Articles by "Dondoo"
Showing posts with label Dondoo. Show all posts
As salaam aleikum wapendwa, je umeshawahi kusikia kuhusu hili la 5G? Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G

Makampuni mengi ya kutengeneza simu tayari yanavutiwa na wazo hili. Wachambuzi wengi wametabiri kwamba mtandao huu wa kizazi cha 5 (5G) utapatikana ifikapo mwaka wa 2020 na Qualcomm kampuni kubwa ya smartphone inafanya kazi kwa bidii ili kufanikisha wazo hili.

Je 5G ni nini?

5G ni teknolojia ya wireless broadband ya kizazi cha tano yenye kiwango cha IEEE 802.11ac. Teknolojia ambazo zitatumika katika 5G bado zinaelezewa.

mitandao ya 5G itatumia aina ya encoding inayoitwa OFDM, sawa na ile inayotumiwa katika 4G LTE, na mitandao ya 5G itakuwa midogo sana na ya kisasa zaidi, ikilinganishwa na mifumo yote ya awali.

Ufafanuzi wa mtandao wa 5G:

International Telecommunication Union (ITU) imetoa maelezo yafuatayo kuhusu kizazi cha tano cha mitandao ya simu. Uwezo wa jumla wa kupakua kwa simu ya mkononi ya 5G lazima iwe angalau 20Gbps.

Kiwango cha 5G kinachokuja kitakuwa na uwezo wa kuunganisha vifaa milioni 1 kwa kilomita ya mraba

Kiwango hicho kitahitaji “carriers” kuwa na angalau 100 MHz za ziada, hadi 1GHz kama inawezekana.

Simu ya Mkono ya 5G ni nini ? Mtumiaji wa Twitter aitwaye Sherif Hanna alishirikisha picha ya smartphone ya kwanza ya 5G dunia. Yeye pia ni Marketing Lead wa LTE na 5G NR Modems za Qualcomm.

Soma [ fahamu kuhusu technolojia ya 2G,3G,4G na 5G ]


Tweet yake inasema – “Ngumu kuamini kwamba nina smartphone ya kwanza ya 5G mkononi mwangu!”

Kwa mujibu wa Digit, picha hiyo kimsingi ni ya mfano wa simu ya kwanza ya 5G ya Qualcomm na sio simu halisi kwa sababu bado ipo kwenye hatua za mwanzo za kutengenezwa. Smartphone hii imewekwa maalum ili kupima na kufanya uboreshaji muhimu wa utendaji wa 5G mmWave.

5G sio tu itawezesha matumizi mazuri ya simu za mkononi, lakini pia itaanzisha zama za magari yasiyo na dereva na smart homes.

Wakati wa Mkutano wa Qualcomm 4G / 5G wa mwaka 2017, walitangaza Qualcomm Snapdragon X50 5G modem na waliweza kufikia uhusiano wa data wa 5G kwenye chipset ya modem ya 5G kwa vifaa vya simu.

Je' unamaoni gani kuhusu teknolojia hii ya 5G niachie maoni yako hapo chini
As salaam aleikum, Inawezekana ukawa mmoja wa watumiaji wa iPhone kwa kipindi sasa na unafahamu mambo mengi sana kuhusiana na simu hizi kutoka kampuni ya Apple. Swali je, ushawahi kuona kitundu cheusi katikati ya kamera ya flash, unafahamu matumizi yake?

Kwa kifupi kuanzia toleo la iPhone 5 kila simu ya iPhone baada ya toleo hili ina kitundu cheusi katikati ya kamera na flash. Kimsingi kitundu hicho ni Microphone. Ndio ni Microphone inayotumika kupunguza mwingiliano wa mawimbi ya sauti.

Microphone (kinasa sauti) hii imewekwa maalumu kwa ajili ya kupunguza mwingiliano wa mawimbi ya sauti ili kumwezesha msikilizaji wa upande wa pili wa simu asisikie vitu vingine tofauti na kile kinachozungumzwa na mwongeaji mwenza.

Haijawahi kukutokea unaongea na mtu kwenye simu alafu kwa mbali unasikia sauti za watu wengine walio karibu yake? Au kukatishwa maongezi na mtu uliyempigia kwa sababu yupo kwenye daladala au sehemu yenye purukashani nyingi? Sasa hapo ndipo hiyo Microphone inapofanya kazi yake, itanasa mawimbi yote ya sauti yasiyohusika na kupunguza mwingiliano wakati mtumiaji wake anaongea na simu.

Kwa kifupi iPhone zote kuanzia iPhone 5 zina vinasa sauti vitatu (3 Microphones), viwili vikiwa chini ya simu na kimoja kikiwa nyuma ya simu. Uwepo wa programu ya Siri inayohitaji kinasa sauti kizuri ili kuweza kutambua mzungumzaji ameongea nini kunachangia sana kuwekwa kwa microphone hizi tatu.

Nadhani sasa utakuwa umeelewa kwanini iPhone ina kitundu cheusi katikati ya Kamera na Flash.
As salaam aleikum mpendwa karibu tena, hapa huwa tunakutaka na Mkanganyiko mkubwa pale tunapotaka kuchagua kati ya aina hizi mbili za Windows 32-Bit au 64-Bit kwa sababu wengi wetu hatujui nini hasa tofauti zao. Baada ya kusoma makala hii utafahamu na utachagua chaguo sahihi kwa ajili ya kompyuta yako.


Mfumo endeshi wa Microsoft Windows unakuja katika matoleo tofauti tofauti na kila moja likiwa na kitu cha ziada zaidi ya mwenzi wake, na muda mwingine inakuwa ngumu sana kuona tofauti hizi. Mfano mzuri ni huu wa aina hizi mbili za Windows kati ya 32-Bit OS na 64-Bit OS inakuwa ngumu sana kwa mtumiaji wa kawaida kufahamu tofauti zake.
Microsoft walianza kuachia toleo la 64-Bit katika mfumo wao endeshi uliopendwa zaidi duniani na uliohudumu kwa zaidi ya miaka 14 Windows XP. Kwa mara ya kwanza 64-Bit ilianza kutumika katika mifumo endeshi na kampuni ya Cray mwaka 1985 ikiwa na mfumo endeshi unaofanana kabisa na UNIX – UNICOS. Baada ya hapo aina hiyo ya mifumo endeshi ilitapakaa katika Windows, Mac OS X, Solaris pamoja na Android kwa sasa.
Mifumo endeshi hii ya 32-Bit na 64-Bit inatengenezwa ili kuendana na aina ya Processor inayopatikana katika kompyuta husika, kwa maana hiyo inategemea na aina gani ya processor unatumia ili kuweza kutumia mifumo hii. 32-Bit Windows ilitengenezwa ili kuendana na 32-Bit Processor na 64-Bit hivyo hivyo ili kuendana na 64-Bit Processor. Kwa hiyo kabla ya kufanya chochote ni muhimu kufahamu tofauti kati ya aina hizi mbili za processor.

‘bit’ ni nini

Sehumu ndogo kabisa ya data katika kompyuta hufahamika kama ‘bit’ au kwa kirefu ‘binary digit’. Inafahamika kuwa kompyuta inaelewa lugha ya binary tu (lugha ya uwili) yaani ya  0 na 1 kwa hiyo kila bit inaweza ikawa na thamani ya 0 au 1. Kwa hiyo kompyuta huwa inahifadhi data katika makundi ya bit nane nane yanafahamika kama Byte au Octet, na makundi haya kadri yanavyozidi kuwa makubwa ndipo tunapopata Kilobyte, Megabyte, Gigabyte pamoja na Telabyte.

Processor ni nini

Processor au CPU ndio ubongo wa kompyuta, kwa maana nyingine processor ndio inafanya kila kitu katika kompyuta kuanzia kupiga muziki, kuangalia picha, kuvinjari katika mtandao pamoja na kazi zote za kompyuta kwa kutumia mahesabu ya 0 na 1 kama tulivyoona katika bit. Wengine huwa wanachanganya CPU na lile jumba linalobeba kompyuta (Computer case).
Ndani ya processor kuna vitu vinavyoitwa Regista na Logical sakiti, sasa hizi regista ndizo zinazosaidia katika kutunza data za ndani ya processor wakati processor ikiendelea na mahesabu ili kufanya shughuli fulani ya kompyuta. Kwa hiyo kuna ukubwa wa regista katika mfumo wa processor wa 32-bit ni 32-bit na hivyo kwa 64-bit ni 64-bit. Kwa hiyo kinachofanya tupate aina hizi mbili za processor ni Regista zilizomo ndani yake.
Kwa hiyo unaona kabisa 64-bit processor inaipa uwezo kompyuta wa kufanya mambo makubwa kwa sababu ina hifadhi kubwa katika ubongo wake (CPU) ukilinganisha na 32-bit processor.

Tofauti kati ya 32-Bit OS na 64-Bit OS

Mifumo endeshi ya Windows yenye 64-Bit ilitengenezwa ili kusapoti kiwango kikubwa cha RAM ukilinganisha na ile ya 32-Bit. Software kubwa kama Autocard, Photoshop, Cinema 4D pamoja na Magemu yanahitaji kiwango kikubwa cha cha RAM hasa inayotolewa na mfumo endeshi mpaka kufikia 16 exabytes. Kiwango cha RAM za kupachika kinachohitajika hutegemea sana na aina ya motherboard unayotumia.
Kiwango kidogo cha RAM kinachohitajika ili mfumo wa 32-Bit ufanye kazi vizuri ni 1GB wakati ule wa 64-Bit unahitaji 2GB na kuendelea.  Hii ipo wazi kwani 64-Bit ina regista kubwa hivyo kiwango kikubwa cha RAM kitahitajika. Kama unahitaji kupata matokeo mazuri kutoka kwenye kompyuta ya 64-Bit ni bora uwe na RAM inayoanzia 4GB na kuendelea na kwa wale wa 32-Bit ni bora uwe na RAM inayoanzia 2GB na kuendelea.
Kitu cha msingi unachotakiwa kufahamu ni kwamba 32-Bit Processor inafanya kazi vizuri tu katika kompyuta ya 64-Bit processor ila hautofurahia uzuri wa processor hii. Unachotakiwa kufanya ni kuweka 64-bit OS. Pia software na Drivers zinahitajika kuwa za 64-bit ili kupata kasi nzuri.
Tatizo kubwa la 64-Bit OS ni kwamba software nyingi zinagoma kufanya kazi na mifumo endeshi hii kwa sababu bado madeveloper hawajatengeneza software za kutosha katika soko zinazoendana na mfumo huu, lakini usihofu kwa sasa utapata software zote za muhimu za 64-bit, mfano Mozila Firefox wameanza kutengeneza kiinjari cha 64-bit hapo Desemba mwaka juzi.
Kwa ushauri, kama unaenda kununua kompyuta kwa sasa ni bora ukanunua ya 64-Bit ili kuendana na mazingira ya teknolojia yanayobadilika kwa kasi hivi sasa na ili kupata faida zaidi ya kile unacholipia.