VERIFY YOUR ACCOUNT. THIS DEVICE WAS RESET. FRP LOCK, KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA?

As salaaKwa wale wanaotumia simu za Android wengi wetu tayari tumekutana na maneno yafuatayo
This device was reset. To continue sign in with Google account that was previously synced on this device

Hayo maneno yanatokana na frp lock ambayo Google huwa wanaiweka kwenye simu za android ambazo zinaanzia Android lollipop. Hili tatizo linatokea pale unapofanya hard reset. Hard reset hii ni njia ya kufuta kila kitu kwenye kwa kutumia recovery ya simu yako. 

Hili tatizo linatokea sana kwenye simu za Samsung. Lakini zipo njia za kuweza kuepuka hili tatizo. Moja njia ambayo itakuwezesha kuepuka hili tatizo ni kuwasha simu yako ya Samsung kwenye download mode kisha tazama kama frp ipo on au off. Mfano kwenye picha chini utaweza ona frp lock ipo on 
Endapo utaona kwenye simu yako ya Samsung imeandika kuwa frp lock ipo on basi usifanye hard reset kama utakuwa ukumbuki email yako na password ambazo ulizitumia ku-sign kwenye simu yako. 

Endapo tayari utakuwa umekumbana na hilo tatizo basi unaweza wasiliana nasi ili kuweza kukusaidia kuitoa hiyo lock kwa gharama nafuu..

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa