Naaam, usishangae umesoma sawa sawa tuu hapo juu, moja ya vipengele ambavyo iOS 16 ilitarajiwa kuja navyo ni uwezo wa mtu kuona asilimia ya chaji isliyosalia katika betri!
Mambo yamebadilika bwana, tulitegemea kila iPhone ambayo itakua na uwezo wa kutumia iOS hii basi itakua na uwezo wa kuonesha asilimia hiyo ya chaji katika betri, lakini jambo zima halipo hivyo.
Iphone Ambazo Hazitakua Na Uwezo Huo Ni:
iPhone XR
iPhone 11
iPhone 12 Mini
iPhone 13 Mini
Najua hapa utakua na maswali juu ya matoleo ya chini ya hapo na utakua unajiuliza vipi kuhusu iPhone 8 maana tangazo linasema kuanzia 8 kwenda juu wote watapata iOS 16.
Hapa cha kufahamu ni kwamba kipengele hicho hakitakua kwa simu zote kama tulivyotemea hapo mwanzo.
Kwa simu zote tajwa hapo juu kama kupitia iOS 16 hazitakua na uwezo huo basi hakuna budi itabidi watumiaji waingie katika eneo la ‘Control center’ kama wakitaka kuona silimia salia za chaji.
Ikumbukwe hapo awali simu zote za iPhone zilikua zikionyesha sehemu ya eneo la chaja katika simu zote pembeni ya betri.
Baada ya kutoka iPhone X na kuendelea mambo yakaanza kubadilika taratibu na sababu kuu ikiwa Apple walijibakizia uwanja mdogo sana sababu ya ‘Notch’ katika iPhone.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa