FAHAMU MADHARA YA KUKOPI NA KUPASTE MAKALA KUTOKA KATIKA BLOG ZA WATU

As salaam aleikum wapendwa kwa wale waandishi wanafahamu kabisa kuwa Uandishi ni kazi ngumu na inayochosha, uandishi unahitaji kujituma, muda, maarifa na hata pesa wakati mwingine. kutokana na ugumu huo imepelekea blogger's wengi kukopi machapisho katika blog za watu wengine, jambo la kuiba machapisho kutoka katika blog za watu linatokana na uvivu na kutokuwa na mipango wengi wao ni kutokana na kukurupuka kufungua blog bila kujua atakuwa akiweka nini katika blog hiyo. [soma : Mambo muhimu ya kufahamu kabla na baada ya kuanzisha blog ]

kama wewe ni mmiliki wa blog/website hii mada leo ni kwaajili yako ili tujuzane zaidi jinsi ya kuendesha mitandao yetu bila dhurma yeyote fuatana nami.
Utaonekana mnyonge
Unapocopy machapisho katika blog ya mtu hii inapelekea kuwafanya watembeleaji au wasomaji au watumiaji wa blog yako kukuona kuwa wewe ni duni huna kitu chakuwashawishi bila kuiba machapisho ya mtu mwingine [ soma : makosa 4 wanayoyafanya blogger bila kujua ]

jambo ambalo hawatakuwa wakirudi tena katika blog yako ivo watatamani kumjua muandishi wa makala unazokopi ili wapate vitu kwa uhakika.
Kukosa kuonekana katika Search Engine
Google wanafahamu chapisho liliwekwa wapi kwanza. Kwa hiyo ukurasa uliokuwa wa kwanza kuchapisha chapisho hilo ndio utakaopata nafasi zaidi kwenye matokeo ya utafutaji ya Google.
kumbuka kuwa kadri unavyokuwa wa kipekee, ndivyo Google wanavyokupa nafasi ya juu. [ soma : mambo muhimu ya kufanya baada ya kufungua blog ]
Google huzichukulia blog zinazokopi machapisho kama blog zinazokusanya taka “blog scraping”, na kuzipa kuzipa nafasi ndogo katika search Engine.
Kukosa wa dhamini wa kutangaza nawe
Watu au kampuni kabla ya kutangaza nawe kwanza wataangalia ubora na upekee wa blog yako kabla hawajaweka matangazo yao katika blog yako. hakuna mtu anayetaka kupoteza pesa zake kwa kutangaza katika blog ambayo haina watembeleaji wa kutosha na mada zenye mashiko. [ soma : njia ya kupata pesa kupitia blog ya kiswahili ]

ndio maana hata makampuni yanayolipa vizuri kama adsense, amazon n.k hawatoi matangazo kwa blog zinazokopi machapisho.
Kupoteza wasomaji
Nani atakayekuja kwenye blog yako kama anafahamu kuwa kazi yako ni kukopi tu? Ni wazi kuwa watu wakijua wewe unakopi na huna jipya unalowashirikisha, hawatakuja tena kusoma blog yako.
Ni vema kujitahidi kuwa mbunifu ili uwe tofauti na wengine, ni lazima msomaji afahamu kuwa vitu vinavyopatikana kwenye blog yako hawezi kuvipata sehemu nyingine yeyote.
Kukosa kuaminiwa
sasa wewe unakopi kila kitu, hata vitu vya uwongo wewe unakopi tu almuhimu blog yako iwe na makala mpya; unadhani kwa mtindo huo watembeleaji au watumiaji wa blog yako watakuamini? jibu unalo mwenyewe. ukipenda utanijibu hapo kwenye sanduku la maoni ni bure kabisa
Ni bora kuandika machapisho machache lakini ziwe nondo kuliko kuweka machapisho kibao halafu ni  upuuzi mtupu.
Nyongeza
Kuna wakati mwingine mtu  hutamani makala aliyoiona mahali fulani wasomaji wake waifahamu, lakini mara nyingi watu hukosea njia bora ya kutimiza lengo hili. [soma : usikate tamaa kublogging hata siku moja ]
Badala ya kunakili kila kitu unaweza kuandika dondoo au ukaweka kiunganishi cha makala hiyo ili wasomaji wako wafikie chapisho halisi. Unaweza pia kuwasiliana na mmiliki ili kama inawezekana akupe ruhusa halali ya kuchapisha chapisho lake kwenye blog yako.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa