Jinsi ya Kutumia IDM (Internet Download Manager) Kudownload Torrent files kwa kasi kubwa

As salaam aleikum wapendwa baada ya kupotea kutokana na maswala ya kujitafutia mkate wa siku leo nimerudi tena kwaajili yako karibu sana katika blog inayojaribu kukutatulia mambo yako ya kiteknolojia kwa mapana zaidi leo tugusie suala zima la kuwepesisha kupakua file za torent kwa speed kubwa zaidi kwa kutumia IDM yaani Internet Download Manager 

Watu wengi wamekuwa wakitumia torrent clients ( kama u-torrent, bittorrent, vuze etc) kwa ajili ya kupakua movies na apps zenye file kubwa kutoka kwenye torrents sites mbalimbali lakini huwa kunakua na changamoto ya speed kuwa ndogo unapokua unapakua file hasa lenye seeders wachache ....ili kuepukana na changamoto hyo leo ntakujuza njia ya kupakua files kwa kasi zaidi;

1. kwanza kabisa  unatakiwa uwe na internet download manager (IDM) kama hauna download hapa bure kabisa DOWNLOAD

2. Link internet download manager na browser unayotumia mimi huwa natumia chrome unaweza kupakua chrome browser hapa DOWNLOAD

3.Unatakiwa ufungue account kwenye website inayoitwa www.seedr.cc ambako utapewa disk kama 2gb ( ila inaweza kufikia 5GB ukifanya sharing na rafiki zako kupitia referral code yako) 



4.Ukishafungua hiyo account utakwenda kwenye torrent site unayopendelea either rarbg.to , katcr.co , limetorrent.cc 13377x.to etc



5 . Copy magnet link ya file kama unavyoona katika picha hapo juu unalotaka kudownload na paste kwenye seedr.cc 


account kuna sehemu imeandikwa paste, kisha bofya kitufe cha jumlisha 

na file lako litaundwa na utaona mshale wa kupakua ukiweka mouse yako katika folder lililoundwa angalia picha hapa chini
na utaweza download kwa kasi nzuri sana ambayo ni tofauti kabisa kama ungetumia utorent

asante kwa kusoma makala hii sambaza upendo kwa washkaji kwa kushare makala hii karibu tena

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa