Wafahamu waanzilishi wa makampuni makubwa ya teknolojia.

 

Teknolojia ikiwa imechukua nafasi kubwa ya maisha yetu katika kipindi hiki , ni vigumu kupita siku haujatumia applications , search engines , operating systems au kwa ujumla software ambazo ni zao la uvumbuzi wa watu ambao leo tunawaita vichwa wa teknolojia.


Stori nyingi zinazoshika chati ni zile kuhusu vijana wadogo walioamua kuacha vyuo na nakujaribu kutimiza ndoto zao kwa kufuata kile wanachokiamini. Basi leo tuwafahamu kwa ufupi watu hawa.


1.Bill Gates na Paul Allen || Microsoft.

Siyo kila stori za co founders wa makampuni makubwa ya teknolojia huwa na mwisho mzuri, japo co founders hawa wote wawili waliishia kuwa mabilionea lakini uhusiano wao haukuisha pazuri.


Wakiwa ni marafiki toka utotoni walikutana katika shule ya Lakeside mjini Seattle, na mwisho wa miaka ya sabini , walihamia Boston ambapo Gates alijiunga chuo cha havard na Paul alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Honeywell.


Wakiunganishwa na mapenzi ya kompyuta na Basic programming walijikuta wakianza kutengeneza na kuuza software kwa ajili ya Altair 8800 moja kati ya personal computers za kwanza kabisa.


Mwisho wa mwaka 1975 wakahalalisha patnership yao na kampuni ya altair wakiwa kama kampuni inayoitwa Micro-Soft.


Gates akiwa kijana wa miaka 19 ,hakuweza kwenda kwenye presentation ya kwanza ya programming language waliyoitengeneza kwa ajili ya Altair akihofia kwamba hawatomchukulia serious hivyo kazi hiyo aliifanya bwana Paul ambaye kidogo alikuwa amemzidi umri Gates.


Microsoft kwenye miaka ya themanini ilikuwa kwa kasi , lakini mahusiano kati ya hawa co founders hayakuwa mazuri, hivyo kupelekea kugawana umiliki wa kampuni hiyo (60/40) Gates akichukua asilimia kubwa zaidi kwa kigezo kwamba yeye alikuwa mwanafunzi huku Paul akiwa mfanyakazi anayepokea mshahara kipindi wanatengeneza kampuni hiyo.


Baadaye magawanyiko ulikuja kuwa (64/36) kwa kile bwana Gates alichokuwa anadai kwamba mchango wa Paul kwenye kampuni umepungua kwa kiasi kikubwa.


Ni katika kipindi hicho Paul alikuwa akipambana na kansaMwaka 1983 Paul aliacha kazi Microsoft lakini akabaki kwenye bodi ya wakurugenzi mpaka pale mauti yalipomkuta akiwa na umri wa miaka 66.


2.Steve Jobs na Steve Wozniak || Apple

Tofauti na uhusiano wa Gates na Paul, combo ya Jobs na Woz ilikutanisha marafiki wawili mmoja (Wozniak) akiwa ni electronic guru na computer hobbist, huku Jobs akiwa ni mtu wa maono ya kibiashara asiyejua chochote kuhusu programming .


Zao lao la kwanza liliitwa " blue box" iliotumika kupiga simu za masafa marefu. Mwaka 1976 walileta kompyuta yao ya kwanza ikiitwa Apple I computer.


Ikiwa ni safari ya misukosuko mwaka 1985 Jobs alitolewa kwenye nafasi yake kama CEO wa Apple na kukaa nje ya kampuni aliyoitengeneza kwa miaka 12 mpaka pale bodi ya wakurugenzi ilipomuomba arudi kwani kampuni ilikuwa inaelekea kufirisika.


Bwana Wozniak aliacha kazi Apple mwaka ambao Jobs aliondolewa kama CEO wa Apple. Sababu kuu ilomtoa Woz Apple alidai kwamba yeye ni injinia na mikakati ya kimasoko ya kampuni hiyo inamzuia yeye ashindwe kuishi kwenye kile anachokipenda.


Woz baada ya kuondoka Apple amekuwa ni co founder wa makampuni mbali mbali kama Electronic Frontier Foundation na Silicon Valley Comic con.


Mpaka sasa Woz yupo kwenye orodha ya wafanyakazi wa Apple na ni mmoja wa wamiliki wa hisa za kampuni hiyo . Anadai kwamba mpaka sasa bado anaripoti kwa Jobs ambaye alikufa mwaka 2011 kwa maradhi ya kansa.


3.Mark Zuckerberg || Facebook.

Akiwa na miaka 19 tu Zuckerberg alitengeneza Facebook February 2004 pamoja na kundi la vijana wenzake Eduardo Saverin, Andrew McCollum, Dustin Moskovitz, na Chris Hughes katika bweni la Havard University.


Wakati huo ilijulikana kama the facebook.com, mwaka huo huo aliacha chuo ili kuwekeza muda wake katika kukuza website yake ambayo kwa maalezo yake anasema ilichukua wiki mbili kui program.


Zuckerberg alifahamiana na Saverin kwa takribani mwaka mmoja mpaka pale alipomkaribisha kuwa muwekezaji wa kwanza wa Facebook, Moskovitz kazi yake kuu ilikuwa ni kupanua wigo wa site hiyo, na kwa mujibu wa Zuckerberg anadai ilimchukua siku kadhaa bwana Moskovitz kujifunza PHP ili kuweza kufanya kazi yake na baadae akawa CTO wa Facebook.


Bwana Hughes alikuwa spokesman wa Facebook, beta tester, Public relations na shughuli zote zinazohusiana na huduma kwa wateja. Huyu hakuandika hata mstari mmoja wa codes.


Zuckerberg alimfahamu Andrew McCollum kupitia darasa la Computer Science nakumuomba atengeneze logo ya kwanza ya Facebook.


Katikati ya mwaka 2004 Zuckerberg, Hughes na Moskovitz walienda Palo Alto California kuanza rasmi kuajiri wafanyakazi ambapo Zuck na Moskovitz waliacha chuo rasmi mwaka huo, huku Hughes alirejea chuoni semester ilipoanza na baadaye aliungana na wenzake mwaka 2006 alipohitimu chuo.


Wakiwa Palo Alto , Zuck alimtoa Saverin kwenye timu yake na kupunguza umiliki wake mpaka asilimia 10 kwa kile alichokuwa akidai kwamba Saverin hakuwa na mchango kwenye timu hiyo.


Mpaka sasa Facebook ina jumla ya watumiaji bilioni 1.86 ulimwengu mzima, ikiwa ni mojakati ya site inayotumika zaii ulimwenguni. Moskovitz aliondoka rasmi Facebook 2007, McColllum mwaka 2006, na Hughes mwaka 2008.


4. Kevin Systrom na Mike Krieger || Instagram.

Kwa wengi ukizungumzia Instagram wanapata picha ya Kevin Systrom, lakini Mike Krieger alikuwepo tangu Instagram inaitwa "Burbn". Mike ambaye alikuwa miaka 2 nyuma ya Kevin pale Stanford university alikuwa akijishughulisha na utengenezaji wa app yake kwa jina la" Meebo" mpaka pale kampuni ya Systrom ilipomchkua, baadaye Kevin pia alijiunga na kampuni hiyo, waliungana pamoja na kutengeneza Burbn ambayo ilikuwa ni photo sharing app.


April 2012 Zuckerberg na Facebook wakaichukua Instagram kwa dola billioni moja . Wawili hao walikaa Facebook mpaka mwaka 2018 ambapo ghafla walitangaza kujitoa Facebook na wakaachia nyadhifa zao kama CEO na CTO.


5.Lerry Page na Sergey Brin || Google.

Kijana Lerry Page akiwa na miaka 22 alitembelea chuo kikuu cha Stanford mwaka 1995 akiwa na nia ya kujiunga kwa masomo ngazi ya PhD, Sergey kijana mwenye miaka 21 ndiye aliyekuwa akimuonesha mazingira bwana Page walipokutana kwani Larry alikuwa tayari ni mwanafunzi chuoni hapo katika ngazi ya PhD.


Page alianza utafiti wa namna gani websites zinaweza jumuika kwa pamoja na hapo ndipo akaanza kutengeneza teknolojia ambayo itaziunganisha websites zote kwa pamoja. Brinn alipendezwa na wazo hilo hivyo wakaunga nguvu kutengeneza search engine ambayo leo inajulikana kama Google.


Rasmi mwaka 1998 , Page na Brinn wakaacha chuo nakuanza rasmi kampuni yao katika karakana. Katika siku za mwanzoGoogle ilikuwa inapokea searches elfu 10 kwa siku lakini hivi sasa inakadiliwa kuwa Google inapokea zaidi ya searches bilioni 3.5 kwa siku.


6.Jack Dorsey ,Biz Stone, Ev Williams, and Dick Costolo || Twitter.

Dorsey ni kijana aliyeacha chuo mara mbili, akiwa chuo kikuu cha Missouri-Rolla , Dorsey alidukua website ya kampuni ya Dispatch Management Services nakugundua mianya ya kiusalama.


Mkurugenzi wa kampuni hiyo alimuajiri na kumuamishia jijini Newyork ambapo aliajiunga na chuo kikuu cha New York ambapo hakukaa muda mrefu akahamia San Fransisco.


Twitter kiuhalisia ilitokana na Odeo , kampuni iliyotengenezwa na Noah Glass pamoja na Evan 'Ev' Williams (aliyekuwa cofounder wa Blogger kabla haijauzwa kwa Google).Williams alitaka wazo jipya mara baada ya itunes kutoa podcasting platform mpya mwaka 2005 kwa ajili ya ipods.


Wazo jipya lililetwa na Dorsey ambaye ndiye aliyekuwa designer wa Odeo. Glass alivutiwa na wazo la Dorsey hivyo akamuanganisha na developer kwa jina la Florian Webber kutengeneza prototype ya Twitter ambayo kwa mara ya kwanza ilijulikana kama "Twittr".


Hadi kufika mwaka 2010 Twitter ilikuwa na watumiaji zaidi ya milioni 105.


7. Evan Spiegel, Bobby Murphy and Reggie Brown || Snapchat.

Ikiwa kama project ya mwaka wa mwisho chuoni bwana Spiegel kijana wa miaka 22 aliwaeleza wenzake kuhusu wazo lake la kutengeneza photo sharing app ambayo picha zinazokuwa shared zitapotea milele.


Lilionekana ni wazo la kijinga lakini haikumkatisha tamaa. Miezi michache baadae Spiegel na wenzake wakaanzisha Snapchat sebuleni kwa baba yake Spiegel jijini Los Angeles ambayo kwa mara ya kwanza ilijulikana kama "Picaboo,".


Murphy, Ilimchukua masaa 18 ndani ya siku kuandika codes za prototype ya Snapchat.Mpaka leo anabaki kuwa CTO wa Snapchat na ndiye muandishi wa asilimia kubwa codes zilizounda Snapchat.


Kama ilivyo kwa wengine wengi CEO wa Snapchat aliacha chuo akikaribia kuhitimu na kujikita katika kuikuza kampuni yake. Mwaka 2018 alirudi chuoni na kumalizia shahada yake.


8. David Karp || Tumblr.

Karp hakumaliza hata high school( ali drop akiwa na miaka 14) na wala hakuingia chuo. Hivyo vyote havikumfanya ashindwe kuingia katika uwanja wa teknolojia na akiwa na miaka 19 tu aliweza kuwa CTO wa kampuni ya Urban Baby ambayo ilikuja kununuliwa na CNET mwaka 2006.


Kutokana na mauzo ya Urban Baby , David alipata dola elfu kadhaa ambazo alizitumia kuanzisha kampuni yake ya DavidVille ambayo ndani yake ilizaa makampuni mengine ikiwemo Tumblr mwaka 2006.


9.Garrett Camp || Uber.

CEO maarufu aliyepita wa kampuni hii ya Uber bwana Travis Kalanick ndiye anayefahamika kwa wengi kama ndiye muanzilishi wa kampuni hiyo lakini bwana Garrett ndiye yuko nyuma ya pazia katika kutengeneza na kuanzisha kampuni hiyo.


Kalanick alaiwahi nukuliwa akisema " "I just want to clap and hug him(Garrett) at the same time". Prototype ya uber iliandikwa na Camp huku Kalanick akiwa kama mshauri mkuu.


Aliteuliwa (Kalanick)baadae kuwa CEO wa kampuni hiyo mpaka mwaka 2010 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Ryan Graves.


Camp kwa sasa yupo kwenye bodi ya wakurugenzi wa Uber japo hajihusishi na shughuli za kila siku katika kampuni hiyo. Anamiliki asilimia 5% za hisa katika kampuni hiyo.


Hao ni baadhi tu ya waanzilishi wa makampuni makubwa ya teknoljia ulimwenguni, wengi wao wakiwa ni college drop outs na vijana wenye uthubutu mkubwa wa kufanya maamuzi magumu ili tu wafuate kile wanachokiamini. Hizi ni stori ambazo hatuzisikii kwa vijana wengi wa Tanzania.


chanzo : JF

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa