Hizi hapa tofauti kati ya Apple pencil na S-Pen

Wiki hii apple imetangaza toleo jipya la bidhaa yake mpya ya apple pencil ikiwa na features mbalimbali na kutikisa vichwa vingi vya habari za kiteknolojia, Je bidhaa hii ni bora kuliko samsung Pen? Zijue tofauti na ubora wa bidhaa hizi


S Pen na Apple Pencil ni kalamu mbili za stylus zinazotumiwa na simu na kompyuta za Samsung Galaxy na iPad.Zote mbili zinatumia teknolojia inayoitwa digitizer


Kalamu hizi hutumika:

Kuandika na kuchora

Kuchukua noti

Kuhariri hati

Kupiga picha na video


1.Ncha: S Pen ina ncha laini ya mpira, wakati Apple Pencil ina ncha ngumu ya plastiki.


S pen ina design nzuri ya ncha ya mpira ili kuilinda screen za vifaa vyake zisiweze kukwaruzwa huku apple pencil zikiwa na ncha ya plastick mahususi kutumika kwa baadhi ya iPads tu

2.Kitufe: S Pen ina kitufe upande, wakati Apple Pencil haina.


3. Kuchaji: S Pen inachaji bila waya(pale inaporudishwa ndani ya simu) , wakati Apple Pencil inahitaji kuchajiwa kwa kutumia kebo ya Lightning au USB-C (2nd gen inauwezo wa kuwa na wireless charging)


Utangamano: S Pen inatumika tu na vifaa vya Samsung Galaxy Note, wakati Apple Pencil inatumika tu na baadhi ya iPad.


Bei: S Pen inajumuishwa na vifaa vya Samsung Galaxy Note, wakati Apple Pencil inahitaji kununuliwa peke yake kama bidhaa nyingine


Apple Pencil ni ghali zaidi inauzwa kuanzia $99-129 sawa na Tsh 247599.00- 322629.00

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa