MAMBO MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUFUNGUA BLOG/WEBSITE

Baada ya kufungua tovuti yako kuna mambo ya msingi na ya muhimu kuweza kuyafanya na kuweza kuweka tovuti yako katika hali nzuri.Vile vile kufanya hivi kutachangia katika kuboresha na kuongeza watembeleaji katika tovuti yako;

Andika mada bora na kila baada ya muda fulani.

Mara baada ya kufungua tovuti yako hakikisha unaanda na kuandika mada ambazo ni nzuri na bora.Andika mada zitakazovutia kusoma na zina hadhira pana.Epuka kuandika mada ambazo zina hadhira ndogo maana hautopata watembelewaji wa uhakika.Andika mada ambazo zinaendana na muda huu (updated content)

Weka tovuti yako katika google/bing webmaster tools. kujiunga na bing bonyeza hapa http://www.bing.com/toolbox/webmaster na kujiunga na google webmaster bonyeza hapa https://www.google.com/webmasters/

Kwa kuweka tovuti yako katika hizi webmaster tools kutakuwezesha kujua tovuti yako ina tatizo gani na uweze kulitatua kwa muda muafaka.kupitia hizi webmaster tools utaweza kufanya mabadiliko yoyote kwenye url yako na kuweka au kupunguza maneno katika search results.Ukitaka baadhi ya url zako zisionekane katika serch results ni lazima upitie hapo katika webtools.Vile vile utaweza kujua site yako kama ina malware au ipo under attack.Hauwezi kujua tovuti yako vizuri mpaka upitie hapo katika webtools.

Unganisha site yako na google analytics(au other free/paid analytics tools) kujiunga na google analytics bonyeza hapa https://analytics.google.com/

Kuunganisa site yako na analytics tools kutakuwezesha kujua idadi ya watembeleaji katika tovuti yako kwa muda fulani.Utajua tabia ya watembeleaji wako ,muda wanaochukua katika site yako ,sehemu wanapo toka,jinsia, umri na vitu vingine vingi.Mjumuisho wa vitu hivi vitakuwezesha kujua watembeleaji wako na kufanya marekebisho katika site yako kuweza kuvutia watembeleaji wengi zaidi.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa