Google bado inafanya kazi kwenye Kufungua kwa Uso katikamfululizo wa simu za Pixel 6


Simu janja nyingi ambazo zinatengenzwa katika miaka ya karibuni wanaziongezea sifa kwa kuzifanya kuwa na uwezo wa “Kufungua kwa uso” ingawa mambo ni tofauti kwa simu janja Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro.


Inakaribia miezi sita sasa tangu simu janja Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zitoke (zizinduliwe) lakini hadi sasa hazina teknolojia ya kuiwezesha mtumiaji kutumia uso kuifungua. Ukweli ni kwamba Google walikuwa na mpango wa kuzifanya simu hizo ziwe na teknolojia ya kutumia uso kufungua wakawa wameshindwa kufanikisha jambo hilo ndani ya wakati hivyo wakalazimika kuzitoa bila ya kuwa na kipengele hicho.


Related Article

Je, kwanini simu hizo hazikuja/hazina teknolojia ya rununu kufunguliwa kwa uso?

Wakati Google wanatengenze na Pixel 6 na Pixel 6 Pro zilifanyika jitihada za kuzifanya rununu husika kuwa na teknolojia hiyo ya kisasa katika kuifanya kuwa na ulinzi ambao ni wa aina yake lakini katika hatua ya majaribio ikabanikika kuwa muundo huo unaifanya simu kutumia umeme mwingi ili kuweza kufunguka hivyo kuwa moja ya sababu kuu ya kuiweka kando na kutoa rununu hizo bila ya teknolojia tajwa.


Inawezekana Google wakapeleka teknolojia hiyo katika maboresho yatakayokuja huko mbeleni au kuamua kuiweka kwenye toleo lijalo la simu janja za Pixel. Hivyo basi, tukae kusubiri na SwahiliTech tutakuhabarisha.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa