Articles by "Apple"
Showing posts with label Apple. Show all posts
Kampuni ya Apple hivi karibuni imezindua simu zake mpya za iPhone, katika uzinduzi wa simu hizo Apple pia ilitangaza rasmi kuwa mfumo wa iOS 12 unatarajiwa kutoka rasmi hivi karibuni.
Hadi kufikia siku ya leo tayari toleo la iOS 12 limeshatoka rasmi na sasa unaweza kusasisha (update) mfumo huo moja kwa moja kwenye kifaa chako chenye uwezo wa kupokea mfumo huo. Kama wewe unatumia vifaa vifuatavyo basi unaweza kusasisha toleo hilo moja kwa moja.
iPhone Zenye Uwezo wa Kupokea iOS 12
 • iPhone X
 • iPhone 8
 • iPhone 8 Plus
 • iPhone 7
 • iPhone 7 Plus
 • iPhone 6s
 • iPhone 6s Plus
 • iPhone 6
 • iPhone 6 Plus
 • iPhone SE
 • iPhone 5s
iPad Zenye Uwezo wa Kupokea iOS 12
 • 12.9-inch iPad Pro 2nd generation
 • 12.9-inch iPad Pro 1st generation
 • 10.5-inch iPad Pro
 • 9.7-inch iPad Pro
 • 9.6-inch iPad
 • iPad Air 2
 • iPad Air
 • iPad 5th generation
 • iPad mini 4
 • iPad mini 3
 • iPad mini 2
iPod touch Zenye Uwezo wa Kupokea iOS 12
 • iPod touch 6th generation
Kama tayari unavyo moja ya vifaa hivi basi unaweza ku-update kifaa chako kwa kuingia kwenye sehemu ya Settings > General > Software Update, kisha subiri kidogo utaweza kuona mfumo huona kisha bofya Download and Install. Hakikisha simu yako inachaji ya kutosha kuanzia asilimia 50 au zaidi. Pia hakikisha simu yako inayo bando ya kutosha angalau GB 2 au zaidi.
Kama kwa namna yoyote umeshindwa ku-update kifaa chako kwa kutumia simu yenyewe unaweza kudownload mfumo huu wa iOS 12 kisha install kwa kutumia iTunes, unaweza kupata mfumo huo kwa kudownload kwa kutumia link hapo chini. Kumbuka hakikisha unadownload mfumo kulingana na kifaa chako.
Kama unataka kujua mabadiliko mapya yanayoletwa na mfumo huu mpya wa iOS 12 unaweza kusoma makala yetu hapa. Pia kama unaona kuna link ambayo haifanyi kazi unaweza kutuambia kwa kutuandikiwa kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
CREDIT : tanzaniatech.one
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, baada ya tetesi za muda mrefu kampuni ya Apple usiku huu imefanya uzinduzi wa bidhaa zake mbalimbali ikiwemo simu mpya za iPhone Xs pamoja na iPhone Xs Max. Simu hizi ni picha halisi ya simu mpya za Apple zitakazo endelea kuwepo kuanzia mwaka huu, hii inamaanisha kuanzia sasa inawezekana kabisa simu zenye muundo wa zamani hazitokwepo tena sokoni na badala yake sasa tegemea kuona simu za iPhone zenye muundo wa iPhone X.
Anyway.. tukija kwenye uzinduzi wa siku ya leo, kampuni ya Apple imeweza kuzindua simu hizi ambazo zinakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na kioo kikubwa cha inch 6.5 kwa simu ya iPhone Xs Max ambayo pia inakuja na kioo chenye teknolojia ya “Super Retina” display chenye resolution ya 1242 x 2688 pixel pamoja na teknolojia zingine kama vile HDR10 pamoja na Dolby Vision.
Kwa upande wa iPhone Xs yenyewe inakuja na teknolojia hizo hizo lakini inakuja na kioo kidogo cha cha Inch 5.8 chenye resolution ya 1125 x 2436 pixels. Simu zote mbili za iPhone Xs na iPhone Xs Max zinakuja na kamera mbili kwa nyuma zenye uwezo wa Megapixel 12 kwa kila kamera huku pia simu hizi kwa mbele zote zikiwa na kamera za Megapixel  7. Sifa nyingine za iPhone Xs na iPhone Xs Max.
Sifa za iPhone Xs
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1125 x 2436 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12
 • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@60fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF , na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery haujajulikana) battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Space Gray na Silver, Gold
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 2m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).
Kwa upande wa simu ya iPhone Xs Max hakuna tofauti sana kwani tofauti kubwa iliyoko kati ya iPhone Xs na iPhone Xs Max ni ukubwa wa kioo pekee.
Sifa za iPhone Xs Max
 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1242 x 2688 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12
 • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
 • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@60fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF , na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery haujajulikana) battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Space Gray na Silver, Gold
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 2m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).
Bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max
Kwa upande wa bei simu hizi mpya za iPhone Xs na Xs Max zinakuja kwa bei ya dollar $999 mbayo ni sawa na Tsh 2,284,000 kwa iPhone Xs yenye GB 64, huku iPhone Xs ya GB 256 itauzwa kwa dollar $1,149 ambayo ni sawa na Tsh 2,627,000, na iPhone Xs ya GB 512 itauzwa kwa dollar za marekani $1,349 sawa na Tsh 3,084,000. Kwa sasa bado bei ya iPhone Xs ya GB 128 haijajulikana rasmi.
Kwa upande wa iPhone Xs Max yenye ukubwa wa GB 64 itakuja kwa dollar za marekani $1,099 ambayo ni sawa na Tsh 2,512,000, huku kwa iPhone Xs Max ya GB 128 yenyewe itauzwa kwa dollar za marekani $1,249 ambayo ni sawa na Tsh 2,855,000, huku iPhone Xs Max ya GB 512 yenyewe itauzwa kwa dollar za $1,449 sawa na Tsh 3,312,000 bila kodi.
Na hizo ndio sifa pamoja na bei ya iPhone Xs pamoja na iPhone Xs Max ambazo zimezinduliwa hivi karibuni, simu hizi zitaanza kupatikana rasmi kuanzia mwezi ujao tarehe 19.
Mkutano wa WWDC 2018 bado unaendelea huko San Jose Convention Center, California, nchini Marekani, ikiwa leo inakuwa siku ya pili ya mkutano huo ulio anza siku ya jana na ukitarajiwa kufikia ukomo wake siku ya tarehe 8 ya mwezi huu wa sita.
Kama ulifanikiwa kuangalia mkutano wa ufunguzi wa WWDC 2018 hapo jana, basi lazima utakuwa uliona baadhi ya mambo mapya ikiwepo ujio wa mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS 12. Kwenye makala hii tutaenda kuangalia mambo yaliyo tangazwa yanayo tarajiwa kuwepo kwenye mfumo huo mpya wa uendeshaji wa iOS 12. Bila kupoteza muda twende tukangalie mambo hayo mapya.
Screen Time

Kwenye mfumo mpya wa iOS 12, Apple imejikita kuhakikisha unatumia kifaa kwa namna bora na kwa kuzingatia afya. Kipengele kipya cha Screen Time kwenye mfumo wa iOS 12 kitafafanua ni muda gani unatumia kwenye kifaa chako na pia itaonyesha ni muda gani unatumia kwenye programu mbalimbali. Sehemu hiyo pia inaweza kutenganisha matumizi ya programu kwa vikundi kama vile (michezo, mitandao ya kijamii nk) ikiwa pamoja na kufuatilia programu ambazo zinatuma taarifa (Notification) zaidi. Screen Time pia itatoa muhtasari wa kila wiki wa tabia zako za matumizi ya kifaa chako.
Kama ilivyo kwenye mfumo wa Android P, utaweza kuweka mipaka ya muda kwa kila programu unayo tumia. IOS itakupa taarifa moja kwa moja kama utakuwa umezindisha muda ulio jiwekea kwenye kila programu. Ujumbe wa “Muda Umeisha” utaonyeshwa kama muda ulio jiwekea utaisha  na endapo unataka kuendelea kutumia programu hiyo, unaweza kuongeza muda kwenye programu husika.
Group Notification

Kwenye mfumo huu mpya wa iOS 12 Apple inakuja na njia mpya ya kuweza kudhibiti taarifa unazopata kwenye kifaa chako. Group Notification hii ni sehemu mpya ambayo itakusaidia kukusanya taarifa (notification) zote zinazo ingia kwenye kifaa chako kwa kuzipanga kwa vikundi (group) maalum. Kwa mfano kama unapata mchanganyiko wa taarifa (Notification) za whatsApp na meseji za kawaida kutoka kwa watu mbalimbali, sehemu hii ya Group Notification itakusanya taarifa zote za WhatsApp na kuziweka sehemu moja na taarifa zote za meseji za kawaida na kuziweka sehemu moja. Pia sehemu hiyo itakupa urahisi wa kufuta taarifa (Notification) nyingi kwa wakati mmoja.
Animoji Tongue Detection
Kupitia mfumo mpya wa iOS 12, Apple pia inaleta Animoji mpya za ghost, koala, tiger, pamoja na tyrannosaurus rex. Lakini kama haitoshi Apple imeongeza uwezo zaidi kwenye katuni za Animoji na sasa zitaweza kujua pale utakapo toa ulimi wako nje.
Memoji
Kwenye iOS 12, Apple imeleta aina mpya ya katuni za Memoji, kupitia sehemu hiyo utaweza kuunda Katuni za Memoji zinazofanana na wewe, Kupitia sehemu ya hiyo utaweza kuchagua rangi ya ngozi yako, macho, mdomo, nywele na vingine vingi ili kuweza kutengeneza sura ya katuni ya Memoji itakayo fanana na wewe.
Group Facetime

Kupitia programu ya Facetime, Apple imeleta maboresho zaidi kwenye programu hiyo kwa kuleta uwezo wa kupiga simu za Video kwa Kikundi. Kupitia programu hiyo utakuwa na uwezo wa kuunganisha hadi watu 32 kwa pamoja. Vilevile Apple imeleta muonekano mpya ambao utasaidia watu wote 32 kuweza kuonekana vizuri kwenye simu au kwenye kompyuta yako ya Mac pale unapokuwa unatumia sehemu hiyo ya Group FaceTime. Mbali na hayo utakuwa na uwezo wa kutumia katuni za Animoji au Memoji wakati unapiga simu za video kupitia programu ya Facetime.
Measure App

Kwenye maboresho mengine ya programu ni pamoja na ujio wa programu mpya ya Measure App, hii ni aina mpya ya programu itakayo kuwepo kwenye iOS 12 ambayo itakupa uwezo wa kufanya vipimo kwa kutumia kioo cha simu yako kwa kutumia teknolojia ya Ukweli ulioongezewa au kwa jina la kitaalamu AR au Augmented Reality.
Maboresho ya App ya Photos
Maboresho mengine ya programu ni pamoja na app ya Photos, ambayo sasa itakuwa na sehemu mpya ya “For You” ambayo itakuwa ikionyesha aina mbalimbali za Effect za kuweka kwenye picha zako, picha gani nzuri ya kushiriki kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na mambo mengine mbalimbali yanayohusu picha ndani ya simu yako yenye mfumo mpya wa iOS 12.
Shortcut App

iOS 12 inakuja na maboresho pia ya Siri na baadhi ya maboresho hayo ni pamoja na ujio wa App mpya ya Shortcuts, App hii inakusaidia kuweza kutengeneza maneno binafsi ambayo utaweza kuyatumia pale unapotaka kutumia programu ya Siri.
Maboresho Mengine
Mboresho mengine ni madogo madogo ambayo ni pamoja na mabadiliko ya App ya Habari Apple News, Mbadiliko ya jina la programu ya iBooks na sasa itakuwa inaitwa Apple Books pamoja na Mabadiliko ya App ya Stocks, ikiwa pamoja na ujio wa App ya Voice Memo kwenye vifaa vya iPad. Mbali na hayo mabadiliko mengine ni pamoja na kuwepo kwa sehemu ya iCloud kwenye sehemu ya Voice memo ambayo utaweza kuhifadhi sauti zako kwenye iCloud.
Na hayo ndio mabadiliko makubwa ya mfumo mpya wa iOS 12 ambao unategemewa kuja rasmi mwaka huu kwa watumiaji wote wa vifaa vya iOS. Kupata habari zaidi za mkutano wa WWDC 2018 endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kutembelea ukurasa wetu maalum wa #WWDC 2018 ili kupata habari zaidi za mkutano huo.