Kutengeneza Bootable USB katika Windows 10 bila ya kutumia Software ndio njia pekee rahisi na  ya usalama zaidi ya kuinstall Windows kwa sasa.

Siku hizi watu wachache sana wanaochoma (burn) ISO ya Windows  kwenye cd na kuitumia katika installation, wengi wanatumia usb flash sababu ni njia ya haraka na rahisi zaidi katika kufanya zoezi hilo. Kuna tools nyingi zinazosaidia katika zoezi hilo na kufurahisha zaidi mpaka Microsoft wenyewe wametengeneza baadhi ya tools za kusaidia zoezi hilo, ila kuna njia rahisi na ya haraka ya kufanya flash yako iwe bootable bila ya kutumia software yoyote ile.
Hebu tuangalie zoezi hilo:

Njia za kufuata ili kutengeneza Bootable USB katika Windows 10 bila software yoyote ile

 • Chomeka flash yako unayokusudia kuifanya kuwa bootable, Angalizo: zingatia ukubwa wa flash na ukubwa wa faili lako.
 • Fungua ukurasa wa komandi (Command Prompt) kwa kutafuta Command Prompt katika Task bar, au unaweza ukabonyeza Windows+R kwa wakati mmoja na sehemu ya kuandika itatokea, andika cmd katika sehemu hiyo alafu bonyeza Enter
 • Kama utajaribu kufungua Command Prompt kwa kutumia Task bar chagua Run as administrator
 • Window mpya nyeusi (Command Prompt) itatokea, hiyo ndio sehemu ya kuandika komandi, andika disk part na bonyeza Enter, subiri kwa muda Diskpart itafunguka katika Windows nyingine.
 • Baada ya window ya diskpart kufunguka, andika list disk na diski zote zilizopo kwenye kompyuta wako kwa muda huo zitafunguka, na zitakuwa na herufi na zimepangwa kwa namba kuelekea chini.
Mara nyingi utakutana na aina mbili za diski, Disk 0 kwa hard disk na Disk 1 kwa flash na ukubwa wake.
Kwa kuwa tunaenda kutengeneza Bootable ISO kwenye flash hivyo tutadili na Disk 1
 • Andika select disk 1 alafu bonyeza enter. Utapata ujumbe unaosema Disk 1 is now the selected disk. Hii inamaanisha chochote utakchokuwa unafanya hapa kitaathiri diski hii moja kwa moja.
 • andika clean alafu bonyeza enter, clean command itafuta kila kitu kilichopo katika diski yako. ikmaliza ujumbe Diskpart succeeded in cleaning the disk utatokea.
 • Andika create partition primary alafu bonyeza enter utapata ujumbe Diskpart succeeded in creating the specified partition
 • Andika select partition 1 alafu bonyeza enter, itachagua partition 1 kama active partion.
 • Bonyeza active alafu bonyeza enter , hii itaactivate partition hiyo
 • Andika format fs=ntfs quick alafu bonyeza enter . Komandi hii itaifanya flash hiyo kuwa na format ya ntfs file system kwa haraka zaidi.
 • Andika exit alafu bonyeza enter, hii itaifunga Diskpart program, ila usiifunge window ya command prompt.
 • Hapa kabla hatujaendelea  hebu tuangalie baadhi ya vitu kwa uangalifu zaidi, angalia flash yako imepewa herufi gani, katika kesi yetu ina herufi drive G: na file lako la Windows unalotaka kulikopi lipo kwenye drive E:.
 • Kwa kawaida Command Prompt’s active directory for Administrator permission lipo kwenye C:\Windows\System32>. Hapa tunatakiwa kuielekeza Command Prompt ichukue mafile kutoka katika drive E:
 • Andika E: alafu bonyeza enter alafu active directory litabadilika lenyewe na kuwa katika E:
 • Andika cd boot alafu bonyeza enter . Hapa active directory litabadilika na kuwa E:\boot>
 • Andika bootsect /nt60 g: alafu bonyeza enter itatengeneza boot sector katika G: drive (USB Flash drive)
 • Andika exit alafu bonyeza enter kufunga command prompt.
Mpaka hapa utakuwa tayari umeshatengeneza bootable USB na flash drive ipo tayari kwa zoezi zima la kuinstal windows.
Ili kuinstall windows katika USB Drive tunatakiwa kuhamisha (kucopy) file zima la windows kutoka katika drive E: na kulipeleka katika Flash Drive.
 • Kufanya hivi kirahisi na kwa uhakika, fungua tena command prompt, baada ya kuifungua andika xcopy e: \ *. * G: \ / E / H / F alafu bonyeza enter. Subiri mpaka mafaili yote yahamie kwenye flash drive.
Baada ya hapo Flash itakuwa tayari kwa zoezi zima la kuinstall Windows kwenye Kompyuta nyingine.
Nadhani utakuwa umefurahia makala hii, kama unaswali lolote tafadhali uliza katika sehemu ya maoni hapo chini.
Axact

Ibrahim Riyad Houmud

As Salaam Aleikum, I'm Ibrahim Riyadi Houmud, Founder and CEO of RiyadiBhai blog from Mororgoro, Tanzania. I started this blog as a Passion and it now empowering thousands of readers around the globe.Here I usually share news, Adsense tips, wordpress, gadget, widget, Themes, windows, etc.

Post A Comment:

0 comments:

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa