Barua yangu ya wazi, Kwa binti yangu mdogo Ghufairah


Kwa mtoto wangu mdogo wa kike Ghufairah,

Nataka kukuambia mambo mengi sana

Tazama Baba ameishi maisha marefu, na amepitia mambo mengi sana

Kwa hiyo naomba ujifunze kutoka kwangu

Makosa, na kufaidika na yale ambayo nimeona

Kwa matumaini kwamba utakuwa vizuri sana

Bora kuliko kila kitu ambacho nimekuwa

Ewe mtoto wangu mpendwa, jua kwamba kuna Mungu mmoja tu,

Na Yeye Subhanahu wataala anastahiki zaidi mapenzi yenu yote

Ameumba kila kitu na ana ujuzi wa kila kitu

Basi usimfanyie mshirika, na mcheni tu Yeye

Na fahamu kwamba mnapofanya dhambi ni lazima mrejee kwake na mkumbuke

Kwa kushikilia kamba yake Mola, itakuongoza tu kuelekea Jannah

Mahali pa raha zote, ambapo mtakaa na kukaa milele

Katika kampuni ya watu bora ambayo mizani ya haki imewahi kupima

Ewe mtoto wangu mpendwa, jua kwamba Mwenyezi Mungu ana haki juu yako na mimi.


Kwanza kabisa, anzisha yako Swalah, na usiiache ipite mpaka ufe

Kwa hivyo omba kila sala kana kwamba ni nafasi yako ya mwisho kusema kwaheri

Na kamwe usione aibu kuinua mikono yako na kumwita nakumtaka msaada

Ewe mtoto wangu wa kike, wewe ni mrembo kuliko vile utakavyowahi kujua

Na hauitaji mtu yeyote kukuambia kuwa wewe ni mrembo.


Hayo ni kwa sababu Mola wako amekufanya hivyo

Basi iheshimu zawadi hii ambayo Mwenyezi Mungu Amekutunuku

Wala usidhihirishe Aliyo yazuilia ila kwa wale Aliowachagua

Na ujue kwamba hijabu hii unayoipenda Kuvaa ni zaidi ya nguo tu

Ni ukumbusho kwa ulimwengu kwamba wewe Ni zaidi ya kile wanachokitazama

Akili, mwili na roho isiyodhibitiwa na kila kisanduku kidogo cha media

Kabla ya kila rafiki na mwenendo,


Unapaswa tu kuwa na wasiwasi juu ya kumvutia Mungu Mmoja

Na kisha baada ya hayo mama yako anastahili upendo wako wote,

Alikubeba kwa muda wa miezi 9 na kukutunza kwa upendo murua

Kwa hivyo mtendee wema kwa rehema na heshima hata unapofikiri amekosea

Na ninaahidi tutajitahidi tuwezavyo kukulea katika nyumba yenye upendo

Nitakuweka miguuni mwangu usiku na kukusomea hadithi hadi ulale

nitashiriki nawe kuijua historia ya Musa na Bani Isreal

Nitakuambia kuhusu Chewa ambaye alimmeza nabii Yunus mzima mzima

Na mchwa aliyezungumza na Suleimani kutoka ndani kabisa ya shimo

Tutajifunza yote kuhusu maswahaba, na kukariri kila jina la mmoja wao

Nitakuambia kuhusu Bilal ibn Rabah,


Na kukuonyesha kuwa ukoo wetu ni sawa Tutapenda hadithi ya Mtume wetu, kila wakati

Na tutalia kila wakati tunapofika mwisho Nataka kuwa rafiki yako bora, nataka kuwa yule ambaye unamtegemea Nataka unipigie kutoka shuleni uniambie Umesahau kazi yako ya nyumbani,tena

Ninataka kukupeleka kwenye safari, nataka uone ulimwengu

Nataka kushikilia mkono wako mbele ya Kaaba na kukuonyesha jinsi gani mbingu inavyoonekana duniani

Ninataka kukufundisha kuendesha baiskeli, nataka kukufundisha kuendesha gari pia.


Nataka kukufundisha kuwafukuza huko Wapenda mali hawatakufikisha mbali

Kwa sababu watu wengine ni masikini, kitu pekee wanalicho nacho ni pesa,

Ninataka kukufundisha kuridhika.


Mwenyezi Mungu na mimi tunaahidi kuwa utakuwa na furaha daima

Kwa sababu ikiwa marais, mawaziri wakuu, wafalme na malkia wote

Walijua baraka za Uislamu, Wakweli pia wangetupigania kwa ajili ya Dini hii uislamu.


Ninataka kuwa karibu yako nikufariji utakapoota ndoto mbaya;

Ninataka kukuambia ukweli kuhusu Halloween

Kwa nini hatuvai kama masheytwan,

Lakini bado nitakununulia pipi zaidi ya unazoweza kula Nataka nikufundishe kwamba unavuna ulichopanda,

Na kwamba kazi ngumu na mapambano yatakusaidia kukua Ninataka kukufundisha kutorudi nyuma kutokana na changamoto Na uaminifu huo ndio njia pekee ya kwenda mbele.


Nataka kukufundisha Qur'an, nataka kukufanya uipende Qur'an

Nataka uihifadhi moyoni mwako,

Chukua hatua na uione dunia nzima kupitia Qur'an

Nataka ufahamu makatazo ya Mwenyezi Mungu na maamrisho yake

Na kufuata kwa ubora wako kuliko mafundisho yoyote

Mfano, mjumbe wake Aleiyh salatu wasalaam

Na siku moja, naomba kwa mola wako na utapata upendo wa kweli, lakini sio tu kwa mwanaume yeyote


Lakini kwamba utaolewa na mwanamume ambaye pia ana mapenzi na uislam

Hivyo kama unataka mwanaume kama Muhammad, Inakubidi uwe mwanamke kama Khadija

Msaidizi wa kwanza wa jambo hili la uislamu na mama kwa waumini

Kuwa na ujasiri kama wa Nusaybah, usirudi nyuma katika ukweli

Tetea kile unachoamini hata wakati ulimwengu wote utasimama kukupinga.


Kuwa na elimu kama ya Aisha, kuwa mwanachuoni wa dini hii

Ponya watu kutokana na imani potofu kwa sababu Ujinga ni ugonjwa

Uwe na uchamungu wa Hafsa, na umuweke Mwenyezi Mungu juu ya mawazo yako

Funga mchana na uswali usiku, ili kuisaidia nafsi yako kukaa sawa

Kuwa na heshima ya Balqis, ifanye dunia ikutendee wema kwa utu wako

Wanapokuona mitaani,wajulishe kuwa wewe ni malkia

Kuwa na nguvu za Sumayya na subira kama ya Hajar,

Kuwa imara kama Maryam, tawakkul kama mama yake Musa

Na mambo yanapokuwa magumu, uwe kama mke wa firuan

Ambatanisha moyo wako na Jannah, na usiiache kamwe ndoto hii.

Maana wewe ni mpenzi wa kweli kwangu, kama Fatima kwa Nabii wetu

Mwenyezi Mungu akubariki kwa utulivu, kuanzia sasa hadi milele. Ameen


Mtoto wangu wa kike, nimekuleta katika ulimwengu wenye mambo mengi sana

Ambapo ukweli unaweza kuumiza, na uwongo unaweza kung'aa kama lulu

Dunia hii ni pepo kwa wale ambao wameuza roho zao

Na ni gereza kwa wale wanaoshikilia kanuni hii ya maadili

Mtoto wangu wa kike, nakuahidi hilo.


Niko hai nitajitahidi kukufanya utabasamu

Nitaenda maili nyingi za ziada kwajili ya mtoto wangu Ghufairah, lakini tambua

Kwamba dunia hii imejaa majaribu

Hiyo itabidi upitie tu, na fahamu ya kuwa wewe huna wakumtegemea ila Mwenyezi Mungu.

Tambua ya kwamba Mwenyezi Mungu ni zaidi ya msaada kwako

Ninakuombea kila wakati, kwa hivyo tafadhali niombee pia,

Muombe Mwenyezi Mungu anisamehe madhambi yangu, na alijaze kaburi langu  Nuru


Lakini nakuahidi, Jannah tutaendelea na mchezo wetu mdogo wa kukimbizana kati ya Baba na msichana wake mdogo.


Nakupenda sana Binti Yangu Ghufairah


Hisia zangu kwa Bint yangu wa kipekee

Ibrahim Riyad Ruwehy


 

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa