Kwa yule nitakayemuoa.
Wakati mwingine mimi hufikiria juu ya mahali ulipo na kile unachofanya na matumaini yangu ni kuwa maisha yanakutendea mema. Natumai unatabasamu na unaishi maisha kwa ukamilifu. Moyo wangu na nafsi yangu inakuonea shauku na nakuombea kila usiku Nikipata wasaa wa kusimama usiku bila kukosa bali kila alichotupangia Mwenyezi Mungu kiwe chenye kheri kwetu.
Nitakuwa mvumilivu. Nataka ujue kuwa utalindwa nami kwa kila njia. Wakati maisha yanaonekana kuwa magumu na ulimwengu unahisi kuwa mkubwa sana, nitakuwa hapo hapo kuhisi yote pamoja nawe.
Unaona, nitakuweka juu ya ulimwengu wangu na utakuwa kiburudisho cha macho yangu; na nitafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa kila wakati kuna tabasamu usoni mwako.
Utakuwa sababu yangu ya kutabasamu lakini siku ambazo unahisi dunia yako inakuangukia, nitakupa baadhi ya tabasamu zangu na upendo huu uliofurika moyoni mwangu utabeba ulimwengu huu unaoanguka.
Nitajifunza tabia zako zote za ajabu hadi ziwe mambo ninayopenda kukuhusu. Tabia hizi ambazo zinaweza kuwaudhi wengine zitakuwa vito vya thamani katika moyo wangu. Nataka ujue kuwa Mwenyezi Mungu ameniwekea upendo mwingi na pengine yote yameandikwa kwa ajili yako.
Kutakuwa na siku ambapo mapenzi hayataonekanika usoni mwangu - na moyo wangu utakuwa na ganzi na huzuni sana kukuandikia sms za mapenzi. Lakini nataka ujue kuwa huyu ndiye mtu yule yule ambaye anachelewa sana katika ibadah kukaa kwa siri kukuombea
na mwanamume yuleyule ambaye ataamka mapema zaidi ili tu akuone umelala kwa amani, kukubusu na kukujulia hali yako asubuhi na kuandaa kifungua kinywa unachokipenda na kukiweka tayari kando ya kitanda chako.
Wakati mwingine tutacheka usoni na wakati mwingine kutakuwa na vizuizi kati yetu usiku lakini sitawahi kwenda kulala bila kutafutasuluhu baina yetu.
Natumai mapenzi yetu yana nguvu sana hata tukijaribu kutoroshana, tunaishia kukumbatiana; maana mwisho wa siku tutakuwa pamoja nyumbani.
Nitachukulia kila kitu chako kana kwamba ni changu na nitakitunza kama changu. Iwe ni wazazi wako, mali yako, chochote na kila kitu. Kweli. Wewe ni kitabu kilichojaa mafunzo mengi mno, nahitaji kujifunza na kusoma ili nielewe jinsi unavyohitaji kupendwa.
Sitakuhukumu kwa tabia zako mbaya na ninatumai kuwa hautahukumu pia. Nataka ujue kuwa sio tu utakuwa mke wangu lakini pia utakuwa rafiki yangu, mshauri, rafiki wa dhati na mpenzi wangu wa kwanza.
na kuna wakati kuna rangi ya huzuni katika macho yako ya kupendeza, nitakuwa wa kwanza kuiona. Kutakuwa na siku za giza mbele yako lakini ninakusihi kamwe usipoteze matumaini kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu tumaini kuu ambalo mtu anaweza kuwa nalo ni kumtumaini Mwenyezi Mungu.
Kupitia nyakati hizi za giza, nitakuwa hapo kwa ajili yako kila hatua,katika hali nzuri na mbaya, wakati wetu wote wa maisha yetu, tunapokuwa na mtoto wetu wa kwanza, wakati anajifunza kutembea kwa mara ya kwanza,
Nitakuwa nawe kupitia yote pamoja. Natumai hautaniacha kamwe kwa sababu sitakuacha kamwe.
Nikiwa kwenye kitanda changu cha Mauti nitakaemuona ni wewe tu na nia yangu ya mwisho itakuwa kukutana nawe tena siku moja. na kuishi siku ambayo ni muda wake ni sawa na miaka elfu. Nitakungoja lakini mpaka hapo nitakuwa nikikuombea.
ni mimi Ibrahim Riyad
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa