MAKOSA 4 YAFANYWAYO NA BLOGGERS WENGI BILA KUJUA

Idadi ya watu Tanzania waofanya blogging inazidi kuongezeka siku hadi siku.Bila ya kujua bloggers wengi wa Tanzania wanajikuta wakifanya makosa ambayo yanaweza kusababisha ukakosa WATEMBELEAJI KATIKA TOVUTI YAKO!.Makosa hayo yanairudia na watu kutojali kwamba kosa moja katika blog yako linakupotezea idadi kubwa ya watembeleaji.Tuanze kujadili moja baada ya jingine;

1.KUWA NA MADA NYINGI ZISIZOKUWA NA UHUSIANO NA ZILIZO FUPI
Ni kweli kabisa ili kuweza kuwa katika kurasa za juu za search engines inakubidi uwe na maudhui ya kutosha na ambayo yanawekwa kila wakati.Hautoweza kuwa na watembeleaji wa kutosha kama unaandika maudhui kila baada ya muda mrefu.Andika maudhui yako angalau mara/mbili kwa wiki endapo site yako sio news website.Tatizo ambalo linawakumba blogger wa tanzania ni kwamba wanajali idadi ya mada(posts) bila kujali ubora wake.Hapa ndio unapokuta mtu ana posts 2000+ lakini mwenye posts chini ya 100 anamzidi page rank na visitors.Ubora tunaongalia hapa ni kwamba mada zako angalau ziwe na maneno angalau 600+(unique content).Kuwe na meta data za msingi katika kila page/post.Kwa hiyo kuwa na posts nyingi hakuna maana yoyote kama hazina ubora.


Uhusiano tunaozungumzia hapa ni kwamba unapoandika mada uwe na hadhira fulani(audience).Andika mada zitakazohusu mada fulani au mada zinazo fanana na hizo.Utapoandika mada ambazo hazihusiani itakuwa ni vigumu tovuti yako kuwa ranked katika keywords fulani.Suala hili ndilo linalosababisha mtu mwenye post nyingi zisizo kuwa na uhusiano kuwa na visitors wachache kulinganisha na mtu mwenye post chache ila zenye uhusiano.


Mada fupi ni sumu kabisa katika tovuti yako,maana unaweza kuandika mada fupi ikakosa keywords muhimu ambazo zingeweza kukuongezea visitors.Andika mada zenye urefu wa kutosha zinazoelezea mada yote kwa kila kitu (mada iwe inajitosheleza).Hakikisha mtu anaposoma mada yako hapati shida kuangalia tovuti nyingine kwa ajili ya kuongeza ujuzi.

2.KUWA NA MADA CHACHE NA FUPI
Bloggers wengi wa Tanzanzia ambao ndio wanaoanza inawawia vigumu kuandiaka mada ambazo ni ndefu na ambazo zinakizi mahitaji ya watu.Kuwa na mada chache na fupi kutasababisha tovuti yako kutokuwa na search keywords ambazo zitaitambulisha katika search engines.Hivyo tovuti yako kwa ujumla itashindwa kujulikana inahusu nini katika mada zake.Vile vile utakapokuwa na mada fupi utasababisha mtu kutopata anachokihitaji katika tovuti yako na kupelekea kukosa watembeleaji.Utakosa returning visitors maana mtu anakuwa anajua kuwa tovuti yako huwa inaandika mada fupi zisizojitosheleza.Utakapokuwa unaandika mada fupi sahau kabisa kuwa katika top pages za search engines.Endapo umeandika mada hizi fupi basi ni wakati sasa wa kuziandika upya(update content).Utakapo kuwa unaziandika upya utapata matokea mazuri ambayo nawe pia utayaona.

3.MUSIC VIDEOS WEBSITES ZISIZO KUWA NA MADA(POSTS)Kuweza kupata watembeleaji wa kutosha katika tovuti inayohusu videos tupu bila content (posts) ni ndoto.Kwa nini nasema hivyo? .Search engines zinauwezo wa ku-index maneno na sio picha wala videos.Endapo utaamua kuunda media website hakikisha ;

(i) Kila video iwe ina maelezo (descriptions) ya kutosha
(ii) Ongeza mada (posts) katika tovuti yako
(iii) Tenga sehemu ya posts na videos usichanganye kwa pamoja
(iv)Tumia youtube ku-link videos zako
(v) Uwe na youtube channel

4.CHAGUA LUGHA YA KUANDIKA POST
Unapoamua kuanzisha tovuti angalia lugha moja muhimu itakayo kuwezesha kuandika mada zako kwa hadhira yako.Utakapo andika mada moja kwa lugha hii na mada nyingine kwa mada nyingie itakuwa ni vigumu kwa mtemeleaji kama haijui hiyo lugha nyingine.Vile vile search engine zitashindwa kujua ni lugha ipi unatumia kwa ujumla na kuonyesha kwa walengwa husika.


Endapo umelenga watembeleaji wa nchi za nje na umetumia labda kiswahili na kiingereza wanapokuta kiswahili na hawakielewi inamaana utapunguza watembeleaji.Utapoandika post zako kwa kiswahili itakusaidia kuwa katika pages za juu kwa urahisi kwa sababu idadi ya wanaotumia lugha hii siyo kubwa sana ukilinganisha na lugha kama kiingereza.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa