Bila kupoteza muda, Gbwhatsapp inakupa uwezo wa kubadili launcher icon ya whatsapp na kuipa muonekano unaotaka wewe. Mfano tazama picha chini na utagundua whatsapp yangu ya kawaida ina icon ileile ambayo kila mtu anayo lakini kwa vile nina Gbwhatsapp nimeweza kubadilisha icon yangu na kuifanya kuwa nyekundu
Kitu kingine muhimu kuhusu GBwhatsapp ni lock chat.Lock Chat inakuwezesha kulock chat ya mtu mmoja hata mtu akijaribu kubonyeza chat ya huyo mtu basi whatsapp itamwambia aweke password ili aweze kusoma hiyo chat. Hii ni nzuri kwa wale mademu zetu wa kibongo wanaopenda kubonyeza chat za wanawake wengine ili kujua unachat nini.. Jinsi ya kuweka lock fungua chat ya mtu unayetaka kumuwekea nywila (password) kisha nenda kwenye kipengele cha setting kisha bonyeza kipengele cha chat lock kisha whatsapp itakwambia uweke password.
Jambo lingine zuri kuhusu GBwhatsapp ni uwezo wa ku-copy status ya mtu. Wengi tunajua kwamba kwenye whatsapp huwezi ku copy status mpaka uandike sehemu halafu ndio ukaweke kwako lakini kwenye Gbwhatsapp mambo kama hayo yanawezekana na ni rahisi kama kumsukuma mlevi. Ukitaka ku-copy status ya mtu unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye status ya huyo mtu unayotaka ku-copy kisha bonyeza na kushikilia kwa sekunde kadhaa utaona ujumbe unaosema status copied to clipboard
GbWhatsapp ina kuwezesha kuchat kwenye magroup kijanja zaidi kushinda ilivyo kwenye Whatsapp ya kawaida. Mfano kwenye Gbwhatsapp ukiwa kwenye group na unataka ujumbe wako utume kwa mtu flani basi unachotakiwa kufanya ni kuandika alama @ kisha utaona majina ya watu ambao waliopo kweye group na utabonyeza jina unalotaka
Kwa wale wanaotaka kujaribu Gbwhatsapp, unaweza ku-download kupitia link chini >>>download
Kuwa karibu nami kwa kujiunga kupitia katika mitandao yangu ya kijamii youtube, facebook, Twitter na istagram kote huko andika jina @Riyadibhai sambaza upendo kwa kushare makala hii
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa