Je' Seebait ni matapeli au wamefilisika!?

 

As salaam aleikum ndugu msomaji wa ukumbi wetu huu katika pitapita na mahangaiko kutoka maeneo tofauti tofauti huko mitandandaoni nimepokea malalamiko kadhaa kutoka kw wasomaji wetu kuhusu seebait je ni matapeli au wamefilisika, naam ili inatubidi tuliangalie kwa undani kidogo kama tulivyoandika makala ya kuhusu kujiunga na kampuni ya matangazo ya seebait yenye makao yake nchini tanzania,


naam katikamahojiano na mmoja katika ya wahusika wakuu wa mtandao wa seebait yeye alidai kuwa amejiondoa kutoka seebait ni miaka miwili mpaka sasa ivo hakutupa mrejesho uliojitosheleza lakini alitupatia namba za mmoja kati ya watu wanaoendesha seebait kwa muda huu ambao yeye hayupo katika ushirika na kampuni hiyo. naam nasi tukamtafuta ili kupata uhakika na jambo linaloendelea.

Tulimpigia simu bwana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la alex anaonekana kama mkenya kutokana na rafudhi yake yeye alipoulizwa kuhusu maombi ya malipo ambayo yamefanyika tangu mwezi wa nne na yapo pending hayajalipwa mpaka sasa mwezi wa sita tarehe 22 alidai kuwa wao wenyewe hawajalipwa kutoka katika makampuni yaliyoyatangazia.


Je' mfumo wa matangazo upoje.

katika dunia yote makampuni ya matangazo ili tangazo lako liweze kuwa hewani ni lazima ulipie kwanza front payment ndio kampeni yako iwekwe hewani, sio kwa kampuni kubwa wala ndogo, kama adword kutoka google lazima ulipie kwanza ndio kampeni yako iwe hewani, hata youtube, facebook, instagram na twitter pia na mitandao yote unayoifahamu mfumo wa malipo huwa unakuwa ivo je vipi hawa seebait wanaleta ngonjera za namna hizi ambazo hazieleweki wala kuaminika hata na mtoto mdogo.


Related Article

hawa seebait kama sio matapeli wa wazi ni kampuni iliyoshindwa kujiendesha na sasa imefilisika na haijui hata pakuanzia inabidi watoe tamko wazi ili ijulikanane kwa jamii ya mapublisher wao kuhusu kizungumkuti kinachoendelea.



Imeandikwa na Ibrahim Riyad Houmud Ruwehy.

Namba ya simu 0717101085

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa