JINSI YA KUPATA LINK YA GROUP LA WHATSAPP

Haya ni wakati mwingine tena leo tugusie whatsapp kuhusu kupata link ya group ulilolianzisha, wenda ulikuwa umesikia jambo hili lakini umeshindwa jinsi ya kuipata hiyo link yenyewe basi Riyadi bhai nipo kwaajili yako tuwe pamoja ili tuelewane vema hapa chini maelezo na picha 

ingia kwenye group lako kama kwenye picha hapo chini
Kisha bonyeza jina la group itakuletea muonekano huu pichani hapa chini
Kisha bonyeza upande wa juu kulia kwenye kinembo cha mtu+ yaani sehemu ya kuadd mtu kwenye group utaona muonekano huu
Nafikiri umeanza kupata mwangaza wa jambo letu hili sasa bonyeza Invite to group via link utaona muonekano huu pichani
naam sasa unaweza kuwatumia watu wako wa whatsapp ili wajiunge na group lako kupitia sehemu iliyoandikwa send link via whatsapp, unaweza kuicopy kwa kubonyeza copy link au unaweza kuisambaza katika mitandao mingine kwa kubonyeza share link
Lakini pia kama umeshare link ya group lako kimakosa au hautaji tena kwa muda huo watu waendelee kujiunga kwa kutumia link ulioisambaza basi unaweza kubadilisha link ya group lako kwa kubonyeza Revoke link
nafikiri kama ulikuwa hujui habari ndio hii hapa sambaza na wenzetu wa jue kuhusu haya mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa tekno, kama kuna sehemu hujaelewa niachie maoni yako kwenye sanduku la maoni riyadi bhai hapa endelea kuwa nami

3 Comments

  1. Ok tunaomba na msaada namna ya kuweka whatsapp button share na pia namna ya kuweka link ya group la whatassp kwenye blog ili mtu aweze kujiunga hata akiwa ametembelea blog

    ReplyDelete
  2. whatsapp button share hii hapa lakini sio kila template inakubali hapana kwenye baadhi haifanyi kazi >>> http://www.riyadibhai.com/2017/03/how-to-add-whatsapp-share-button-in.html

    ReplyDelete
  3. damas mapunda link ya kuweka whatsapp button share hii hapa https://riyadibhai.blogspot.com/2017/05/jinsi-ya-kuweka-whatsapp-button-share.html

    ReplyDelete

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa