Mtandao wa Instagram Waleta Rasmi Sehemu ya Nametags

Miezi michache iliyopita mtandao wa instagram ulikuwa ukifanya majaribio ya sehemu ya Nametags, sehemu ambayo inakupa uwezo wa kumfollow mtu kwa urahisi kwa kutumia mfumo kama wa QR Code.
Baada ya majaribio ya muda mrefu hatimaye sehemu hiyo tayari imeanza kuwafikia watumiaji wa mtandao huo kupitia App za Android na iOS. Kupitia sehemu hiyo ya Nametags utawezesha mtu kupata akaunti yako kwa haraka na pia utaweza kushiriki na watu akaunti yako kwa namna ya kipekee.


Sehemu hiyo ya nametags inapatikana kwa kubofya sehemu ya mitari mitatu kwa iliyoko upande wa kulia juu kisha chagua nametags, hapo utaona username yako ikiwa na rangi ambazo unaweza kubadilisha kwa kubofya sehemu yoyote kwenye rangi hiyo, pia utaweza kuchagua picha ya selfie, emoji au kuwa rangi mbalimbali.
Kwa sasa tayari tumesha ona sehemu hii kupitia app ya Instagram ya Android lakini bado hatujaona sehemu hii kupitia programu ya Instagram ya iOS, hivyo ni wazi sehemu hii bado inaendelea kutoka na pengine itawafikia watumiaji wengine siku za karibuni.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa