WATUMIAJI WA WHATSAPP WAWEZA KUDUKULIWA

Programu ya WhatsApp ndio yenye watumiaji wengi zaidi duniani na kuwa moja ya kitu muhimu katika mawasiliano ya kila siku hata hivyo kwa mara kadhaa wadukuzi wamekuwa wakidhirisha kuwa inaweza kuchezewa.

Kuna mengi yaliyawahi kubainishwa kuhusu usalama wa kutumia WhatsApp na suala zima la udukuzi. Watafiti kutoka Check Point Software Technologies wameweka wazi kuwa WhatsApp bado inaweza kuchezewa, utajiuliza kivipi?

Wadukukuzi wanaweza kutengeneza toleo la WhatsApp ambalo ni la uwongo kisha kubadilisha majibu ambayo yanatokana na ujumbe ulionukuliwa kwenye mazungumzo kupitia WhatsApp.
Ripoti hiyo inakwenda mbali zaidi na kusema kwamba wadukuzi hao wanaweza wakabadili kile kinachojibiwa au kubadili mtu ambae ameutuma ujumbe husika.

Mfano wa ujumbe ulionukuliwa kwenye WhatsApp.
Wanaoimiliki wanafanya/wamefanya nini kuhakikisha usalama dhidi ya wadukuzi?
Kitu kizuri ni kwamba wahusika wanafahamu kitu cha namna hiyo kinaweza kutokea na wamekuwa wakiwaondoa watu ambao wanatumia toleo la WhatsApp lililodukuliwa na uwezekano wa kubadilisha ujumbe ulionukuliwa sio udhaifu kwani mfumo wa end-to-end encryption ni kitu ambacho kinaaminiwa sana kwa maana ya kwamba hakiingiliki.

India ndio yenye watumiaji wengi duniani wa WhatsApp ikielezwa kufikia zaidi ya watu mil. 200 na kampuni za simu zimeelezwa kutafuta mbinu ya kufunga programu tumishi za kutuma/kupokea ujumbe iwapo zikitumika vibaya.

Mpaka sasa hakuna taarifa ya ujumbe ambao umenukuliwa lakini majibu yake yanatatanisha (kudukuliwa) ila ni vyema kuchukua tahadhari na kuweza kutambua udukuzi iwapo ukitokea.

Chanzo: CNet

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa