Kabla ya Kuanza Mchakato Huu hakikisha Simu yako ina vitu vifuatavyo
- Simu iwe Imewashwa
- Iwe na Chaji Angalau kuanzia Asilimia 50%
- Internet Connection, (WiFi Ikiwezekana)
- Ruhusu Uwekwaji wa Apps Kutoka Nje ya Play Store (Yaani unknown sources). (Nenda Settings>>>Security>>>Unknown Sources> weka Tiki)
Namna ya Ku’Root’ Android kwa Kutumia ‘Kingo Root’
- Download Kingo Root APK Hapa
DownLoad Itaanza Yenyewe, Mara baada ya Ku’click’ Download, Kama Chrome Ikikuonya
Bofya ‘OK‘ Kuendelea.
- Install Kingo Root APK katika Simu yako, Kabla ya kufanya Hivyo Hakikisha Umeruhusu Installation ya Apps Kutoka Nje ya Play Store. (Nenda Kwenye Settings>>>Security>>>Unknown Sources>> Weka Tick) Unaweza kusoma na hii [Soma Jinsi ya kuweka Playstore kwenye simu zisizokuwa na playstore]
Fungua Kingo Root APP na Uanze mchakato wa Ku’Root‘
Subiri kwa Muda Fulani Mpaka Matokeo Yatakapo Onekana kwenye kioo chako.
- Umefanikiwa Ku’Root’ Au ‘Imeshindikana’
Ikiwa Umefanikisha Utaletewa Ujumbe “SUCCEEDED” Kama inavyoonekana katika Picha.
KIDOKEZO MUHIMU: ‘ROOT AT YOUR OWN RISK’ RIYADI BHAI HAITAHUSIKA IKITOKEA TATIZO LOLOTE LITAKALOPELEKEA KUHARIBU KIFAA CHAKO
1 Comments
asante sana kaka nimefanikiwa
ReplyDeleteJe unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa