JINSI YA KUJUA KAMA SIMU YAKO IMEKUWA ROOT AU BADO

Wengi tumekuwa na kiu ya ku root simu zetu ili tuweze kubadili muonekano mzima wa simu. Simu ikiwa rooted ina faida nyingi. Moja ya faida kubwa ni kuweza kuweka custom rom pamoja na exposed framework.

Swali linakuja kwamba utajuaje kama simu yako tayari imekuwa rooted au bado.



Njia rahisi ya kujua kama simu yako ipo rooted au bado unatakiwa ku download ROOT CHECKER kutoka kwenye play store

STEP 1
Search for root checker kwenye play store kama picha inavyoonyesha chini kisha install kwenye simu yako


STEP 2
Baada ya kumaliza ku install root checker kwenye simu yako ifungue hiyo app kisha utaona muonekano kama kwenye picha chini

STEP 3
Bonyeza sehemu iliyoandikwa VERIFY ROOT. Endapo utaona muonekano kama huo hapo chini basi simu yako tayari ipo rooted kama utapata muonekano mwingine tofauti na huo hapo chini basi simu yako haipo rooted. Unapaswa ku root ili uweze kuweka custom rom

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa