Kama bado unakunywa energy drinks, soma hii.
Utajifunza:
-Madhara
-Ingredients
-Tafiti zinasemaje
-Energy hufanya nini kwenye mwili wako?
-Namna bora ya kupunguza matumizi
share Wengi Wajifunze
Tafiti zinaonesha hali ni mbaya sana.
Umewahi kujiuliza kwa namna watu wanvyobwia energy, baada ya miaka 10-20 itakuwaje?
Mazoea hujenga tabia, tabia itakupa uraibu.
Sio vijana, watoto, sio wanawake, wote wanabwia energy utasema kuna jambo la maana wanafaidika.
Binafsi huwa najiuliza watu wanakunywa energy drinks kupata nguvu, utamu au uraibu?
Eti kwenye energy unapata nini?
-Nguvu
-Utamu
-Imekuwa uraibu?
Kwa madhara yake, kwa hakika hii ni kasumba tupu.
Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watumiaji wa energy drinks.
Tafiti nyingi zinafanywa kwenye kuangalia madhara yake.
Pengine zingekuja tafiti nyingi zaidi za kuangalia kwanini watu wanatumia bila kuacha,
Hasa kwa mazingira yetu ya Kitanzania na aina ya energy zinazouzwa kwetu.
Mwaka 2017, huko North Carolina USA, Davis Cripe, kijana wa miaka 16.
Alipoteza maisha baada ya kunywa energy drink, kahawa na kinywaji chenye caffeine nyingi.
Matukio kama haya yanashangaza sana, kwa kijana mdogo kama huyu kuanguka na kufariki kwa shambulio la moyo.
Sio kitu cha kawaida kabisa.
Baada ya uchunguzi, energy drink na kinywaji chenye caffeine nyingi vilihusishwa moja kwa moja na kifo cha bwana mdogo.
Source:
https://bbc.com/news/world-us-canada-39932366…Nini kinawekwa kwenye energy?
Ingredients za kawaida kwenye energy drinks:
1. Caffeine
2. Taurine
3. B vitamins
4. Guarana
5. Ginseng
6. L-carnitine
7. Sugars
8. Green Tea Extract
9. Guarana
10. Green Coffee Extract
11. Ginkgo Biloba
12. Glucuronolactone
Chunguza namna hivi vitu vinavyoathiri mwiliNini Kinatokea Ukinywa Energy drinks?-Baada ya Dak. 10
Caffeine inaingia kweye damu na mapigo ya moyo na presha inaanza kupanda.
-Baada ya Dak. 15-45
Caffeine inafanya kazi na kukufanya uwe high na kujisikia mwenye nguvu.
-Baada ya Dak. 50
Caffeine yote inakuwa absorbed na sukari inakuwa imefonzwa sana kutoka kwenye damu.
-Baada ya Saa 1.
Sukari inaisha kwenye damu na caffeine inakuwa ipo chini.
Hapa unaanza kujisikia mchovu na kutokuwa na nguvu.
-Baada ya Saa 12.
Caffeine ndo inaisha kwenye damu.
-Baada ya saa 12-24
Kichwa kuuma, maumivu na constipation.
-Baada ya wiki 1+.
Mwili ndo unaanza kuzoea caffeine.
Source:
https://medicalnewstoday.com/articles/298202Madhara ya Energy drinks
-Mwili kupungukiwa na maji
-Anxiety na kujisikia vibaya
-Kukosa usingizi kwa walio wengi
-Sukari huleta madhara kama saratani, unene na kisukari
-Kuongezeka kwa stress na depression
-Kuongezeka hatari ya magonjwa ya moyo
- Kudhuru figo n.k
Mambo ya kuzingatia kupunguza madhara
- ACHA KABISA KUNYWA HII KITU
Kama unakomaa basi hakikisha:
-Usinywe zaidi ya kopo moja lenye ujazo wa mililita 250 ndani ya saa 24
-Usichanganye pombe na energy drink
-Usinywe kabla ya kwenda kulala.
-Watoto, wajawazito na wanaonyonyesha, wakae mbali (Juzi kati kuna mjamzito alidondoka baada ya kupiga hii kitu).
-Usichanganye na vinywaji vingine vyenye caffeine au sukari nyingi.
-Usitumie kabla au wakati wa kazi nzito.
-Usitumie kama kiondoa usingizi.
NB: Ni Ushauri tu, Kwa FAIDA yako:
ACHA KABISA KUNYWA HII KITU
ACHA KABISA KUNYWA HII KITU.
ACHA KABISA KUNYWA HII KITU.
0
Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa