Jinsi ya kushare internet kwa kutumia Bluetooth

As salaam aleikum ndugu msomaji wa riyadi bhai Umeshawahi kutumia intaneti kwa mfumo wa Bluetooth kupitia simu yako ? Najua wengi tunaotumia simu kwenye mambo mengi tu ila wengi hatujui kama tunaweza kushare intaneti kwa kutumia Bluetooth.


Watu wengi tunatumia njia ya hotspot kuweza kushare intaneti kwenye vifaa vingine lakini sio lazima unaweza tumia Bluetooth kuweza kushare intaneti kwenye kifaa kingine kama vile simu , kompyuta pamoja na tablet.


Kwenye simu zetu Kuna kitu kinaitwa Bluetooth tethering, ni njia moja wapo ya kutumia mfumo wa wireless kuweza kusambaza upendo wa intaneti kwenye vifaa vingine kupitia Bluetooth.


Tusema huna bando Kuna mtu anahitaji kushare na wewe kidogo sio lazima uwashe hotspot unaweza tumia tu Bluetooth kuweza kushare intaneti na wengine.

Wala uhitaji password kuweza kuunganisha kwenye ivyo vifaa unafanyaje ku share intaneti kwa kutumia Bluetooth kupitia simu yako 

• ingia  setting kwenye simu yako 

• Kisha hotspot & tethering

• utagusa kwenye Bluetooth tethering

• hakikisha data Iko Kisha kwenye simu nyingine inahitajika kupata intaneti awashe tu Bluetooth  ikishakua connected anaweza tumia intaneti bila password.

Pia unaweza tumia njia hii kuunganisha na kompyuta yako kuweza kushare intaneti kwenye kompyuta kama upendi watu uwatajie password ya hotspot yako.


Umeshawahi kutumia hii njia au ndo unasikia Leo tuachie maoni yako ?

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa