba ruhusa ya kusoma majina na namba za simu zako, kutumia kamera yako pamoja na kutumia kinasa sauti chako, mara nyingi huwa tunaziruhusu kwa kubonyeza allow. Sasa hapa ni kwa kuzingatia zaidi hasa unapojaribu kuinstal application ambazo zinaomba ruhusa ya kutumia namba zako za simu au picha zako, lazima uwe na uhakika na hiyo application kwanza.

Kwenye toleo jipya la Android Marshmallow unauwezo wa kuruhusu au kuzuia ruhusa kwa application hata kama tayari umeshainstall.

6. Kuwa makini na taarifa unazoshare
Simu nyingi za Android zinatumia kivinjari cha Chrome kama kivinjari cha kwanza, kivinjari hiki kina uwezo wa kutunza taarifa zako zote za kuperuzi na kuzituma katika vifaa vyako vyote unavyotumia kama vile Tablet, Laptop pamoja na desktop zenye kivinjari hichi. Passwords, bookmarks pamoja na vingine vya ziada kupitia Google account vinaweza kuwa shared kwa kukurahisishia kazi wewe mtumiaji. Ila jaribu kufikiri kama umepoteza simu na ina kivinjari cha Chrome chenye taarifa zako zote, inakuwa rahisi kwa mtu aliyeiokota au kuiiba kusoma au kunakili taarifa zako. Hivyo hakikisha unakuwa makini linapokuja suala la kuchagua ni aina gani ya taarifa unataka kushare na vifaa vyako vingine.

7. Kumbuka kuset Android Device Manager
Android Device Manager ni njia inayokusaidia kutafuta simu yako pale inapopotea au kuibiwa. Kwa kuwasha Android device Manager unakuwa na uwezo wa kufuta data zako zote pale simu yako inapokuwa imeibiwa au kupotea au kuipiga na kuilia kwa sauti. Jinsi ya kuwasha Android Device Manager, nenda kwenye settings–>Securty–>Device administration na hapo utaona kitufe cha kuwasha chaguo hilo.

8. Backup Data zako
Kubackup data zako ni jambo la muhimu la msingi sana hasa linapokuja swala la simu za mkononi au tablet. Kwa mfano kurusu Synchronization ya namba zako za simu kati ya kifaa chako na akaunti yako ya gmail ni jambo la msingi zaidi kwa sasa. hii itakusaidia hata pale unapoamua kubadilisha simu hautakuwa na haja ya kuandika upya contact zako, ni kitendo cha kuingiza email (barua pepe) yako na contact zako zote zitajisave. Pia ni muhimu kutunza data zilizomo kwenye simu yako katika kifaa kingine tofauti na simu yako. Kwenye matoleo ya Lollipop pamoja na Android Marshmallow mtumiaji anaweza akaset backup kwa kuingia tu kwenye settings za simu yake.

9. Jaribu kujikinga na Virusi vya Android pamoja na Malware
Siku hizi kuna mamilioni ya virusi vya kompyuta vimetapakaa mtandaoni, hii haishii kwenye kompyuta tu, hapana mpaka kwenye simu zetu kuna mamilioni ya virusi vinavyoweza kudhuru simu zetu huko mtandaoni na ni muhimu kujua njia fasaha za kujizuia na mashambulizi ya virusi hivi. Ndio wengi tunajitahidi kuinstall Antiviruses katika simu zetu kama vile Avast, Android au Kaspersky lakini hii si ya muhimu sana kwa sasa. Njia pekee na ya usalama ni kuepuka kuinstall applications nje ya Google Play store.

10. Set User Accounts
Kama imetokea simu yako huitumii peke yako, au kama wewe ni baba na simu yako huwa inatumika na watoto wako au mkeo kwenye kucheza magemu, ni vizuri kuset user accounts ili kuruhusu ni nani atakuwa na uwezo wa kufungua nini katika simu yako. Kuanzia toleo la Android Lollpop mtumiaji ana uwezo wa kuset user accounts bila wasiwasi wowote. Fungua Settings–>Users–>Add Users na hapo utaset kulingana na matakwa yako.


as salaam aleikum mpendwa, Zimebaki siku chache sana simu ya Samsung Galaxy S9 itoke na tayari kwenye mitandao mbalimbali kumefurika tetesi mbalimbali juu ya ujio wa simu hii, lakini je ni vitu gani vinategemewa kuja kwenye simu hii.?
Kupitia makala hii tutaenda kuangalia baadhi ya vitu ikiwa pamoja na sifa zinazo tegemewa kuja kwenye simu hii mpya ambayo imepanga kuzinduliwa rasmi siku ya jumapili ya tarehe 25 mwezi huu.


 • Kamera

Kwa kuanza tuanze na kamera ambayo ndio sehemu inayotegemewa kuangaliwa sana kwenye toleo hili jipya la Galaxy S9. Simu hii inatarajiwa kuja na kamera mbili za nyuma zikiwa na uwezo wa Megapixel 12 kwa Galaxy S9 Plus na kamera moja kwa Galaxy S9. Kamera hizi zimeboreshwa zaidi na kuongezewa uwezo wa kuchukua picha vizuri hasa wakati wa usiku au kwenye mwanga mdogo.
 • Ulinzi

Mbali na matoleo ya nyuma ya Simu za Galaxy, toleo hili jipya la Galaxy S9 linakuja na ulinzi wa aina mpya ambao unaitwa Intelligent Scan, ulinzi huu ni mchanganyiko wa sehemu muhimu za Facial Recognition pamoja na Iris Scanner zote zikifanya kazi kwa pamoja.
 • Ujio wa 3D emoji

Itakuwa kama ilivyo sehemu ya Animoj kwenye iPhone X na kutumia simu mpya ya Galaxy S9 utaweza kutengeneza Emoji zenye kutembea na kufanya kazi kama ilivyo kwenye simu ya iPhone X. • Ujio wa Slow Motion
Hii ni sehemu ambayo itakuwa kwenye kamera na inategemewa kuongeza uwezo wa kamera ya Galaxy S9 kuchukua video za taratibu au Slom Motion.
Sifa Nyingine
Sifa zingine ambazo zinategemewa kuja kwenye simu hii mpya ya Samsung Galaxy S9 ni pamoja na kioo cha Inch 5.8 chenye teknolojia ya QHD na Super AMOLED curved display (570ppi / 529ppi), Processor ya Qualcomm Snapdragon 845 (kwa simu za  marekani) na Samsung Exynos 9810 (kwa simu za UK). Pia Samsung Galaxy S9 Plus inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6  na Galaxy S9 itakuwa na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4.
Na hivyo ndivyo baadhi ya vitu vinavyo tegemewa kuja kwenye kwenye simu mpya ya Galaxy S9 pamoja na S9 Plus.
Je' unaionaje samsung s9 niachie maoni yako hapo chini
As salaam aleikum mpendwa msomaji wa ukumbi huu, hakika kila mmoja wetu anapenda kumiliki simu kali tena simu janja ya kisasa, lakini wenda tunakosea wakati wa kufanya manunuzi, kwani sio kila simu inafaa kununua kuna nyingine ni matatizo hapa chini nimejaribu kukuelezea mambo ya kuzingatia wakati wa kununua simu


Epuka kuwa na haraka/pupa/ kukimbilia

Unapaswa kuepuka kuwa na haraka/pupa/kukimbilia kununua kitu ambacho utaweza kujuta baadae. Unahitaji kuchukua muda kufanya uchunguzi juu ya simu unayoitaka kabla ya kwenda kuinunua, sote tunajua haraka haraka haina baraka ukiwa na haraka itapelekea ukauziwa simu ya bei rahisi kwa pesa nyingi kutokana na kukosa umakini katika manunuzi yako.

Epuka ushindani

hasa kwa dada zangu, Hatupaswi kuwa na mashindano yoyote wakati wa kununua simu nzuri. Aina ya simu za mkononi ambazo wengine wanatumia hazipaswi kukuongoza kununua yako. Huna haja ya kushindana, sio lazima. Nunua kulingana na pesa zako zinazoweza kumudu, kwani unaweza kujikuta unashindwa kufanya mambo ya msingi kutokana na kufikiria kuwa na simu kama ya jirani yako wakati uwezo njaa zimekata break.

Epuka kununua smart phone iliyotumika

mwaka jana nikiwa kituo cha polisi rumande nilisikia mashtaka mengi kuhusu simu, kila aliyelalamika alijitetea kwa kusema kuwa alinunua kwa mtu yeye hausiki, Watu wengi hutumia au hununua simu ya mkononi iliyotumiwa na hatimaye kupata matatizo mengi baadaye. Ili kuepuka hili, unahitaji kununua simu (smart phone) ambayo ni mpya na inayoweza kudumu/kuishi kwa muda mrefu. Hasa kwenye uwezo wa betri.

Epuka kununua smart phone mitaani

Hili jambo siku hizi limezoeleka sana. Watu wengi wananunua smart phones mitaa kwa kigezo cha bei rahisi kisa simu anayoinunua imetumika kwa muda fulani. Wengi wa wanaouza smart phones mitaani ni walaghai na wanaweza kukupa simu mbovu na mbaya. Ni dhahiri kabisa wengi tushawahi kuuziwa simu mbovu mitaani. Ni vyema kujishauri na kufanya maamuzi sahihi kabla ya kununua simu huko mtaani ili kuepuka hayo matatizo hasa kutapeliwa.

Neno la Muandishi: sio simu zote zinazouzwa mitaani ni Fake au hazina Ubora ila ni vema ukanunua simu mpya.
As salaam aleikum. Je, unakumbuka simu za mkunjo za kipindi cha miaka ya 90 na 2000? Kama ndio basi zimerudi tena lakini katika kiwango cha ubora wa juu, muonekano wa kuvutia zaidi pamoja na teknolojia ya kisasa.

Kampuni ya Samsung ikishirikiana na China Telecom imetangaza uzinduzi wa simu ya bei ghali ya mkunjo yenye vioo viwili inayofahamika kama Samsung W2018.

Uzinduzi wa simu janja hiyo umefanyika Desemba mosi mwaka jana huko Xiamen, nchini China ukiambatana na sherehe za kutimia miaka 15 ya toleo la familia ya W kwa simu za Samsung Galaxy na miaka 25 ya soko la Samsung nchini China.

Samsung W2018 ambayo sifa zake za ndani inafanana sana na Sansung Galaxy S8, inakuja na kioo cha ukubwa wa nchi 4.2 chenye teknolojia ya AMOLED pamoja na RAM yenye ukubwa 6GB na ukubwa wa uhifadhi wa ndani wenye ukubwa wa 64GB na 256GB.
Uzuri wa simu hii utaweza kutumia aidha kioo cha nje au ndani baada ya kuikunjua simu yako. Mfano unaweza kutumia kioo cha ndani na ukabadili kwa kutumia kioo cha nje kwa kazi ileile iliyokuwa kwenye kioo cha ndani na ukaendelea nayo ama ukaendelea na kitu kingine kipya.

Pia itakupa na uwanja mpana wa kutumia baobonye/kicharazio (keyboard) halisi au ya kugusa (Touch).

Ukubwa wa Betri katika Samsung W2018 ni 2,300mAh na itakuwa na mfumo endeshi wa Android Nougat. Simu hiyo itakuwa katika rangi nyeusi, Fedha na Dhahabu.

Kwa upande wa kamera kutakuwa na kamera ya nyuma yenye 12MP na kamera ya mbele yenye 5MP na kuweza kurekodi video kwa teknolojia ya 4K. Simu hiyo itaendeshwa na  prosesa ya Snapdragon 835.

Hata hivyo kikwazo kikubwa cha simu hiyo ni bei yake. Kama ulidhani iPhone X ni ghali zaidi, basi kwa Samsung W2018 ni ghali zaidi.

Ingawa bei haijawekwa rasmi lakini inaelezwa bei ya Samsung W2018 itauzwa kwa Dola za kimarekani 2,400 ambazo ni takribani Tsh 5,399,040 ambazo pesa hizo zinamuwezesha Mtanzania wa kawaida kumudu kununua kiwanja cha ukubwa mzuri kilichopimwa na serikali.

Hii sio simu janja ya kwanza ya Samsung Galaxy kuwa ya mkunjo. Simu janja ya mkunjo nyingine ilizinduliwa mapema mwaka huu inayofahamika kwa jina la Samsung leadership 8 ambayo nayo inapatikana kwa soko la China pekee.

Simu ya Samsung W2018 kwa sasa itapatikana katika soko la China pekee na hakuna taarifa rasmi kama itapatikana katika masoko mbalimbali katika nchi zingine.

Nini maoni yako kuhusiana na makala haya. Je una swali lolote. kwa maoni au maswali kuhusu makala haya usisite kutuandikia hapo chini nasi tutakujibu haraka iwezekanavyo.
As salaam aleikum, USB Debugging kama inavyosomeka katika sehemu ya settings (mipangilio) ya mfumo endeshi wa android inaonekana kama kitu kigumu sana kwa baadhi ya watumiaji wa simu za mfumo endeshi huu. Hapana, USB Debugging ni rafiki yako wa karibu na unapaswa kumtumia pale unapolazimika.
Kwa kifupi USB Debugging ni njia inayoruhusu simu yako ya android kuweza kuhamisha mafaili kati yake na kompyuta. Kwa maana ya kitaalamu zaidi, USB Debugging ni njia ya kutest (kujaribu) au kugundua bugs (mapungufu) katika application za android inayotumiw zaidi na madeveloper wa applications mbalimbali za mfumo endeshi huu.

Mara nyingi USB Debugging hutumika katika kujaribu software mbalimbali zilizotengenezwa na Android Studio, hapa madeveloper  watakuwa wanaelewa zaidi. Kuinstall Custom ROM, Kuroot au hata kubadilisha baadhi ya vitu katika software.

Jinsi ya kuwasha (Enable) USB Debugging

Kufungua USB Debugging, inakupasa kufungua kuruhusu ‘Developers Options’ katika simu yako kwa sababu katika matoleo ya sasa huduma hii huwa inafichwa. Fuata hatua zifuatazo kufanya hivyo;

Fungua sehemu ya settings kwenye simu yako, shusha chini mpaka katika sehemu iliyoandikwa About Phone.
Baada ya kufungua About Phone, shuka mpaka chini kwenye sehemu iliyondikwa ‘Build Number’, bonyeza mara saba hapo ili kufungua developers options. Baada ya kubonyeza mara saba utakuja ujumbe utakaokupa tahadhari kuwa unaelekea kufungua developers options.
Baada ya hapo rudi nyuma kwenye menu yako ya settings na utaona Developers Options ipo katika settings, ifungue na anza kushusha chini kuitafuta USB Debugging na iruhusu.
Kwa watumiaji wa matoleo ya chini ya Android 2.3 wanaweza kufungua moja kwa moja deveopers options kwa sababu inakuwa haijafungwa na wataweza kuona hii setting ya usb debugging.
Kingo Root ni moja ya njia maarufu ambayo inatumiwa na watu wengi ili ku-root simu zao. Lakini hii njia huwa haifanyi kazi kwenye kila simu. Zipo baadhi ya simu ambazo hazifai kabisa kuroot kwa kutumia Kingo Root

HTC

Simu nyingi za aina ya HTC huwa hazifai kabisa ku-root kwa kutumia Kingo root. Moja ya sababu inayo sababisha hizi simu zisifae kuroot kwa kutumia kingo root ni ulinzi mkali ambao HTC wanaweka kwenye simu zao. Locked Bootloader na S-ON ni ulinzi ambao HTC wanaweka kwenye simu zao ili kuzuia mtumiaji asiweze ku-access au ku-modify system files. Ndio maana ili uweze ku-root simu za HTC inabidi kwanza unlock bootloader na uhakikishe S-ON ipo S-OFF. Tazama picha chini kuelewa zaidi.

SAMSUNG

Kama ilivyo HTC, Samsung nao wanaweka ulinzi mkali ambao unazuia simu zao kuwa ngumu sana ku-root kwa kutumia Kingo Root. Zipo baadhi ya simu za Samsung ambazo zinakuja na locked bootloader. Ukiachana na locked bootloader, Samsung wana ulinzi mwingine mkali unao julikana kama Knox. Knox security inamzuia mtumiaji asije modify au ku-access system files. Ili uweze ku-root simu za samsung basi ni lazima Knox security iwe turned off. Tazama picha chini ili kuelewa zaidi

HUAWEI

Huawei pia wapo kwenye hili kundi ambalo huwezi ku-root simu zao kwa kutumia kingo root. Zipo baadhi ya simu za huawei ambazo utaweza ku root kwa kutumia kingo root lakini ni chache sana. Huawei pia ana lock bootloader za simu zao na kusababisha kuwa vigumu sana ku-root simu za huawei. Sio kwamba Huawei hawa ruhusu simu zao kuwa rooted, jibu ni kwamba Huawei wana ruhusu simu zao kuwa rooted lakini wanapenda ufwate utaratibu maalumu walioweka ili endapo uta root simu yao basi ujue kabisa utakuwa umepoteza warranty yako
Samsung Galaxy J7 (SM-J700F) ni moja ya simu zenye uwezo mkubwa licha ya kuwa bei nafuu. Kitu kingine kizuri kuhusu hii simu ni kwamba ina kuja na android 6 (marshmallow) na pia unaweza kutumia SIM card mbili kwa wakati mmoja. Leo tutaona jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy J7 (SM-J700F)
Custom Recovery ni jambo la muhimu sanaa hasa pale unapotaka kuweka custom rom. Kwa wale wanaopendelea kuweka custom rom kwenye simu zao basi lazima watakuwa wanafahau umuhimu wa custom recovery.

Vigezo na Masharti

 • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
 • 1: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy J7 (SM-J700F)
 • 2: Hakikisha simu yako inatumia android 6.0.1(marshmallow)
 • 3: Soma maelekezo kwa umakini kisha ndio ujaribu kwenye simu yako
 • 4: Hakikisha ume install samsung drivers kwenye computer yako.

STEP 1

Download ODIN program kwa kutumia link chini kisha tengeneza folder kwenye desktop yako. Liweke hilo file ulilo download ndani ya folder kisha lifungue au extract
http://dl.sammobile.com/Odin3_v3.10.7.zip

STEP 2

Download TWRP Recovery kwa kutumia link chini kisha liweke hilo file kwenye folder ulilo tengeneza kwenye STEP 1
https://dl.twrp.me/j7elte/twrp-3.0.2-0-j7elte.img.tar

STEP 3

Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha tafuta kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyo onekana chini. Kama hicho kipengele haukioni basi nenda kwenye about phone kisha shuka chini mpaka utakapoona kipengele kinachosema build number kisha kibonyeze haraka haraka kama mara saba kisha rudi tena kwenye setting na uangalie kama developer options imetokea

STEP 4

Fungua developer options kisha hakikisha umeiwasha (turn on) halafu umeweka tick ua umekiwasha kipengele kinachosema USB debugging kama picha inavyo onekana chini.

STEP 5

Ukiwa hapo hapo kwenye Developer option, hakikisha kipengele kinachosema OEM UNLOCK kipo on kama picha chini

STEP 6

Zima simu yako kisha iwashe kwenye downloading mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu kwenye downloading mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kupunguza sauti(vol down button)} na cha kuwashia (power button) mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 7

Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Kwa wale watoto wa mama wenye wasiwasi kwamba simu zao zita haribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi toa battery kisha rudishia washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezoNOTE
Kabla hujaendelea hakikisha kwenye simu yako sehemu iliyoandikwa Product Name ni SM-J700F. Kama ni tofauti na hivyo tafadhali nakuomba usiendelee maana utaaribu simu yako.

STEP 8

Rudi ndani ya lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, kisha double click ile program inayoitwa odin ambayo ulipata baada ya ku extract file ulilo download kwenye STEP 1. Endapo upo sahihi utapata muonekano kama picha chini kwenye computer yako

STEP 9

Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy J5 (SM-J700F) halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chini

STEP 10

Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file ulilo download kwenye STEP 2 ambalo linaitwa twrp-3.0.2-0-j7elte.img.tar kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.

STEP 11

Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.

STEP 12

Simu yako itazima na kujiwasha. Chomoa USB yako kutoka kwenye computer. Utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako. Kujua kama umefanikiwa kuweka custom recovery unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuongeza sauti(vol up button)} na cha kuwashia (power button) kwa muda wa sekunde kama tatu au nne kisha achia. Baada ya hapo utaona custom recovery yenye muonekano kama picha chini.Mpaka hapo tumefikia mwisho. , kama unataka kusaidiwa ku update Samsung Galaxy J7 au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye kupitia whatsapp namba +255652732383.Can't talk, whatsapp only.
Mara nyingi tumekuwa tukinunua simu dukani bila kuijaribu kiukamilifu hivyo baadhi ya matatizo kuyajua bada ya siku kadhaa kupita, na urudishapo simu hiyo waweza pata usumbufu mkubwa sana kutoka kwa mmiliki wa duka, Leo nakupatia CODE ambazo utatumia kujaribu simu mpya dukani bila kuwako na line yeyote ndani ya simu na waweza kujua kama simu hiyo inamatatizo ya kiutendaji au Laa.

Code hizo ni -:

 1. *#*#4636#*#*  –  Code hii itakupatia maelezo kuhusu simu yako, maelezo kuhusiana na battery na matumizi
 2. *#*#34971539#*#* kuonesha maelezo yote kuhusiana na kamera na ubora wake.
 3. *#*#232339#*#* AU *#*#526#*#* Njia ya kujaribu ufanyaji kazi wa Wireless
 4. *#*#1472365#*#*  – kuangalia uhai wa  GPS
 5. *#*#1575#*#* – Njia mbadala ya kujaribu GPS
 6. *#*#0283#*#* – Jinsi ya kujaribu ‘Packet Loopback’
 7. *#*#0*#*#* – Majaribio ya tach screen yako (LCD display)
 8. *#*#0673#*#* AU *#*#0289#*#*  – Majaribio ya sauti
 9. *#*#0842#*#* – Majaribio ya sauti mtetemo (Vibration) na Mwito wa muwako (Backlight)