NJIA 10 ZA KULINDA KIFAA CHAKO CHA ANDROID SMARTPHONE NA TABLET

As salaam aleikum mpendwa kama kawaida msomaji wangu kutokana na kutokuwa hewani kwa muda mrefu sasa ni muda wa kuweka makala za kutosha hadi tuombane po, wacha tuendelee Kulinda simu yako au tablet yako ya Android hakuishii kwenye kuweka screen lock tu, la hasha kuna njia nyingine nyingi za kuifanya simu na data zako kuwa salama muda wote.
Leo tujaribu kuangalia njia 10 zitakazokusaidia kuifanya simu yako iwe salama muda wote. Tumeamua kuanza na simu na tablet za android kwa sababu asilimia kubwa simu zinazotumika hapa Tanzania kwa sasa ni za Android.

1. Weka Screenlock
Kuweka lock kwenye screen yako ni njia moja ya muhimu ya kuilinda simu yako hasa pale unapoipoteza au unapoiacha kwenye mikono isiyo salama. Katika mfumo endeshi wa android unaweza ukaweka screen lock tofauti kama PIN lock, Pattern lock, Password lock au Fingerprint scanner kama simu yako inauwezo huo. Kuna baadhi ya matoleo unaweza ukaweka voice lock au eye scanner lock. Hii inamzuia mtu mwingine asiyehusika na simu yako kuweza kuifungua bila ridhaa yako. Kuset screen lock fungua Settings–> Security–> Screen lock na hapo utachagua inayokufaa.

2. Lock Application zako za msingi, picha pamoja na video
Unaweza ukaongeza ulinzi katika application zako ambazo hutaki mtu mwingine aweze kuzitumia au kuzifungua kwa kuzilock kwa kutumia baadhi ya application za kulock mafail na application kama App Lock inayopatikana googe play store. Hii itakusaidia sana kulinda taarifa zako za ndani hata kama mtu amefanikiwa kutoa screen lock yako.

3. Hakikisha Mfumo Endeshi wako (OS) pamoja na Application zote unazotumia zipo Updated
Hii ni ya msingi zaidi kwani wengi wetu tumekuwa tukipuuzia kupdate application zetu hata pale zinapotuomba kuziupdate. Makampuni yanayotengeneza application husika huwa wanaziupdate sio tu kuongeza vitu vipya au kuongeza ufanisi, hapana bali kuziba mianya yote ya kiusalama iliyoachwa wazi hapo kabla. Unatakiwa kuset simu yako iwe inaupdate application zake automatically pale tu zinapotoka kwa kufungua Settings–> General –>Auto update application ( Hapa inategemea na toleo la android unalotumia).

4. Usidownload Application nje ya Googleplay store
Kwa kawaida simu yako huwa haikuruhusu kudownload application nje ya play store, ila unaweza kubadilisha hili kwenye settings–> security–>Device Administration –> Unknown sources kiurahisi. Sasa sio vizuri kabisa kupakua application nje ya play store kwa usalama wa simu yako. Wadukuzi wengi wamekuwa wakitumia mwanya huu kuiba data za mwenye simu au hata kuiharibu simu yenyewe (Kwa wenye tecno Y6 na H6 watakuwa mashuhuda wa simu zao inafikia kipindi huwezi kuicontrol) . Kwa hiyo unatakiwa kuzima hiyo kama unajua unachokifanya na unauhakika na application unayotaka kuinstal.

5. Kuwa makini na Application Permissions wakati unapoziinstal
Hii ni ya muhimu na kuzingatia sana, mara nyingi huwa tunapoinstal application kutoka Google Play huwa zinaomba ruhusa ya kutumia baadhi ya vitu katika simu yako. Kwa mfano punde tu unapoanza kuinstall Whatsapp huwa inaomba ruhusa ya kusoma majina na namba za simu zako, kutumia kamera yako pamoja na kutumia kinasa sauti chako, mara nyingi huwa tunaziruhusu kwa kubonyeza allow. Sasa hapa ni kwa kuzingatia zaidi hasa unapojaribu kuinstal application ambazo zinaomba ruhusa ya kutumia namba zako za simu au picha zako, lazima uwe na uhakika na hiyo application kwanza.

Kwenye toleo jipya la Android Marshmallow unauwezo wa kuruhusu au kuzuia ruhusa kwa application hata kama tayari umeshainstall.

6. Kuwa makini na taarifa unazoshare
Simu nyingi za Android zinatumia kivinjari cha Chrome kama kivinjari cha kwanza, kivinjari hiki kina uwezo wa kutunza taarifa zako zote za kuperuzi na kuzituma katika vifaa vyako vyote unavyotumia kama vile Tablet, Laptop pamoja na desktop zenye kivinjari hichi. Passwords, bookmarks pamoja na vingine vya ziada kupitia Google account vinaweza kuwa shared kwa kukurahisishia kazi wewe mtumiaji. Ila jaribu kufikiri kama umepoteza simu na ina kivinjari cha Chrome chenye taarifa zako zote, inakuwa rahisi kwa mtu aliyeiokota au kuiiba kusoma au kunakili taarifa zako. Hivyo hakikisha unakuwa makini linapokuja suala la kuchagua ni aina gani ya taarifa unataka kushare na vifaa vyako vingine.

7. Kumbuka kuset Android Device Manager
Android Device Manager ni njia inayokusaidia kutafuta simu yako pale inapopotea au kuibiwa. Kwa kuwasha Android device Manager unakuwa na uwezo wa kufuta data zako zote pale simu yako inapokuwa imeibiwa au kupotea au kuipiga na kuilia kwa sauti. Jinsi ya kuwasha Android Device Manager, nenda kwenye settings–>Securty–>Device administration na hapo utaona kitufe cha kuwasha chaguo hilo.

8. Backup Data zako
Kubackup data zako ni jambo la muhimu la msingi sana hasa linapokuja swala la simu za mkononi au tablet. Kwa mfano kurusu Synchronization ya namba zako za simu kati ya kifaa chako na akaunti yako ya gmail ni jambo la msingi zaidi kwa sasa. hii itakusaidia hata pale unapoamua kubadilisha simu hautakuwa na haja ya kuandika upya contact zako, ni kitendo cha kuingiza email (barua pepe) yako na contact zako zote zitajisave. Pia ni muhimu kutunza data zilizomo kwenye simu yako katika kifaa kingine tofauti na simu yako. Kwenye matoleo ya Lollipop pamoja na Android Marshmallow mtumiaji anaweza akaset backup kwa kuingia tu kwenye settings za simu yake.

9. Jaribu kujikinga na Virusi vya Android pamoja na Malware
Siku hizi kuna mamilioni ya virusi vya kompyuta vimetapakaa mtandaoni, hii haishii kwenye kompyuta tu, hapana mpaka kwenye simu zetu kuna mamilioni ya virusi vinavyoweza kudhuru simu zetu huko mtandaoni na ni muhimu kujua njia fasaha za kujizuia na mashambulizi ya virusi hivi. Ndio wengi tunajitahidi kuinstall Antiviruses katika simu zetu kama vile Avast, Android au Kaspersky lakini hii si ya muhimu sana kwa sasa. Njia pekee na ya usalama ni kuepuka kuinstall applications nje ya Google Play store.

10. Set User Accounts
Kama imetokea simu yako huitumii peke yako, au kama wewe ni baba na simu yako huwa inatumika na watoto wako au mkeo kwenye kucheza magemu, ni vizuri kuset user accounts ili kuruhusu ni nani atakuwa na uwezo wa kufungua nini katika simu yako. Kuanzia toleo la Android Lollpop mtumiaji ana uwezo wa kuset user accounts bila wasiwasi wowote. Fungua Settings–>Users–>Add Users na hapo utaset kulingana na matakwa yako.


0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa