TAHADHARI: App Zinazoweza Kuiba Taarifa za Benki, Email na Password Zako

UKIANGALIA katika simu yako ni dhahiri Application nyingi ulizopakua ni za bure. Wote tunapenda App za bure.

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako.

Wengi wetu tumekuwa hatusomi vigezo wakati tunapoingiza App hizo ndani ya simu zetu, huwa tunabonyeza tu ‘agree to continue’ bila kusoma.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUS aina ya TROJAN

Virusi hao ambao hutumia majina tofauti-tofauti wana uwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa hackers (wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zina uwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing) ambapo ukijichanganya tu, basi taarifa zako za siri kama bank details, email, password (nywila au neno la siri) zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa wadukuzi.

Credit : JF

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa