JINSI YA KUJIUNGA NA ADSENSE HATUA KWA HATUA

Habari tena karibu hapa tujuzane haya na yale baada ya kufahamu jinsi ya kujiunga na seebait kama ulipitwa soma hapa Jinsi ya kujiunga na seebait kutokana na maoni na maombi ya wasomaji wangu nimeona nitimize haja za wasomaji wangu kwa kuwafahamisha kuhusu kujisajili na adsense je unajua adsense ni nini soma hapa jinsi ya kupata pesa kupitia adsense 

Tukumbuke kila kitu kina sheria zake na utaratibu wake hivyo ni vema kufamu kuhusu sheria na sera za google , kwanza fahamu ya kuwa adsense hawasapoti lugha ya kiswahili kufahamu zaidi soma hapa sababu za kiswahili kutokubaliwa katika mfumo wa adsense hivyo ikiwa unaweka machapisho kwa lugha ya kiswahili katika blog yako ni vigumu kukubaliwa.

baada ya kufahamu hayo machache nafikiri tuanze lakini unaweza kuniachia maoni yako kama hujaelewa maelezo yangu



Ingia katika blog yako kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa ernings
Utaona sehemu imeandikwa Sign Up for adsense kama huoni na unatumia domain kama SwahiliTech.Net ingia hapa https://www.google.com/adsense/signup watakuletea chagua hili 
bonyeza sign in kama umetumia link watakuletea sehemu ya kujaza website yako na lugha lakini kama umetumia blogger moja kwa moja sehemu ya website watakujazia kisha wewe utajaza lugha
lugha zote watakazokuletea hapo zinasapoti mfumo wao kwahiyo ni chaguo lako hapo ila mimi huwa nachagua kiingereza baada ya kuchagua lugha bonyeza Accept association watakuletea muonekano huu
utajaza form hiyo kama wanavyokuomba namba ya simu time zone sehemu ulipo yaani nchi na mkoa jina n.k kisha utasubmit chini kabisa ya hiyo fomu kisha watakuletea muonekano kama huu chini pichani
Bonyeza hapo Continue watakurudisha kwenye dashibodi ya blog yako sehemu ya ernings utaona ujumbe kuwa adsense yako ipo kwenye mchakato itakuwa aproved baada ya muda kidogo, hivyo wataiangalia kama umekidhi vigezo na mashariti yao watakukubalia ndani ya siku tatu na utaona muonekano huu kama utakuwa umekubaliwa
mpaka hapo utakuwa umefanikiwa na kuhusu kupokea pesa zako soma hapa Jinsi ya kupokea pesa yako kutoka adsense mpaka hapo nafikiri utakua umepata muangaza japo kidogo natumaini makala yangu haijakamilika ila wewe  unaweza kuikamilisha kwa kuniuliza swali hapo kwenye coment nami nitakujibu ili tukamilishe makala hii, pia sambaza upendo kwa blogger wenzetu kwa kusambaza makala hii nao wajipatie ujuzi huu bure, nimekufahmisha bure basi nawe toa bure

15 Comments

  1. kwa mfano kama account yangu imekuwa approved na youtube nweza kuitumia na kwenye blog?

    ReplyDelete
  2. Inawezekana tena inachukua muda mfupi zaidi kukubaliwa lakini kuna trick ambayo inabidi utumie ambapo itakulazimu kufungua na admob, pia ni lazima blog yako iwe imekidhi zigezo vya google adsense. Nikipata wasaa mzuri nitawaletea trick hiyo ya kufungua blog adsense kupitia youtube

    ReplyDelete
  3. Kwa mfano kuna Account ya adsense ambayo ilikuwa imekubaliwa Adsense katika blogu nyingine but haitumii tena katika hiyo Blog.. je inaweza hamishiwa katika blog nyingine na sio walioungia mwanzo...

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndio inawezekana lakini katika email utakayotumia inabidi iwe haijawahi kufanyia maombi yeyote ya Adsense

      Delete
    2. iyo e-mail ilikubaliwa adsense but mwenyew akatoa matangazo ya adsense na pia e-mail hakuitumia tena katika blog hio... so inaweza tumiwa katika blog nyingine bila kuomba tena mkuu

      Delete
  4. kaka nahitaji kujua youtube adsense unajiunga vipi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma makala hii http://www.swahilitech.net/2017/05/jinsi-ya-kuingiza-pesa-kupitia-youtube.html?m=1 nimeelezea kwa upana na mifano ya picha

      Delete
  5. asante kwa msaada ila ningepata mawasiliano yako ingekuwa poa namba yako ya simu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaweza kutumia email hii riyadibhai@gmail.com karibu

      Delete
  6. nilijiunga na adsese wakasema wanarevew ndani ya siku 3 wataaprove lakini naona kimya leo iku ya 4

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inategemea labda haujakidhi vigezo au uliomba wakati wa siku za weekend.

      Delete
  7. Je kama mimi sına akaunti bankı naweza jiunga na mfumo huo au ni lazima uwe na account bank?? Lakini pia katika blog yangu naweza kuchapisha machapisho ya lugha ya kiswahili na kiingereza??

    ReplyDelete
    Replies
    1. unaweza kujiunga hata kama hauna bank akaunti, kuhusu machapisho lazima yawe ya kiingereza ili kuepeuka kufungiwa akaunti yako

      Delete
  8. kaka nina account mbili youtube moja nimeiunga adsense naweza ongeza na yaut pili ili ili mapato yawe yanakuja kwa pamoja ila zote zinz email tofa

    ReplyDelete

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa