Articles by "Mobile"
Showing posts with label Mobile. Show all posts

As salaam aleikum mpendwa msomaji wa ukumbi huu makini kuhusu uchambuzi wa masuala ya Tech, wenda ilishawahi kukutokea unahitaji kununua simu lakini haujui ni vitu gani vya kuzingatia basi leo Riyadi Bhai nimekuwekea vitu vya msingi ambavyo unatakiwa kuvizingatia kabla ya kununua simu mpya
● Battery
Fikiria: Wewe ni mtumiaji ambaye una apps nyingi na kuzifungua wakati huo huo? Je! Unajiona kuwa mtumiaji mkubwa wa apps za video au kucheza games? Matumizi makubwa kwenye mtandao hufanya kupunguza betri kwa kasi. Ikiwa wewe ni wa mtumiaji mkubwa, basi ni bora kwenda kwenye simu yenye battery yenye kutunza chaji.

● Memory
Simu za mkononi zina aina mbili za memory - Random Access Memory(RAM) na Read Only Memory (ROM). RAM, pamoja na processor ya simu yako (angalia chini), huamua kasi ya simu na urahisi wa kuitumia. ROM kama watu wengi tunavyojua kuwa uwezo wa kuhifadhi. Hii ni memory ambayo hutumiwa kuhifadhi programu za OS, apps na video zote, picha na nyimbo ambazo unataka kuhifadhi kwenye simu.Hivyo, nasisitiza kuwa simu zenye RAM kubwa zitakuwa na kasi zaidi na wale walio na ROM kubwa watahifadhi vitu vingi zaidi. Mtumiaji wa wastani hili kufurahia simu yako unapaswa kuwa na 2 GB RAM na 16 GB ROM. Lakini kama wewe ni mtumiaji mkubwa, nenda kwenye simu yenye angalau 3-4 GB RAM na 64GB ROM. Kuongeza ROM yako unaweza kutumia micro SD, lakini kumbuka, sio simu zote unaweza kuweka micro SD.

● Camera
Kuna aina nyingi za vitu vinavyozunguka camera na kufanya iwe bora. Kuna kampuni za simu zinazojaribu kutoa megapixels zaidi mfano kwasasa simu nyingi wanaweka 20MP - 48 MP wakati inaweza pitwa na simu yenye 16 MP kwa ubora wa picha. Usiruhusu hii iwe sababu ya wewe kuwa mjinga. Kwani kamera yenye megapixels zaidi haina matokeo ya picha bora kama tunavyodhani. Mbali na megapixels, picha nzuri ni kazi ya vitu kama ISO standard, kasi ya autofocus. Ukiwa ni mpenzi wa kupiga picha nyingi, inakupasa uende kwenye simu yenye kamera ya 12 au 16 MP ambayo ina aperture ya f / 2.0 au chini, kwa picha bora hata kwenye mwanga mdogo. Ikiwa matumizi yako ya kamera hayawezi kuwa makubwa, simu yenye kamera ya 8-12 MP na aperture f / 2.2 itafaa kwa matumizi yako.

● Processor
Kama vile kwenye upande wa kamera za simu,kuna vitu vingi vinachangia processor iwe na nguvu. Simu nyingi zina Snapdragon, MediaTek nk. Angalia kasi ya processor ambayo imeelezwa kwa GigaHertz (GHz) simu ikiwa na processor nzuri utaweza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.

● Display
Simu iliyo na display ya 5.5 - 6-inch HD au QHD ni chaguo bora. Hii itakuwezesha kufurahia ubora wa muonekano wa screen pia inakuwa rahisi kuishika na kuiweka katika mfuko wako.

● Operating System
Hapa napendelea Android, pia angalia UI na hiyo Based Android OS. Kama haupendi mbwembwe nyingi chukua Android Stock (Android One). Pia kuna baadhi ya hizi Stock firmware zinazokuja na simu zinakuwa na bloatware, na hivyo kupunguza ROM na RAM ya simu. Kwa hiyo, jaribu kuangalia hili kabla ya kufanya uamuzi.

● Cost
smartphones huja kwa bei ambazo hutofautiana sana. Ni wazi, bei zinatokana na specs, simu yenye specs za juu thamani yake huwa juu pia kwa mfano: processor, memory, camera na display.Lakini usiruhusu bajeti yako ikuzuie kununua smartphone bora unayotaka, unaweza kujichanga hata miezi mitatu upate kitu bora zaidi.

Kwa uelewa wangu hivyo ndio vitu muhimu vya kuzingatia.
Kampuni ya LG kama ilivyo kampuni ya Samsung, kila mwaka inazindua simu mbili ambazo ni flashship, flagship ni Simu zinazobeba Jina la kampuni au ni simu ambazo ndio muhimu sana kwa kampuni husika. Kwa mwaka huu simu ya LG G7 ThinQ na simu hii mpya ya LG V40 ThinQ ndio simu ambazo ni flagship kutoka kampuni ya LG na kwa sababu ya hilo sifa nyingi za simu hizi zinafanana.
Sasa tukiangalia simu hii mpya ya LG V40 ThinQ, simu hii inakuja na mabadiliko mengi mbalimbali lakini mabadiliko makubwa kwenye simu hii ni pamoja na simu hii kuwa na uwezo wa kamera 5. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera mbili ambazo moja ya kamera hizo ni kwaajili ya kupiga picha za kawaida za selfie, ambayo inakuja na Megapixel 8 na nyingine ni kwaajili ya kupiga picha za Group Selfie (wide lens) ambayo inakuja na uwezo wa Megapixel 5.
Kwa nyuma simu hii ya LG V40 ThinQ inakuja na kamera tatu, ambazo kamera moja ni kamera ya kawaida na nyingine ni super wide angle lens na nyingine ni telephoto lens. Kamera ya kawaida iliyoko upande wa kulia inakuja na uwezo wa Megapixel 12 yenye f1.5 lens, Kamera ya pili iliyoko katikati ambayo hii ni super wide angle lens inakuja na uwezo wa Megapixel 16 yenye f1.9 lens na kamera ya mwisho ambayo ipo upande wa kushoto ambayo hii ni telephoto lens yenyewe inakuja na uwezo wa Megapixel 12 yenye f2.4 lens.
LG V40 ThinQ inakuja na uwezo mzuri sana na wa kipekee kwenye kamera hizi kwani utakuwa na uwezo wa kuweza kuona (preview) vidokezo vya picha za kamera hizo zote tatu moja baada ya nyingine kwenye kioo cha simu yako hata kabla ya kupiga picha, kitu ambacho hakipo kwenye simu zote zilizowahi kutoka zenye uwezo wa kamera tatu au zaidi. Maana yake ni kuwa unaweza kupiga picha tatu tofauti kwa kutumia kamera moja baada ya nyingine ndani ya kamera hizo tatu zilizopo kwa nyuma ya simu hizo.
Tukiachana na kamera kwa upande wa sifa LG V40 ThinQ inakuja na sifa za kawaida na kama vile kioo cha inch 6.4 chenye ukingo wa juu maarufu kama notch, processor ya Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 ambayo ipo sambamba na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 6, Sifa nyingine za LG V40 ThinQ ni kama zifuatazo.
Sifa za LG V40 ThinQ
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3120 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~537 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver)
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset
 • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele, kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 8 yenye f/1.9, 1.4µm na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 5 yenye f/2.2, 1.4µm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.5, 1.4µm, 3-axis OIS, PDAF & laser A na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.9, 1.0µm, no AF na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.4, 1.0µm, 2x optical zoom, OIS, PDAF. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3300 mAh battery yenye uwezo wa fast charging  yenye uwezo wa kujaza asilimia 50% kwa dakika 36 (Quick Charge 3.0).
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za New Aurora Black na New Moroccan Blue.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line ya Nano-SIM, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inayo uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP68.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer na color spectrum
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya LG V40 ThinQ
Simu hii mpya inatarajiwa kupatikana kuanzia siku ya October 18 huko nchini marekani na bei yake itakuwa inatofautiana kutokana na kuwa simu hii itapatana kupitia kampuni mbalimbali za simu nchini marekani. US Cellular itakuwa inauzwa simu hii kwa dollar $900, na kupitia T-Mobile itakuwa inauzwa dollar $920, Sprint itapatikana kwa dollar $960 na kuptia Verizon simu hiyo itapatina kwa dollar $980. Kwa Tanzania simu hii inawezekana ikauzwa kwa bei zaidi kuanzia dollar za marekani $1000 bila kodi sawa na Tsh 2,290,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika.
Kampuni ya Nokia kupitia HMD Global hivi leo imefanya tamasha lake la uzinduzi rasmi wa simu yake mpya ya Nokia 7.1, Simu hii ni toleo jipya la simu ya Nokia 7 ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi october mwaka jana 2017. Simu hii mpya ya Nokia 7.1 inakuja na maboresho na muonekano bora zaidi huku ikiwa na kioo kikubwa zaidi kuliko Nokia 7 ya mwaka jana.
Simu hii ya Nokia 7.1 inakuja na kioo cha inch 5.84 chenye resolution ya 1080 x 2280 pixel pamoja na uwiano wa 16:9, kioo hicho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD na pia kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch.
Nokia 7.1 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 636 SoC ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 au GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 32. Kwa upande wa kamera simu hii inakuja na kamera ya mbele yenye Megapixel 8 huku kamera za nyuma ambazo ziko mbili zenyewe zinakuja na uwezo wa Megapixel 12 na Megapixel 5 ambazo zote zimetengenezwa na Zeiss optics. Kamera hizo za nyuma zinakuja na sehemu mpya ya “bothie” ambayo in akupa uwezo wa kupiga picha kwa kutumia kamera zote za mbele na nyuma kwa wakati mmoja.
Simu hii mpya ya Nokia inapewa nguvu na battery yenye uwezo wa 3,060 mAh ambayo pia inakuja na uwezo wa Fast Charging yenye uwezo wa kuchaji simu hii kwa haraka. Sifa nyingine za Nokia 7.1 ni kama zifuatazo.
Sifa za Nokia 7.1
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.84 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 16:9 ratio (~432 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie (Android One)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 32 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu tatu moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4 na ya mwisho ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 24mm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1.28µm, Dual Pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4, 1.12µm, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Zeiss optics, dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3060 mAh battery battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa mbili za Gloss midnight blue, na gloss steel.
 • Mengineyo – Bado haijajulikana kama inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Nokia 7.1
Kwa upande wa bei simu hii inatarajiwa kuanza kuagizwa kuanzia October 5 huku tarehe ya kufikiwa na simu hizo kama uliagiza itakua kuanzia tarehe 28 ya mwezi huu October. Kwa upande wa Nokia 7.1 yenye GB 32 na RAM ya GB 3 itauzwa kwa dollar za marekani $349 sawa na Tsh 797,000 bila kodi. Toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 4 lenyewe litauzwa kwa dollar $401 ambayo ni sawa na Tsh 913,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.
Kampuni ya Huawei hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Huawei Y9 (2019), Simu hii inakuja na maboresho mapya ukitofautisha na toleo la Huawei Y9 (2018). Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.5 chenye resolution ya 1080 x 2340 pixel ambapo pia kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama top notch.
Simu hii pia inakuja na processor ya Kirin 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6 huku simu nzima ikiwa inaendeshwa na battery kubwa yenye uwezo wa 4000mAh. Huawei Y9 (2019) inakuja na kamera mbili kwa nyuma na kamera mbili kwa mbele, huku kwa nyuma kamera hizo zikiwa na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 2. Kwa mbele Huawei Y9 (2019) inakuja na kamera hizo mbili zenye uwezo wa Megapixel 13 na Megapixel 2, sifa nyingine za Huawei Y9 (2019) ni kama zifuatazo.
Sifa za Huawei Y9 (2019)
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~396 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Hisilicon Kirin 710 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 128 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 ambayo ni depth sensor.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye depth sensor. Kamera zote za nyuma zinasadiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Blue Swarovski na Aurora Purple.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Huawei Y9 (2019)
Kwa upande wa bei ya simu hii bado kampuni ya Huawei haijatangaza bei ila endelea kutembelea Swahili Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata taarifa zaidi kuhusu bei ya simu hii.
Kampuni ya Motorola hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Motorola One Power au P30 Note huko nchini India, simu hii inakuja na muonekano unaofanana sana na iPhone X huku ikiwa na ukingo wa juu maarufu kama top notch tofauti na simu nyingi kutoka kampuni hiyo.
Motorola One Power au (P30 Note) inakuja na Battery kubwa ya 5000mAh ambayo kwa mujibu wa kampuni hiyo inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku mbili kwa kuchaji mara moja tu, vilevile motorola inadai kuwa simu hii pia inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku moja na masaa kadhaa iwapo utakuwa unacheza game mfululizo kwenye simu hiyo.
Mbali na battery ambayo ndio maboresho makubwa ya simu hii, Motorola One Power (P30 Note) inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS display ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2246 pixels pamoja na uwiano wa 18.7:9 ratio.
Simu hii pia inakuja na mfumo wa Android 8.1 ambao unaweza ku-update hadi kwenye mfumo mpya wa Android 9 Pie. Simu hii inatumia processor ya Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 3, GB 4 na GB 6. Motorola One Power inakuja na kamera mbili za nyuma ambapo kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 16 na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 5. Sifa nyingine za Motorola One Power ni kama zifuatazo.Sifa za Motorola One Power
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCS capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2246 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~402 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 32 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu tatu moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4 na ya mwisho ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 yenye f/2.0, 1.25µm.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye ff/2.2, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging (15W)
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa moja ya Midnight Black.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Motorola One Power
Kwa upande wa bei, simu hii imetangazwa hivi leo kuanza kupatikana huku inchini India ambapo itakuwa inaanzia kuuzwa kwa rupee ya india Rs 15,999 ambayo ni sawa na Tsh 503,000 bila kodi. Bado hakuna taarifa zaidi kuhusu ujio wa simu hii kwenye nchi nyingine mbalimbali hivyo endelea Kutembelea Swahili Tech kujua zaidi kuhusu simu hii.