Habari msomaji wa blog hii hapa leo nitakujuza kuhusu kupata pesa kupitia blog au website yako wengi hutumia mitandao bila mafanikio leo inabidi tujue kutumia kwa mafanikio yetu
kama unamiliki blog au website kuna kitu kinaitwa google adsense hii ni
program ambayo inatupatia pesa sisi wanablog wenda unaijua au ushawahi kuisikia mahali.
GOOGLE ADSENSE NI NINI ?
Ni mfumo wa Matangazo kwa njia ya mtandao unaihusisha matangazo kwenye kurasa za tovuti , programu , blogu , majukwaa na huduma zingine za mawasiliano haswa kwenye mtandao .
Google Adsense ina aina 2 za matangazo kuna yale ya maandishi pekee yaani Text na yanayotembelea kama picha na video yote ni mazuri na yote yana gharama zake .
GOOGLE ADSENSE NA MAISHA YAKO
Kwa kutumia Google Adsense unaweza kupata karibu laki 9 na zaidi kila mwezi na ukasahau kufanya shuguli zingine , Adsense inaweza kufunga Akaunti yako muda wowote au blogu yako muda wowote ule usipozingatia Masharti yao , kwahiyo usitegemee sana , Soma sheria za Adsense Hapa
GOOGLE ADSENSE INAFANYAJE KAZI
Kama unatovuti yako ukiweka matangazo ya mfumo wa adsense utalipwa kutokana na wingi wa watu wanaitembelea tovuti hiyo na jinsi watu watakavyo gonga click matangazo hayo.
Mfano mrahisi ni Bwana Riyad ana kampuni yake inaitwa Riyadi Bhai , badala ya kutengeneza matangazo makubwa kwenye magazeti pamoja na kufungua tovuti ataenda kuongea na google au wawakilishi wa google atatoa tangazo lake atasema jinsi anavyotaka liangaliwe kwa mfano idadi ya nchi au maeneo ndani ya nchi husika , Matangazo ya Riyadi Bhai yanaweza kuonekana kwenye blogu ya Zote kali inayoitwa www.zotekali.com na tovuti nyingi za watu mbalimbali zilizokuwa na huduma za Adsense .
Kwahiyo Riyad atafaidika kwa tovuti yake kutembelewa na watu wengi kutokana na kutangaza kupitia adsense na watu wanaotembelea Zote kali kuona kiunganishi cha tovuti yake.
NOTE > Kufuatilia masharti na maelezo mengine ni muhimu sana kwa mfano unatakiwa usiwaambie watu wagonge matangazo yako waache wa gonge click wenyewe ukifanya hivyo unaweza kufungiwa .
SWALI MUHIMU
Je ukubwa wa Tovuti au Blogu au umaarufu ndio kuongeza kipato cha Adsense ?
Jibu ni hapana utaweza kupata mapato zaidi kutokana na jinsi ulivyoweka matangazo yako na jinsi watu wanavyogonga matangazo hayo hapo ulipoweka kwenye kurasa za tovuti au blogu yako
USAJILI WA GOOGLE ADSENSE UKOJE
Wale wanaotumia huduma za Gmail ambayo ni mali ya Google ni rahisi kujisajili ili kutumia mfumo wa Adsense kwenye blogu na tovuti zao unaweza kutembelea www.google.com/adsense
NOTE>Kila mtu anahaki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kufuatilia malipo yake mwenyewe na kulipwa yeye.
KUKUBALIWA NA PIN NUMBER
Usajili wa Goolge Adsense hauwezi kukamilika kama huna PIN NUMBER na kujaza vitu vingine vya kuthibisha jinsi unavyolipa kodi , kama uko nchi za ulaya kuna namba unatakiwa kuandika ndio utapewa PIN NUMBER .
Kama ukiwa nje ya ulaya kama Tanzania , unaweza kutumiwa PIN NUMBER kutumia DHL ambapo utaingiza namba hiyo kukamilisha mfumo wa usajili au unaweza kuwatumia google kitambulisho au aina nyingine ya utambulisho kuthibitisha uwepo wapo kama kadi ya benki au passport.
NOTE> Bila pin Number hutoweza kutambulika kwenye mfumo wa google adsense na malipo yako hutopatiwa .
MALIPO YA GOOGLE ADSENSE
Google huwa inalipa wenye Adsense kwenye tovuti zao kila mwisho wa mwezi kwa mfumo wa cheki , benki au western Union kutegemea na nchi ambayo mtu yupo , malipo hulipwa pale kunapokuwa na kiasi cha pesa kuanzia dola 100 kwa mwezi ambapo dola 17 hutumika kama gharama za kusafirisha cheki kama uko nchi ambayo wanatuma cheki .
Kwahiyo unavyofanya kazi hii ya matangazo hakikisha unapata hela nyingi zaidi ili uweze kulipa gharama za benki na usafirishaji wa cheki yako , angalau uweze kuwa na dola za kimarekani 700 kila mwezi .
NOTE > Malipo ya kila mwezi hulipwa mwezi unaofuatia kama yalifikia zaidi ya dola 100 za kimarekani
MALIPO YANAVYOTUMWA
Kwa nchi ya Tanzania malipo ya Google Adsene huja kwa njia ya DHL ambapo hufika kila tarehe 2 kila mwezi , malipo yakifika kwenye ofisi za DHL wateja hupigiwa simu na kupelekewa au kama unaweza kufuatilia mwenyewe kutumia tracking number ya DHL kujua kama mzigo umefika au la .
Jambo la kujua ni kwamba watu wengi hufikiri cheki zinatumwa kwa njia za posta za kawaida hapana ni DHL .
UTARATIBU WA KIBENKI
Unatakiwa uwe na Akaunti kwenye benki yoyote Tanzania kwa sababu cheki za google huandikwa jina la mtu au kampuni kwahiyo lazima uwe na Akaunti kama uko Tanzania .
Ukishaweka cheki kwenye Akaunti yako huchukuwa siku 21 za kazi ili kuweza kulipwa malipo kwenye Akaunti yako na gharama zingine za kibenki .
Kutokana na gharama nyingine za kibenki ina maanisha ukiwa na shilingi laki 5 kwa mwezi ujiandae kutoa elfu 70 kama gharama za kushugulikia Cheki yako kwenye benki yako.
NOTE > Watu wengi hukata tamaa mapema na huishia njiani kwahiyo wanapoteza hela zao nyingi na watu wanatangaza kwenye tovuti au blogu hizo bure .
Kumbuka unavyofungua blogu ukaweka adsense matangazo yataendelea kuwa hapo na watu wataona wanavyotafuta vitu mbalimbali kwenye mtandao kwahiyo usikate tamaa mapema .
ZINGATIA NA UWE MAKINI NA MATAPELI
Hapo juu nimesema kila mtu ana haki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kulipwa kwa jina lake hela yake mwenyewe , kuna watu wa nchi za nje haswa Uganda wanapenda kuwalaghai watu wa Kenya na Tanzania kwamba washirikiane kuendesha Mfumo wa Adsense kwenye tovuti zao na kugawana Hela nusu kila mwisho wa mwezi .
Usikubali kuingia kwenye mtego huu , unatakiwa uwe na Akaunti yako unayoweza kuitolea maelezo na inayolipwa kwa jina lako kwenye nchi yako unaporuhusu hivyo faida haiendi nchini mwako inaenda Uganda kwa jina la Raia wa Uganda ambaye atatumia jina bandia ili asimwone akisha kutapeli hela zako .
Hata kama unapata hela kidogo mfano dola 1 kwa siku usikate tama utaweza kuongeza vitu kwenye tovuti yako haswa kwa lugha ya kiingereza na kifaransa na kuweza kupata hata dola 50 kwa siku moja jinsi unavyoendelea kukuwa .
CHANGAMOTO ZA MFUMO HUU
Baadhi ya maeneo Adsense haifanyi kazi kutokana na aina ya matangazo yaliyofungiwa kutokana na mila na desturi za maeneo hayo .
Mfumo wa Adsense uko zaidi kwa lugha ya kiingereza na nyingine za kimataifa bado haijasambaa sana kwenye lugha zingine ndogo ndogo kama Kiswahili ingawa mtu anaweza kutangaza pia
Benki nyingi haswa za afrika hazitambui mfumo wa google adsense kwahiyo baadhi ya watu wanapata tabu pale wanapoenda kuingiza cheki zao kwenye Akaunti na kudhani ni utapeli badala yake nyingi hutumwa kupitia CITIBANK ambayo huduma zake ziko juu sana .
Nchi nyingi hazina mfumo wa kulipa kodi kwa njia ya mtandao kwahiyo unakuta wanachama wote wa google adsense wanalipa kodi kwenye nchi ya marekani kwa kwa kila malipo ya adsense nchi nyingi zinapoteza malipo hayo kutokana na mifumo yao .
Kwa sasa nchi ya Kenya na Uganda wamefanya mazungumzo na google kwahiyo ukiwa nchi hizo malipo yako unapata baada ya siku 3 kila mwezi kwa njia ya western union au kuingiziwa fedha kwenye Akaunti yako moja kwa moja .
Nakaribisha maoni yako hapo chini kuhusu makala hii usisahau Kushare
4 Comments
habari,nina blog yangu ina miezi 2 na inatakribani vewers 44,000 lakin bado natumia domain name ya bure kutoka google(blogspot.com),je google adsense wanakubali matumiz ya domain hii ya bure? na je nikanunua new domain sasa hiv na kuhost blog yangu itaonekana mpya na kushindwa kukidhi kigezo cha muda wa miez 6?
ReplyDeleteMimi ni mzima kaka, naam adsense wanakubali hata kama ukiwa unatumia blogspot, kama utatumia wordpress itaonekana mpya lakini sio lazima ifikishe miezi sita, ili google wakukubalie katika blog yako yenye domain yako na host, ni lazima utimize masharti yao ambayo ni lazima utumie lugha wanayoikubali kama kiingereza n.k, pia ni lazima uandike usikopi na kupaste ukitimiza masharti yao hawana hiyana lazima wakukubalie. Bila shaka nimejitahidi kukujibu kwa kadri nilivyokuelewa ndugu yangu
DeleteNimepata adsense ila nimetumiwa pin kwenye box address yangu na hii ni mara ya tatu ila sijaipata.Je natakiwa niende ofisi za dhl au nisubir kwenye sanduku langu au nitakuwa nakosea kujaza address? Maana kuna line 1 na line 2 address pia kuna Zip code
ReplyDeleteInawezekana ukawa umekosea jinsi ya kujaza
DeleteJe unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa