JINSI YA KUBADILI (UPADATE) STATUS YA MANENO KATIKA WHATSAPP

As salaam aleikum mpendwa karibu tena katika blog yako pendwa kwaajili ya kutatua matatizo yako madogo na makubwa ya kila siku katika tech leo tuangalie kuhusu kubadili status ya maneno katika vision hii mpya ya whatsapp maana hata mimi imenisumbua kwa muda kidogo bila kujua jinsi ya kubadili leo nimeweza so nawewe ni vema ukajua.

Kwanza kabisa ingia katika whatsapp yako kisha bonyeza status kama kwenye picha hapa chini
Kisha bonyeza nukta tatu juu upande wa kulia kisha bonyeza setting kama kwenye picha hapa chini
kisha bonyeza sehemu ya status yako ya zamani, picha au jina kama kwenye picha hapa chini
kisha bonyeza status yako ya zamani kama inavyoonekana pichani hapa chini
kisha bonyeza status yako tena au alama ya kalamu upande wa kulia 
itakuletea uwanja wa kuandika maneno mapya
haya sasa andika status unayoipenda kisha bonyeza ok mpaka hapo umekamilisha kubadilisha status yako

Maneno ya muandishi
Imeandikwa na Riyadi Bhai, sambaza kama ilivyo kama kuna eneo hujaelewa niachie maswali yako hapo kwenye sanduku la maoni nami nitashughulikia

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa