WHATSAPP WAZIDI KUMKOPI TELEGRAM WAJA NA MABORESHO HAYA MANNE

Katika kuboresha huduma kwa wateja wake, Programu ya WhatsApp ipo mbioni kuongeza sehemu (Features) mpya nne ambazo zitawasaidia watumiaji wake kupata unafuu na urahisi zaidi wakati wa kutumia.

Taarifa kutoka kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya Teknolojia duniani zinasema kuwa WhatsApp inafanyia kazi sehemu kubwa nne ikiwemo ya kubadilisha na kuhaririri ujumbe uliyomtumia mlengwa kabla hajausoma, sehemu hii itafanya kazi pale ambapo meseji hiyo itakuwa haijapokelewa kwa kuweka tiki mbili za blue.

Maboresho mengine ni kucheza moja kwa moja kwa video za Youtube ndani ya Programu ya WhatsApp, Kwa sasa mtandao wa Youtube ukitumiwa Link ya video kutoka Youtube ni lazima ufungue ila baada ya maboresho hayo mtumiaji ataitizama video yeyote kutoka Youtube bila kufunguwa Link kama ilivyo mitandao mingine ya kijamii.

Kurudisha meseji, picha au video ulizotuma kwa muhusika, kwa wazoefu wa mtandao wa WhatsApp au watu walioanza kutumia tangia mwaka 2015 sehemu hii ilionekana kwenye Whatsapp beta kabla ya kuondolewa mwaka jana 2016, Sehemu hii itarudishwa tena ambapo mtu atapata dakika 5 za kurudisha meseji, Jumbe, picha au video alizotuma kimakosa.

Sehemu nyingine muhimu itagusa kwenye makundi, Kuweka maelezo ya Kundi (Group Description), Kwa sasa watu wengi wanaunganishwa kwenye makundi bila kusoma maelezo ya kundi husika ambapo inakupasa ujiunge kwanza ndiyo upewe maelekezo, Kwa marekebisho hayo utaweza kuandika maelezo kuhusu group, kwa mfano kama ukitengeneza group utaweza kuandika maelezo kuhusu Group hilo, Maelezo ambayo mtu kabla ya kujiunga atayasoma kwanza hii itatokea kwa njia zote mbili ile ya kwanza ya moja kwa moja ya kuunganishwa na Admin na ile ya kutumiwa Link.

Kwa mujibu wa mtandao wa WABETA Info umeripoti kuwa kabla ya mwezi Septemba mwaka huu, Programu ya WhatsApp ambayo inatumiwa na watu zaidi ya Bilioni 1 duniani itatangaza mabadiliko hayo.


Maboresho haya yanaweza kuja kuifunika telegram ambayo kwa sasa ina feature nyingi nzuri lakini haijapata sana umaarufu?


Chanzo : http://wabetainfo.com/

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa