Jinsi ya kuweka Playstore kwenye simu zisizokuwa na playstore

Simu nyingi zinatoka china au zile ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kutumika china huwa hazina Google Account na kupelekea kushindwa kutumia apps za google kama Youtube, Google Playstore, Maps etc.

Leo tutaona jinsi ya kuweka Google Account kwenye simu za android ambazo hazina Google Account. Endapo utafanikiwa kuweka Google Account basi simu yako itaweza kutumia apps za google kama Playstore, Youtube, Google maps, Google Calendar, Google photos etc. 

Cha kwanza unachotakiwa kufanya kabisa ni ku-download file kwa kutumia link chini kisha lifungue hilo file na ndani yake utakuta mafile yafuatoyo Google Account managerGoogle Play ServicesGoogle Services Framework,Vending.apk, pamoja na Google Play Store Ili uweze kudowanload bonyeza hapa DOWNLOAD  Kisha utasubiri kwa sekunde 5 kisha bonyeza SKIP AD kisha bonyeza download now.

Weka Google Account manager , kisha baada ya kumaliza weka tena Google Services Framework kisha install tena Google Play Services halafu zima na kuwasha simu yako (restart) 

Baada ya simu yako kuwaka install Vending.apk halafu install google play store. Ili kuakiki kama Google Account imeingia kwenye simu yako, nenda kwenye setting kisha account na utaiona Google Account. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka google account kwenye simu yako na utaweza kutumia apps za google kama Youtube, Google Playstore, Maps etc.

Mwisho umefanikiwa lengo, sambaza makala hii kwa marafiki kadri uwezavyo kama hujaelewa acha maoni yako hapo chini ni vema ukatumia blogger coment box kwani kutakujibu kwa haraka zaidi kuliko kutumia facebook coment box

2 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa