NJIA 5 ZA KUBORESHA BLOG/TOVUTI YAKO KUFIKIA WATUMIAJI WAKO KWA URAHISI

As salaam aleikum ndugu yangu Unapoanzisha tovuti, unataka kupata trafiki kubwa kadri iwezekanavyo. Unataka watumiaji (target audience) wako waweze kutembelea tovuti yako ili waweze kuwa wateja wako au watembeleaji wa kudumu baada ya kuona chapisho lako kwa mara ya kwanza na maudhui kwenye tovuti. Kwa hiyo, ni mambo gani ambayo mtu anaweza kufanya ili aweze kupata Trafiki ya uhakika ?

Naam, kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya ili kuhakikisha unapata watu uliowalenga (target traffic) kwenye tovuti yako. Hapa chini kuna mbinu 5 za kusaidia tovuti yako kufikia walengwa (target audience):

1. Weka lengo, na uwajue walengwa wako
Mtu hauwezi kuanzisha tu tovuti/blog bila ya kuwa na wazo kuhusu kitu utakacho wapatia watembeleaji wa tovuti. Lazima uwe na lengo la tovuti yako. Unataka kufikia nini na tovuti? Walengwa ni kina nani, watu ambao unataka kuwasiliana nao kupitia tovuti yako? Unapoweza kujibu maswali haya, ni wakati wa kuanzisha tovuti ambayo inalenga watazamaji wako.

Ukiweza kufafanua malengo yako, unaweza kuanzisha tovuti yenye maudhui yaliyo sahihi na maneno muhimu (keywords) ambayo yatatumika kama njia ya kuleta trafiki husika kwenye tovuti na google watakupa kipao mbele ukiwa hautachanganya mambo tovuti yako ni vema ikawa na maudhui maalum mfano ikiwa inazungumzia Tech basi usianze kuweka na muziki na udaku na mifano yake shika moja ili upate watembeleaji wa uhakika.


2. Maudhui yanayoendana na wasomaji

Njia rahisi ya kupata trafiki kwenye tovuti yako ni kupitia maudhui unayoweka kwenye tovuti. Je! Maudhui yako yanafaa? Kwa mfano, kama tovuti yako yote inahusu  muziki, basi kama una picha au taarifa muhimu ambazo zinahusiana na muziki ndio inakubidi uchapishe vitu vya namna hiyo, Ikiwa sio, huwezi kupata aina sahihi ya trafiki kwenye tovuti yako na kama hivyo, huwezi kufikia malengo yako.
Ikiwa unataka mafanikio zaidi, unapaswa pia kuwa na faili za video na sauti kwenye tovuti ili wasomaji wako waweze kuburudika na kupata taarifa zaidi. Hii itawawezesha wasomaji kuja kwenye tovuti yako mara kwa mara na kwa wingi.

3. Hakikisha tovuti yako inavutia


Ni muhimu kufanya tovuti yako iwe inavutia kupitia maudhui safi na maudhui yaliyopangwa vizuri. Je, tovuti imewekwaje upande wa maudhui? Tovuti ina kurasa ngapi? Ni aina gani za viungo vya nje (outside links)  vipo kwenye tovuti? Je! unaweka vitu kwenye tovuti mara kwa mara? Je, tovuti yako ina maingiliano? Vitu vyote hapo tulivyovieleza ni njia nzuri unazoweza kutumia kufanya tovuti yako iwe inavutia wasomaji wako. Wasomaji wako daima hupenda maudhui mapya mara kwa mara. Kumbuka kwamba injini za utafutaji pia zinapenda aina hii ya maudhui na hii ni njia nzuri ya kupata targeted audience kwenye tovuti.

4. Hakikisha tovuti inafunguka haraka


Hiki ni kipengele muhimu sana kwenye tovuti ambacho watu wengi hawakizingatii. Tovuti inapofunguka haraka, ni rahisi kupata trafiki zaidi. Kumbuka kwamba watu wachache sana ulimwenguni pote wana uwezo wa kufikia mtandao wenye kasi kubwa. Kwa hivyo, kasi ya kufunguka kwa tovuti, ni muhumu kwa wasomaji wako. Google pia inaziweka juu tovuti zinazofunguka kwa haraka zaidi kuliko zile ambazo hufunguka polepole.

5. Tumia Google Translate kwenye tovuti


Huenda usiwe na uwezo wa kuunda tovuti kwa kila lugha au nchi unayoilenga. Unaweza kutumia Google Translate kwenye tovuti yako ili wasomaji uliowalenga waweze kupata urahisi wa kupata ujumbe na habari kutoka kwenye tovuti yako. Hii ni nzuri zaidi kwa ajili ya startups na makampuni madogo ambayo yanataka kulenga wasomaji kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Bila shaka umepata mwanga kuhusu kuendeleza blog yako tuachie maoni yako usisahau kushare makala hii katika mitandao ya kijamii

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa