Articles by "Apps"
Showing posts with label Apps. Show all posts
As salaam aleikum ndugu wapendwa wasomaji wa Jukwaa hili ni wakati mwingine tena wa kupeana mawili matatu, wenda imeshawahi kukutokea katika pitapita zako katika mitandao ya kijamii ghafla ukatua facebook ukakutana na video ambayo imekuvutia kisha ukashindwa kuipata kutoka na kutokufahamu jinsi ya kuipakua video hiyo, basi leo nimekuletea njia ya kukuwezesha kuishusha video yeyote kutoka facebook bila usumbufu wowote twende sawa hapa chini nimekuwekea maelezo kamili.

kwanza kabisa pakua App ya Fb Video Downloder hapa

kisha fuata hatua hizi ili kushusha video yeyote
fungua app yako ya Fb video downloder kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa GO TO FB Kisha log in katika facebook akaunti yako
kisha tafuta video unayihitaji kuishusha kutoka facebook kisha iguse au ibonyeze hiyo video
utaona option kama inavyoonekana pichani hapo juu kama unahitaji kuiangalia kabla ya kuishusha bonyeza sehemu iliyoandikwa Stream kama unahitaji kudownload bonyeza sehemu iliyoandikwa download
kama utahitaji kuona idadi ya video ulizopakua kupitia app ya Fb Video Downloader bonyeza sehemu iliyoandikwa Gallery
hapo utaona video zako zote pia zitakuwa zimehifadhiwa katika memory ya simu 
Mpaka hapa utakuwa umeshafahamu jinsi ya kupakua video za facebook kama unaswahili kuhusu makala hii unaweza kuniuliza katika sanduku la maoni nami nitakujibu kwa haraka zaidi Enjoy
UKIANGALIA katika simu yako ni dhahiri Application nyingi ulizopakua ni za bure. Wote tunapenda App za bure.

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako.

Wengi wetu tumekuwa hatusomi vigezo wakati tunapoingiza App hizo ndani ya simu zetu, huwa tunabonyeza tu ‘agree to continue’ bila kusoma.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUS aina ya TROJAN

Virusi hao ambao hutumia majina tofauti-tofauti wana uwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa hackers (wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zina uwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing) ambapo ukijichanganya tu, basi taarifa zako za siri kama bank details, email, password (nywila au neno la siri) zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa wadukuzi.

Credit : JF
Kampuni ya Yahoo ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za barua pepe, hivi karibuni imetangaza kuja na huduma mpya ambayo itawaruhusu watumiaji wa huduma za Yahoo kuweza kuchat na ndugu na jamaa pamoja na marafiki kwa kutumia huduma mpya inayoitwa Yahoo Together.
Yahoo Together ni app ambayo imechukua muonekano na mtindo wa App ya Slack ambayo pia hutoa huduma ya kuchat kama ilivyo kwenye app hiyo mpya ya Yahoo Together. Tofauti na app ya Slack, App hii mpya ya Yahoo inakupa uwezo wa kuchat kwenye magroup lakini ni lazima kuwa na barua pepe ya mtandao wa Yahoo ndipo uweze kutumia app hiyo mpya.

Moja kati ya sehemu nzuri kwenye app hii ni sehemu inayoitwa Smart Reminders, sehemu hii itakuwezesha kuweka meseji ili ijitume yenyewe kwa wakati fulani na muda huo utakapo fika meseji hiyo itajituma kwa watu wote kwenye group husika. Sehemu nyingine ni Blast, highlights sehemu ambazo zitakupa uwezo wa kuwekea rangi kwenye meseji fulani ili watu wengine kwenye group waweze kuiona meseji husika pale watakapoingia kwenye group.
Kwa sasa tayari app hii ipo kwenye masoko ya Play Store na App Store hivyo unaweza kuipakua moja kwa moja kupitia masoko hayo
Miezi michache iliyopita mtandao wa instagram ulikuwa ukifanya majaribio ya sehemu ya Nametags, sehemu ambayo inakupa uwezo wa kumfollow mtu kwa urahisi kwa kutumia mfumo kama wa QR Code.
Baada ya majaribio ya muda mrefu hatimaye sehemu hiyo tayari imeanza kuwafikia watumiaji wa mtandao huo kupitia App za Android na iOS. Kupitia sehemu hiyo ya Nametags utawezesha mtu kupata akaunti yako kwa haraka na pia utaweza kushiriki na watu akaunti yako kwa namna ya kipekee.


Sehemu hiyo ya nametags inapatikana kwa kubofya sehemu ya mitari mitatu kwa iliyoko upande wa kulia juu kisha chagua nametags, hapo utaona username yako ikiwa na rangi ambazo unaweza kubadilisha kwa kubofya sehemu yoyote kwenye rangi hiyo, pia utaweza kuchagua picha ya selfie, emoji au kuwa rangi mbalimbali.
Kwa sasa tayari tumesha ona sehemu hii kupitia app ya Instagram ya Android lakini bado hatujaona sehemu hii kupitia programu ya Instagram ya iOS, hivyo ni wazi sehemu hii bado inaendelea kutoka na pengine itawafikia watumiaji wengine siku za karibuni.
As salaam aleikum ndugu wasomaji wetu katika ule mfululizo wa Kutengeneza app kwaajili ya kurahisha maisha yetu ya kila siku leo tumekuletea App kwaajili ya mapishi Ingia playstore tafuta Mapishi.

App yetu hii itakurahisishia kupika mapishi mbalimbali ambayo yameandaliwa kwa lugha ya kiswahili bila kusahau Juisi za asili, App yetu hii ya Mapishi ni bure kabisa hakuna kulipia.

app ya Mapishi inakuwezesha kufahamu Mahitaji yote ya pishi unalohitaji kulipika pia unaweza kuforwad au kutuma meseji ya vitu au mahitaji ya mapishi unayohitaji kujifunza ivo unaweza kumtumia sms muuzaji bila hata kunakili sehemu nyingine.

App yetu ya mapishi imegawanyika katika kategori zaidi ya nane kila kategori moja inamapishi ya aina moja kama kama unahitaji mapishi ya aina fulani unaweza kuchagua kategori unayoipenda pia ipo sehemu kwaajili ya mapishi yote, Mapishi App ni rahisi zaidi kuitumia ijaribu sasa hautajutia kuwa na app ya mapishi.

unaweza kuidownload hapa DOWNLOAD hii ni kwaajili ya watumiaji wa vifaa vya android tu
WhatsApp imekuwa ikifanyiwa maboresho karibia kila mwezi, lakini hivi karibuni mabadiliko mapya yanayokuja kwenye programu ya WhatsApp ni ya tofauti kidogo na mabadiliko mengine. Mabadiliko hayo mapya yanahusiana na chanzo cha mgunduzi wa WhatsApp kuamua kuachana na kampuni ya Facebook ambayo kwa sasa ndio inayomiliki programu hiyo maarufu ya kuchat duniani.
Kama wewe ni mmoja wa wafuatiliaji wa tovuti ya Swahili Tech lazima utakuwa umesoma makala juu ya mmoja wa wagunduzi wa WhatsApp kuachana na kampuni ya Facebook na baadae kutangaza kwa wafuasi wake kwenye mtandao wa Twitter huku akiwahitaji wafute mtandao huo.
Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawajui sababu ya mgunduzi huyu kusema maneno hayo na kuachana na kampuni ya Facebook basi nitakwambia leo. Miaka kadhaa iliyopita waanzilishi hao waligundua programu ya WhatsApp kipindi hicho kama unakumbuka vizuri njia iliyokuwa inatumika na wagunduzi hao kujipatia pesa ni pamoja na watumiaji kulipia dollar $0.99 sawa na Tsh 2,289 kwa mwaka kwa ajili ya kutumia programu ya WhatsApp.
Mara baada ya Facebook kununua App hiyo sehemu hiyo ilitolewa kabisa na WhatsApp ilibaki kuwa programu ya bure kwa asilimia 100. Lakini sasa hivi karibuni kumetokea kutoelewana kwa Facebook na mwazilishi huyo mweza wa programu ya WhatsApp mara baada ya Facebook kutaka kuanza kuonyesha matangazo kupitia App ya WhatsApp. Kama alivyo hojiwa na tovuti ya Forbes mwazilishi huyo alisema kuwa, mpango wa Facebook kutaka kuonyesha matangazo kwenye App hiyo kunatofautiana na sababu ya wao kuanzisha app hiyo hivyo haoni haya ya kuendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo inayo kinzana na sababu zake.
Mpango wa Facebook ni kuja na njia mpya ambayo sasa watumiaji wa App ya WhatsApp watakuwa wanaona matangazo kwenye programu hiyo, najua unajiuliza ni sehemu gani matangazo hayo yatakuwa yanaonekana.? Sasa kwa mujibu wa tovuti ya express.co.uk ambayo lithibitsha hayo kwa kufanya mahojiano na mmoja wa wafanyakazi wa Facebook aliandika kuwa, Hadi kufikia mwaka 2019 WhatsApp itakuwa ikionyesha matangazo kupitia sehemu ya Status ambayo inaonyesha video kwa sekunde kadhaa.
Bila shaka kubadilika huku kwa whatsApp kutakuwa ni pigo kubwa sana kwa watumiaji wa WhatsApp, lakini pengine kwa watu wengine hasa wafanyabiashara hii itakuwa ni habari njema kwani sasa wataweza kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia programu hiyo.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini sehemu hiyo itakuja rasmi kwenye programu ya WhatsApp ila mpaka 2019 tegemea kuanza kuona matangazo kwenye programu ya WhatsApp kama ilivyo programu za Facebook na Instagram. Hebu tuambie wewe onaonaje hii imekaa poa au..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Credit : TanzaniaTech
Wakati mtandao wa Instagram ukiwa kwenye hatua za awali za kuja na programu maalum ya kununua bidhaa kwa kupitia akaunti za Instagram, Kampuni ya Facebook kupitia mtandao wa huo wa Instagram hivi juzi imetangaza kuja na njia mpya ya kuweza kurahisha watu kununua bidhaa moja kwa moja kupitia kwenye app ya Instagram.

Kupitia sehemu ya Stories, Instagram inategemea kuleta sehemu mpya ya Shopping ambayo itakuwa kwenye sehemu ya Explore iliyotambulishwa hivi karibuni ambapo Kupitia sehemu hiyo ya Stories utaweza kuona bidhaa mbalimbali zikiwa zimewekewa stika ambazo utakapo bofya hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye tovuti yenye bidhaa uliyo iona kupitia sehemu hiyo ya Stories.
Kama unavyoweza kuona sehemu hiyo kwenye picha hapo juu, pale utakapo bofya sehemu ya Shopping Explore utaweza kuona bidhaa nyingi kutoka kwenye akaunti mbalimbali ndani ya mtandao wa Instagram. Mbali ya hayo pia watumiaji wa mtandao huo watapewa uwezo wa kuuza bidhaa mbalimbali kwa urahisi kwa kuweka stika ya Shopping ambayo itapatikana kwenye sehemu ya Stika kwenye sehemu ya Stories.

Sehemu hii inatarajiwa kuwafikia watumiaji mbalimbali kuanzia siku ya leo hivyo hakikisha unasasisha (update) toleo jipya la App ya Instagram kupitia masoko ya Play Store na App Store.
As salam aleikum ndugu wasomaji wa blog yetu, katika ule mfululizo wa Apps zetu tunazozitengeneza leo tumewaletea App kwaajili ya Tafsir ya quran, App hii tumeitengeneza katika matoleo mawili Ambayo ni tofauti kidogo.


App yetu hii inaitwa Soma Quran lakini Toleo la pili linaitwa soma quran - All languages, Tafauti ya Toleo la kwanza ni kuwa Toleo la kwa Tumeweka Tafsiri ya quran kwa lugha ya kiswahili pekee, Lakini katika toleo la Soma Qran - All Languages ni kuwa tumeweka tafsir kwa lugha zaidi ya 52+ pia inakuwezesha kusikiliza Quran Mp3, pia utaweza kusambaza Aya moja au surah mzima, pia tumeweka bookmark.

kuistall toleo la kwanza bonyeza hapa Soma Quran

kuistall toleo la kwanza pili bonyeza hapa Soma Quran - All languages

Je unahitaji kutengenezewa App au Website wasiliana nasi 

Asante kwa kuendelea kuwa mengi yanakuja endelea kuwa nasi
Asalam aleykum ndugu zetu watembeleaji wa blog hii. Leo hii katika mfululizo wa applications tunazokuja nazo ni pamoja na apps  ya kukusaidia kupata videos zote za matukio muhimu na kusikiliza Radio Abood Popote pale utakapokuwapo . App hizi zinalenga zaidi katika kukuhabarisha na kukuburudisha. Naam, burudani ni sehemu ya maisha na ni muhimu zaidi kufahamu yanayoendelea katika nchi na dunia yetu kwa ujumla. dunia ni kiganja siku hizi kwa kulizingatia hilo tumekuletea apps muhimu kwaajili ya kuhakikisha hupitwi na tokio wala burudani

Zotekali TV
Hii ni app yakijanja zaidi kuwahi kutokea app hii itakuhabarisha na kukuburudisha masaa 24 kwani app hii inakukusanyia videos zote za matukio, mahojiano kutoka katika channel zote kubwa hapa nchini unaweza kuipakua hapa Zotekali TVAu ingia katika playstore kisha tafuta Zotekali TV

Radio Abood
kwa wale wataalamu burudani basi hapa ndio mahali sahihi kabisa kutokana na maoni ya ndugu Jamaa na marafiki tumeonelea tukekeleze na hili, hii ni App Rasmi kwaajili yakusikiliza Radio Abood popote pale ulipo hata ukiwa chini ya andaki lakini hakuna kitakachokupita katika ulimwengu wa Burudani, ili kuiweka katika simu yako bonyeza hapa Radio Abood


Asalam aleykum ndugu zetu watembeleaji wa blog hii. Leo hii katika mfululizo wa applications tunazokuja nazo ni pamoja na app ya kukusaidia kufanya mazoezi au watu huita "gym". App hii inalenga zaidi katika kukuhimiza kufanya mazoezi na kujua ubora wa mwili wako. Naam, mtu ni afya. Ubora wa binadamu uko katika afya. Kwa kuliona hilo tumefikiria kuja na app hii ya "Mazoezi kwa Dakika 7" yenye aina mbalimbali za mazoezi utakayofanya ndani ya dakika hizo 7. Sanjari na hilo, app hi inatumia lugha nzuri ya kiswahili pamoja na sauti katika kutoa maelekezo.

VILIVYOMO KATIKA APP HII.

1. Orodha ya Mazoezi: Hapa utapata aina ya mazoezi utakayofanya na maelekezo yake kabla hujaanza kwa vitendo.


2. BMI Kalkuleta: Sehemu hii itakusaidia kujua kipimo sahihi cha ulingano kati ya uzito na urefu wa mwili wako. Utaingiza uzito wako na urefu kisha utapata kujua kama mwili wako uko fiti au hapana. Kulingana na shirika la afya la National Institutes of Health (NIH); uzito uliozidi ni kati ya BMI 27.3 au zaid kwa wanawake na 27.8 au zaidi kwa wanaume. BMI 30 au zaidi ni uzito uliokithiri.3. SETTINGS: Hapa utaweza kuseti kiwango cha mazoezi unachotaka kufanya, kama vile idadi ya push-up n.k. App itakupa machaguo (rahisi, kiwango kati, na ngumu). Pia unaweza weka sauti au kuzima wakati wa kutumia app hii.


4. MUONEKANO:  Huu ni mfano wa jinsi utaongozwa katika kufanya mazoezi. Utaona picha pamoja na bar-mzunguko ya kukuonesha kiwango cha ufanyaji kama inavyooneka hapa chini.

Kwa hayo machache tunawaomba mkae nasi na endeleeni kutembelea blogi hii ili kujua mengi. Kupakua app hii bonyeza hapa 7 min Training App (Mazoezini)
As salaam aleikum ndugu zetu leo tunatambulisha Rasmi app yetu mpya kwaajili ya watoto wetu, Tumetengeneza app hii ili kuwafurahisha na kuwajali watoto wetu, app hii itamsaidia mtoto kusoma na kusikiliza simulizi mbalimbali zenye maadili mazuri ya kumjenga mtoto, kwasasa app yetu inahadithi moja ispokuwa tutakuwa tunaongeza hadithi kila tutakapoi-update.

App hii ya Hadithi za Watoto inaweza kutumika hata ukiwa offline yaani hauna bando la Internet. App hii ni bure kabisa haiuzwi unaweza kuinstall katika kifaa chako cha android kwa kuingia playstore na kutafuta Hadithi za Watoto, au unaweza kuinstall kwa kubonyeza hapa Hadithi Za Watoto
Katika kuboresha huduma kwa wateja wake, Programu ya WhatsApp ipo mbioni kuongeza sehemu (Features) mpya nne ambazo zitawasaidia watumiaji wake kupata unafuu na urahisi zaidi wakati wa kutumia.

Taarifa kutoka kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya Teknolojia duniani zinasema kuwa WhatsApp inafanyia kazi sehemu kubwa nne ikiwemo ya kubadilisha na kuhaririri ujumbe uliyomtumia mlengwa kabla hajausoma, sehemu hii itafanya kazi pale ambapo meseji hiyo itakuwa haijapokelewa kwa kuweka tiki mbili za blue.

Maboresho mengine ni kucheza moja kwa moja kwa video za Youtube ndani ya Programu ya WhatsApp, Kwa sasa mtandao wa Youtube ukitumiwa Link ya video kutoka Youtube ni lazima ufungue ila baada ya maboresho hayo mtumiaji ataitizama video yeyote kutoka Youtube bila kufunguwa Link kama ilivyo mitandao mingine ya kijamii.

Kurudisha meseji, picha au video ulizotuma kwa muhusika, kwa wazoefu wa mtandao wa WhatsApp au watu walioanza kutumia tangia mwaka 2015 sehemu hii ilionekana kwenye Whatsapp beta kabla ya kuondolewa mwaka jana 2016, Sehemu hii itarudishwa tena ambapo mtu atapata dakika 5 za kurudisha meseji, Jumbe, picha au video alizotuma kimakosa.

Sehemu nyingine muhimu itagusa kwenye makundi, Kuweka maelezo ya Kundi (Group Description), Kwa sasa watu wengi wanaunganishwa kwenye makundi bila kusoma maelezo ya kundi husika ambapo inakupasa ujiunge kwanza ndiyo upewe maelekezo, Kwa marekebisho hayo utaweza kuandika maelezo kuhusu group, kwa mfano kama ukitengeneza group utaweza kuandika maelezo kuhusu Group hilo, Maelezo ambayo mtu kabla ya kujiunga atayasoma kwanza hii itatokea kwa njia zote mbili ile ya kwanza ya moja kwa moja ya kuunganishwa na Admin na ile ya kutumiwa Link.

Kwa mujibu wa mtandao wa WABETA Info umeripoti kuwa kabla ya mwezi Septemba mwaka huu, Programu ya WhatsApp ambayo inatumiwa na watu zaidi ya Bilioni 1 duniani itatangaza mabadiliko hayo.


Maboresho haya yanaweza kuja kuifunika telegram ambayo kwa sasa ina feature nyingi nzuri lakini haijapata sana umaarufu?


Chanzo : http://wabetainfo.com/
Simu zimekuwa ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku. Kuongezeka kwa huduma za mitandao ya kijamii, kamera bora kwa ajili ya kuchukulia matukio na picha, viwango bora vya app za muziki na vitu vingine vingi vinaifanya simu yako kuwa kama kiungo mojawapo cha mwili. 


Kwa sasa makampuni makubwa ya utengenezaji wa simu yamekuwa yakishindana kutoa matoleo ya simu yenye uwezo mkubwa hasa ule wa kamera. Uwezo wa kamera umekuwa ni moja ya vitu vinavyoifanya simu kuonekana bora au la. 
Hii yote ni kutokana na ukweli kwamba wengi wa watumiaji wa simu za kisasa, smartphones wanapendelea kushare picha na video fupi katika mitandao ya kijamii kama instagram, facebook, twitter au whatsapp. Vipi linapokuja suala la uhifadhi wa picha hizi,  hasa zile tunazopenda kupiga tukiwa maeneo ya faragha au baadhi ya picha ambazo hatupendi wengine wazione?
Hapa ndipo unapokuja umuhimu wa kuwa na app bora ya ulinzi na usalama wa picha zetu. Kuna app nyingi playstore na iTune Store kwa ajili ya uhifadhi na utunzaji wa picha na video za siri. Nyingi ni nzuri lakini hazikidhi moja kwa moja mahitaji ya mtumiaji wa kawaida wa simu. 
Hapa ndipo NQ Vault inapoingia, Vaulty ni app bora kabisa kwa watumiaji wa simu za android. Vault kutoka kwa NQ Vault ina uwezo mkubwa sana linapokuja suala la utunzaji wa data zako siri.
Baadhi ya Faida za NQ Vault ni:
  • Kuficha picha na video na kuzifanya zisionekane hata kwa kuchomeka simu kwenye kompyuta
  • Kuficha sms na missed calls za baadhi ya namba zilizochaguliwa. 
  • Kubackup picha na taarifa zako za siri mtandaoni kulingana na uhitaji wako
  • Uwezo wa kuficha icon ya app yenyewe
  • Uwezo wa kulock app muhimu
Kuna vitu vingi zaidi unaweza ukafaidika navyo kwa kutumia app hii. 
baadhi ya madereva wakilalamika sana kuhusu kulipa fine barabarani kwa kuzidisha mwendo.
Kufuata sheria za barabarani ni jambo la kwanza, ila kuna matrafic wengine wanakera kweli kweli.

Download hii app hapa chini kwenye simu yako, itakujulisha uwepo wa speed kamera nusu kilometa kabla hujaifikia. Utaepuka fine kirahisi.


Speed Cameras & Traffic Sygic - Android Apps on Google Play