Articles by "Internet"
Showing posts with label Internet. Show all posts
As salaam aleikum, Hivi leo kuna mambo mengi kuhusu intaneti, lakini hapa nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuvutia na kukushangaza. Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambamba na maendeleo ya kompyuta.

Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi.

Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua.

1. Tovuti ya kwanza bado ipo
Tovuti ya kwanza kutengenezwa bado ipo na inafanya kazi hadi leo. Jambo pekee ni kuwa tovuti hiyo inaonekana vile vile kama ilivyokuwa zamani. Unaweza kutembelea hapa ili kuiona.
2. Takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kwa siku
Kampuni ya Radicati inakadiria kuwa takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kila siku. Inaelezwa kuwa asilimia 90 ya barua pepe hizo ni barua pepe hatarishi (SPAM) na Virusi, hivyo kuwa makini na barua pepe unazofungua.
3. Tweet ya kwanza ilichapishwa Machi 21, 2006 na Jack Dorsey
Nani alifahamu kuwa Twitter ingekuwa maarufu duniani kama ilivyo leo? Mnamo Machi 21, 2006 Jack Dorsey aliandika tweet ya kwanza iliyokuwa inasema, “Just setting up my twttr.” lakini hivi leo Twitter imeshakuwa na mamilioni ya watumiaji ulimwenguni kote.

4. Video iliyotazamwa kuliko zote kwenye mtandao ni Despacito
Wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi na Daddy Yankee ni wimbo unaoongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Wimbo huu umeshatazamwa mara bilioni 3.55 hadi sasa.

5. Mgunduzi wa intaneti Tim Berners-Lee alipewa cheo cha Knight na malikia Elizabeth
Kutokana na ugunduzi mkubwa alioufanya Tim Berners-Lee, malikia Elizabeth wa Uingereza alimpa cheo cha Knight kwenye serikali yake mwaka 2003.
6. Saa 300 za video hupakiwa kila dakika kwenye YouTube
YouTube ni mtandao maarufu ambao wengi wanaufahamu kama mtandao wa kusambaza na kutazama video kwenye mtandao. Lakini je unajua kuwa kwa muda wa dakika moja video zenye jumla ya urefu wa saa 300 hupakiwa katika mtandao huu? Tovuti hii hupokea video kutoka kwa watumiaji mbalimbali duniani kote.
7. Neno kuperuzi mtandao (Surfing the internet) liliundwa mwaka 1992
Kabla ya mwaka 1992 neno (surfing the internet) halikuwa linafahamika hadi pale Jean Polly alipoandika makala iliyosomwa sana na kupakuliwa na watu wengi na kusababisha kusambaa kwa neno hili.

8. Mitandao ya kutafuta wapenzi inazalisha takriban dola bilioni 2.2 kila mwaka
Teknolojia imebadili mfumo wa maisha. Watu hutafuta wapenzi au wenzi wa maisha kwenye mtandao. Hili limepelekea tovuti za kutafuta wapenzi kuzalisha zaidi ya bilioni 2.2 kwa mwaka 2014 pekee.

9. Asilimia 10 ya wahalifu wa kijinsia wanatumia mitandao ya kutafuta wapenzi
Kutokana na umbali au kutokufahamiana vyema, wahalifu wengi wa kijinsia hutumia mitandao ya kutafuta wapenzi kufanya uhalifu wao.

10. Takriban Watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kupitia Match.com
Mtandao wa match.com unadai kuwa takriban watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kwenye tovuti hiyo ya kutafuta wapenzi.

11. China ina kambi za kutibu waathirika wa kutawaliwa na mtandao (internet addict)
Wakati china ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao zaidi ya milioni 721, inaaminika kati yao milioni 23 ni waathirika wa kutawaliwa na mtandao. Hivyo wameanzisha kambi mbalimbali za kuwasaidia watu hawa.

12. Watumiaji wengi wa intaneti ni roboti na programu haribifu (malware)
Wakati mwingine unaweza kufikiri watumiaji wa mtandao ni watu pekee. Lakini asilimia kubwa ni roboti na programu haribifu zilizobuniwa na watu mbalimbali ili kutimiza shughuli fulani.
13. Tweets milioni 500 zinatumwa kila siku
Kutokana na Twitter kuwa na watumiaji milioni kadhaa, inaaminika kuwa zaidi ya tweets milioni 500 hutumwa kila siku.

14. Huwa unatumia kisehemu kidogo tu cha mtandao
Ni wazi kuwa sehemu unayoitumia kwenye intaneti ni sehemu ndogo sana ambayo inaonekana kwenye injili pekuzi (search engines). Ipo sehemu nyingine ambayo imefichwa kwenye injini pekuzi (dark web); sehemu hii inajumuisha taarifa binafsi za watu, taasisi na makampuni mbalimbali. Unaweza kuperuzi sehemu iliyofichwa ya intaneti kwa kutumia kivinjari (browser) ya Tor.

Soma pia: Sehemu ya Mtandao wa Intaneti Iliyofichwa (Deep web na Dark web).

15. Tovuti 30,000 zinadukuliwa kila siku
Kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa kwenye mtandao, inakadiriwa kuwa zaidi ya tovuti 30,000 hudukuliwa na wadukuzi kila siku.
16. IMDb ilikuwepo tangu miaka ya 1990
Tovuti maarufu ya kutafuta video, filamu, vipindi vya televisheni pamoja na michezo ya video ilianzishwa mnamo Oktoba 21, 1990, na Col Needham. Baada ya miaka minne ilipata jina lake la IMDb ambalo imedumu nalo hadi leo.

17. Tovuti milioni 7 zilifungwa mwaka 2009
Huduma ya GeoCities ya Yahoo iliyokuwa inawaruhusu watu kutengeneza tovuti zao binafsi ilifungwa mwaka 2009 na kupelekea kufutwa kwa zaidi ya tovuti milioni 7. Tovuti hizi zilifutwa kutokana na kuwepo kwa tovuti nyingi zilizokuwa na ubora duni.

18. Watu takriban asilimia 100 wa Iceland  wanatumia intaneti
Nchi nzima ipo kwenye mtandao? Ndiyo, nchi ya Iceland ina wakazi wapatao 331,778 ambao takriban wote wanatumia mtandao wa intaneti. Je nchi yako ni ya ngapi? Unaweza kutazama hapa.

As salaam aleikum ndugu msomajiwa blog hii, Hakika ulimwengu huu una mambo mengi ambayo hatuyafahamu bado, kila siku tunaweza kujifunza jambo jipya hadi mwisho wa maisha yetu.

Intaneti ni kitu ambacho kwa ulimwengu huu wa sasa kila mtu anakitumia kwa njia moja au nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na kutumika huku kwa intaneti bado kuna mambo mengi ya kushangaza tusiyoyajua.

Je wajua kuwa ipo sehemu ya mtandao wa intaneti iliyofichwa? Sehemu hii inajulikana kama Deep web na Dark web.
Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe juu ya sehemu hii ya mtandao wa intaneti iliyofichwa (Deep web na Dark web)

Deep web ni nini?
Deep web ni sehemu ya intaneti ambayo haionekani kwenye injini pekuzi kama vile Google na Bing — moja kwa moja injini pekuzi haziwezi kuona sehemu hii kwa sababu imefichwa isionekane.

Deep web siyo kitu kilicho nje ya huu ulimwengu bali ni kitu ambacho umekuwa ukikitumia mara kwa mara — barua pepe yako, benki mtandao, meseji zako za Twitter, LinkedIn n.k Taarifa hizi haziwezi kuonekana kwenye injini pekuzi kwa kuwa zinalindwa kwa nywila (password) au kulipiwa ili kuziona.

“Vitu vyote visivyoweza kupatikana kwenye uso wa juu wa mtandao kwa kutumia injini pekuzi ni sehemu ya Deep web”
Ikizingatiwa kuwa tuna mabilioni ya watumiaji wa mtando wa intaneti duniani, hivyo inaelezwa kuwa kuna mamilioni ya taarifa au data zilizoko kwenye Deep web.

Hata hivyo inaaminika kuwa Deep web inaunda sehemu kubwa ya mtandao; Deep web inaweza kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida kama vile Chrome na Firefox n.k.

Dark web ni nini?

Dark web siyo sehemu tofauti na intaneti bali ni sehemu ya Deep web ambayo haiwezi kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida.

Kwa nini Dark web haiwezi kuonwa kwa kivinjari cha kawaida? Ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web ni haramu, si rahisi wahusika wake kuruhusu mambo haya kuonekana kwenye vivinjari vya kawaida.

Je kwenye Dark web kuna shughuli gani?


 • Uuzaji wa madawa ya kulevya
 • Uhalifu wa kila namna (uuzaji wa viungo vya binadamu, ajira za kutisha, ugaidi n.k)
 • Wadukuzi hatari wa kompyuta
 • Uuzaji wa taarifa na vitu vilivyoibiwa
 • Picha za unyanyasaji wa kingono hasa watoto
 • Uuzaji wa silaha
 • Mawasiliano ya wanaharakati na waandishi wa habari wanaotaka kuibua maswala mbalimbali. Hutumia njia hii kujificha wasije wakakamatwa na serikali au mahasimu wao. Mtandao wa wikileaks unapokea pia taarifa kupitia Dark web.


Je tovuti za Dark web zinaperuziwaje?

Tovuti za Dark web zinaishia na anwani mtandao (domain) zenye .onion, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia kivinjari cha Tor pekee.

Tor ni kivinjari (browser) cha namna gani?

Tor ni kivinjari kilichotengenezwa na watu wakujitolea (voluntiers) kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambacho hufanya kazi kwa usiri wa hali ya juu wa kuficha mawasiliano pamoja na watumiaji wake.

Hivyo mtu anayetembelea tovuti fulani au kufanya chochote kwenye mtandao kwa kutumia kivinjari hiki siyo rahisi kubainika.

Kwa mfano unaweza ukawa unaperuzi mtandao kwa kutumia Tor ukiwa Tanzania lakini ukaonekana mara uko Japan, mara Uingereza au hata Marekani.

Ikumbukwe kuwa kutembelea Dark web siyo kinyume cha sheria lakini kufanya vitu huko kunaweza kuwa kinyume cha sheria kutokana na tovuti nyingi kufanya vitu vinavyokiuka sheria.

Kwenye Dark web siyo mahali panapovutia kama sehemu ya kawaida ya mtandao wa intaneti tulio uzoea. Tovuti nyingi huku zimetengenezwa kwa makusudi maalumu au pengine ya siri, hivyo hazikujali wala kukulinda.

Ili kuperuzi kwenye Dark web ni lazima uwe na kiungo (link) cha tovuti unayotaka kutembelea kinachoishia na .onion kwa mfano http://zqktlwi4fecvo6ri.onion. Hii ndiyo Dark web, hakuna kugoogle hapa, mambo yanaenda kwa namna ya ajabu ajabu tu.

Je Dark web ni mbaya?

Hapa kuna majibu mawili ndiyo na hapana. Pamoja na kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web sio halali, bado kuna toleo lake la Facebook na ProPublica kwa anauani ya .onion.

Lakini ukumbuke kuwa wachambuzi wa mambo wanasema tovuti hizi zinaweza zisiwe za kweli, kwani si rahisi Fecebook kukubali watumiaji wake kutumia anwani za kujificha za .onion. Hivyo kuwa makini na taarifa zako za siri huku.

Uzuri wa Dark web ni kuwa inawawezesha waandishi wa habari, wanaharakati na wale wanaoibua taarifa za siri kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila wao kujulikana.

Ni wazi kuwa hakuna kitu kibaya kwenye mtandao bali ni matumizi pekee ndiyo hukifanya kiwe kibaya.

Neno la mwisho

Naamini umejifunza mengi ambayo hukuwa unayafahamu kuhusu sehemu ya intaneti iliyofichwa. Lakini pamoja na hayo uliyojifunza ningependa kukushauri kuwa makini sana kama utaamua kutumia Dark web. Kumbuka pia kuzingatia sheria kwani uhalifu, maovu na ukatili wa kutisha umejaa kwenye Dark web.

Kwa mfano picha za video za watu wakichinjwa, ubakaji wa watoto, wizi, chuki na ubaguzi husambazwa bila woga wowote. Wadukuzi hatari pia wamejaa kwenye Dark web, hivyo epuka kutoa taarifa zako, kupakua kitu chochote au kufanya muamala wowote.

Credit : JF
As salaam aleikum Mswahili mwenzangu kama kawaida yetu leo Jifunze hatua saba rahisi kabisa za kuongeza speed ya internet maradufu kwenye kompyuta yako. Mara tu baada ya kumaliza utaona mabadiliko makubwa kwani speed ya Interneet itakuwa kubwa zaidi na kukuwezesha kufanya kazi kwa raha zaidi.


 • Hatua ya kwanza bonyeza  kitufe cha start alafu utaandika kama inavyoonekana hivi  gpedit.msc
 • sasa bonyeza marambili sehemu iliyo andikwa  Computer configuration


 • Bonyeza tena mara mbili Administrative Templet
 • Bonyeza Tena mara mbili Network   
 • Bonyeza tena marambili QoS Packet Schedule
 • Bonyeza mara mbili tena Limit reservable bandwith
 • kwanye Namba 1 chagua Enable na kwenye Namba 2 weka namba 0 malizia na kwanye namba tatu kwa kuchagua Apply alafu OK

Hadi hapo utakuwa umemaliza unaweza anza furahia Internet yenye kasi ya ajabu. Karibu sana SwahiliTech kwa habari na msaada wa kitaalamu.
Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini?
G kwenye tarakimu hizi inawakilisha ‘Generation’, yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.

Teknolojia Ya 1G, Ungeweza Tu Kupiga Simu

Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.
Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa

Kisha 2G Ikaja na Uwezo wa Kutuma Ujumbe Mfupi Au Arafa

Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.
Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi.
Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service).
Na pia simu za wakati huo zilikuwa na teknolojia ya GSM, GPRS, EDGE kama hii iliyopo hapa chini.

Teknolojia ya 3G Ikaja Na Uwezo Wa Kupiga Simu Kwa Video Kuanzia Mwaka 2001

3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya Smartphone zilianza kuuzwa madukani.
Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya Na Watu waliweza Kupiga Simu za Video. Angalau ilikuwa hatua fulani.

Teknolojia ya 4G Ilianza Kutumika Mwaka 2010.

Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.
Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.  Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.
Tanzania, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.

Je 5G Ndiyo Mwendo Kasi?

Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.
Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.
Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?

Hii kitu safi sana zaidi ni kwa wale Team Popoz, naziset video zote ninazotaka kushusha(Kudownload) then naenda zangu kulala!

Personally natumia JDownloader JDownloader.org - Offizielle Homepage

Ila zipo njia nyingi tu uazoweza kutumia kushusha video kutoka Youtube
=================

(Updated):
 Video za Youtube Bure

Furahia kutazama video za Youtube bila kikomo – usiku kucha, kila usiku – bila malipo yoyote kutoka Tigo. Tazama video zako za muziki uzipendazo, trailer za muvi, sehemu za video na kila kitu kingine ambacho Youtube kitakupa usiku mzima.

Maelezo kuhusu Ofa

 • Ofa inaanza kuanzia saa 6 usiku mpaka saa 12 asubuhi
 • Ofa ni kwa ajili ya wateja wa Tigo Peke yake
 • Hakuna malipo
 • Hakuna malipo kutoka salio lako
 • Hauhitaji kujiunga
Nahitaji kufanyaje ili kufurahia ofa hii?

Unahitaji kuwa mteja wa Tigo mwenye huduma ya internet na simu inayoruhusu kutumia internet

Kwa watu wasiokuwa wateja wa Tigo wanahitaji kununua laini ya Tigo

Naweza kufurahia ofa hii mchana?

Ofa hii ni kuanzia saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi, ukitumia huduma hii muda mwingine wowote utakatwa malipo ya kawaida ya huduma ya internet.

Furuahia kuangalia video bila internet

Zaidi ya kuangalia video usiku, Youtube inakupa uwezo wa kuhifadhi video zako uzipendazo ukiwa huna internet na kuzicheza baadae kipindi cha ambacho huna internet au ikiwa na spidi ndogo kwa kipindi cha masaa 48. Bofya sehemu ya kuangalia video bila internet kuhifadhi video hizo.

Imetoka: Tovuti ya Tigo