JINSI YA KUWEKA AUDIO (Mp3) KATIKA BLOG KUPITIA MTANDAO WA HULKSHARE

As salaam aleikum watu wangu karibuni tena na tena leo nimeleta hili la kuweka au kupost audio katika blog au webiste kupitia mtandao wa hulkshare nimeandika hili mahususi kwaajili ya maombi ya wasomaji wangu Steve cheuc mmiliki wa blog ya swahibanewz.blogspot.com na ndugu yangu mwingine Shafii Omary mmiliki wa blog ya al-imaani.blogspot.com, lakini na kwaajili yako pia wewe unaesoma muda huu.


jisajili katika mtandao wa hulkshare

Unaweza kujisajili kupitia twitter au facebook lakini njia bora zaidi ni kujaza fomu hiyo waliyokupa kisha bonyeza SIGN UP kisha watakupa mtihani wa kujaza namba au maneno ya kuthibisha kuwa wewe sio Robot kama picani hapa chini
watakuletea fomu nyingine kujaza kama wewe ni blogger au artist au produce n.k pia unaweka muziki wa aina gani na baadhi ya vitu kama inavyoonekana pichani hapa chini
Utaletewa dashbodi ya akaunti yako ambayo inakuwezesha wewe kuedit akaunti yako yote kwaujumla kama upatikanaji wako katika mitandao ya kijamii n.k

mpaka hapo akaunti yako ya hulkshare imekamilika sasa unaweza kuanza kupakia audio zako

jinsi ya kupakia audio katika hulkshare

Bonyeza sehemu iliyoandikwa UPLOAD kisha bonyeza SELECT FILE TO UPLOAD 
chagua audio unayohitaji kupakia kisha jaza jina la msanii na jina la album
itasoma asilimia kama hapo juu itafika mia kisha hapo kwenye kialama cha mtu watatokea watu kisha upande mwingine itatoke tiki mpaka hapo audio  yako itakuwa tayari kutuka tazama picha hapa chini
kisha bonyeza jina la hiyo audio yako itatokea audio yako katika mfumo huu pichani

Jinsi ya kuweka katika blog post yako

Bonyeza sehemu iliyoandikwa share kisha copy code zilizopo katika widget hii ni kwa watumiaji wa blogger ila kama unatumia wordpress copy code zilizopo katika wordpress
kisha nenda katika blog yako katika uwanja wa post kisha andika kichwa cha chapisho lako kisha bonyeza HTML kisha paste (pachika) zile code ulizocopy katika upande wa HTML kisha compose kisha post 
Ukisha compose unaweza usione kitu ila baada ya kupost utaona muonekano wa audio yako kama hapa chini



Mpaka hapo umefanikiwa kuweka audio katika blog yako kilichobakia ni kuwa utakuwa una UPLOAD tu kisha unacopy code kama nilivyokueleza hapo juu hakuna kujisajili tena.

Imeandika nami Riyadi Bhai Sambaza kama ilivyo. unaweza kuniuliza sehemu ambayo hujaelewa nitakusaidia jisikie huru

6 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa