MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUNUNUA SMARTPHONE (Simujanja)

As salaam aleikum mpendwa msomaji wa ukumbi huu, hakika kila mmoja wetu anapenda kumiliki simu kali tena simu janja ya kisasa, lakini wenda tunakosea wakati wa kufanya manunuzi, kwani sio kila simu inafaa kununua kuna nyingine ni matatizo hapa chini nimejaribu kukuelezea mambo ya kuzingatia wakati wa kununua simu


Epuka kuwa na haraka/pupa/ kukimbilia

Unapaswa kuepuka kuwa na haraka/pupa/kukimbilia kununua kitu ambacho utaweza kujuta baadae. Unahitaji kuchukua muda kufanya uchunguzi juu ya simu unayoitaka kabla ya kwenda kuinunua, sote tunajua haraka haraka haina baraka ukiwa na haraka itapelekea ukauziwa simu ya bei rahisi kwa pesa nyingi kutokana na kukosa umakini katika manunuzi yako.

Epuka ushindani

hasa kwa dada zangu, Hatupaswi kuwa na mashindano yoyote wakati wa kununua simu nzuri. Aina ya simu za mkononi ambazo wengine wanatumia hazipaswi kukuongoza kununua yako. Huna haja ya kushindana, sio lazima. Nunua kulingana na pesa zako zinazoweza kumudu, kwani unaweza kujikuta unashindwa kufanya mambo ya msingi kutokana na kufikiria kuwa na simu kama ya jirani yako wakati uwezo njaa zimekata break.

Epuka kununua smart phone iliyotumika

mwaka jana nikiwa kituo cha polisi rumande nilisikia mashtaka mengi kuhusu simu, kila aliyelalamika alijitetea kwa kusema kuwa alinunua kwa mtu yeye hausiki, Watu wengi hutumia au hununua simu ya mkononi iliyotumiwa na hatimaye kupata matatizo mengi baadaye. Ili kuepuka hili, unahitaji kununua simu (smart phone) ambayo ni mpya na inayoweza kudumu/kuishi kwa muda mrefu. Hasa kwenye uwezo wa betri.

Epuka kununua smart phone mitaani

Hili jambo siku hizi limezoeleka sana. Watu wengi wananunua smart phones mitaa kwa kigezo cha bei rahisi kisa simu anayoinunua imetumika kwa muda fulani. Wengi wa wanaouza smart phones mitaani ni walaghai na wanaweza kukupa simu mbovu na mbaya. Ni dhahiri kabisa wengi tushawahi kuuziwa simu mbovu mitaani. Ni vyema kujishauri na kufanya maamuzi sahihi kabla ya kununua simu huko mtaani ili kuepuka hayo matatizo hasa kutapeliwa.

Neno la Muandishi: sio simu zote zinazouzwa mitaani ni Fake au hazina Ubora ila ni vema ukanunua simu mpya.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa