Yahoo Yaja na App Mpya ya Kuchat ya Yahoo Together App

Kampuni ya Yahoo ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za barua pepe, hivi karibuni imetangaza kuja na huduma mpya ambayo itawaruhusu watumiaji wa huduma za Yahoo kuweza kuchat na ndugu na jamaa pamoja na marafiki kwa kutumia huduma mpya inayoitwa Yahoo Together.
Yahoo Together ni app ambayo imechukua muonekano na mtindo wa App ya Slack ambayo pia hutoa huduma ya kuchat kama ilivyo kwenye app hiyo mpya ya Yahoo Together. Tofauti na app ya Slack, App hii mpya ya Yahoo inakupa uwezo wa kuchat kwenye magroup lakini ni lazima kuwa na barua pepe ya mtandao wa Yahoo ndipo uweze kutumia app hiyo mpya.

Moja kati ya sehemu nzuri kwenye app hii ni sehemu inayoitwa Smart Reminders, sehemu hii itakuwezesha kuweka meseji ili ijitume yenyewe kwa wakati fulani na muda huo utakapo fika meseji hiyo itajituma kwa watu wote kwenye group husika. Sehemu nyingine ni Blast, highlights sehemu ambazo zitakupa uwezo wa kuwekea rangi kwenye meseji fulani ili watu wengine kwenye group waweze kuiona meseji husika pale watakapoingia kwenye group.
Kwa sasa tayari app hii ipo kwenye masoko ya Play Store na App Store hivyo unaweza kuipakua moja kwa moja kupitia masoko hayo

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa