Asalam aleykum ndugu zetu watembeleaji wa blog hii. Leo hii katika mfululizo wa applications tunazokuja nazo ni pamoja na app ya kukusaidia kufanya mazoezi au watu huita "gym". App hii inalenga zaidi katika kukuhimiza kufanya mazoezi na kujua ubora wa mwili wako. Naam, mtu ni afya. Ubora wa binadamu uko katika afya. Kwa kuliona hilo tumefikiria kuja na app hii ya "Mazoezi kwa Dakika 7" yenye aina mbalimbali za mazoezi utakayofanya ndani ya dakika hizo 7. Sanjari na hilo, app hi inatumia lugha nzuri ya kiswahili pamoja na sauti katika kutoa maelekezo.

VILIVYOMO KATIKA APP HII.

1. Orodha ya Mazoezi: Hapa utapata aina ya mazoezi utakayofanya na maelekezo yake kabla hujaanza kwa vitendo.


2. BMI Kalkuleta: Sehemu hii itakusaidia kujua kipimo sahihi cha ulingano kati ya uzito na urefu wa mwili wako. Utaingiza uzito wako na urefu kisha utapata kujua kama mwili wako uko fiti au hapana. Kulingana na shirika la afya la National Institutes of Health (NIH); uzito uliozidi ni kati ya BMI 27.3 au zaid kwa wanawake na 27.8 au zaidi kwa wanaume. BMI 30 au zaidi ni uzito uliokithiri.3. SETTINGS: Hapa utaweza kuseti kiwango cha mazoezi unachotaka kufanya, kama vile idadi ya push-up n.k. App itakupa machaguo (rahisi, kiwango kati, na ngumu). Pia unaweza weka sauti au kuzima wakati wa kutumia app hii.


4. MUONEKANO:  Huu ni mfano wa jinsi utaongozwa katika kufanya mazoezi. Utaona picha pamoja na bar-mzunguko ya kukuonesha kiwango cha ufanyaji kama inavyooneka hapa chini.

Kwa hayo machache tunawaomba mkae nasi na endeleeni kutembelea blogi hii ili kujua mengi. Kupakua app hii bonyeza hapa 7 min Training App (Mazoezini)
Axact

Ibrahim Riyad Houmud

As Salaam Aleikum, I'm Ibrahim Riyadi Houmud, Founder and CEO of RiyadiBhai blog from Mororgoro, Tanzania. I started this blog as a Passion and it now empowering thousands of readers around the globe.Here I usually share news, Adsense tips, wordpress, gadget, widget, Themes, windows, etc.

Post A Comment:

0 comments:

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa