Faida za maji ya nazi/Dafu Je ni kweli yanasababisha Busha

 

As salaam aleikum ndugu yangu mtembeleaji wa Blog hii karibu tena leo katika dondoo za Afya leo tutajaribu kuangazia Faida za maji ya madafu au nazi je ni kweli yanasababisha Busha au ni alifu lela ulela za vijiweni

Maji ya madafu yana ladha nzuri na ya kipekee ukiachilia kuwa ladha ya kipekee, maji ya madafu yana faida nyingi na manufaaa katika mwili wa binadamu


Faida ya maji ya dafu ni kama zifuatazo


(i)  Maji ya madafu yana utajiri mkubwa sana wa vitamin mbalimbali, amino acids,vimen’genyo, viondoa sumu pamoja na virutubisho mbalimbali.


(ii)  Maji ya madafu yana imarisha mzunguko wa damu mwili


(iii) .Maji ya madafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. 


 Yanazuia Upungufu wa Maji Mwilini.


(iv)  Maji ya madafu yanasaidia kuzuia muonekano wa kizee (anti-aging ): Matumizi ya mara kwa mara ya maji ya madafu yatakufanya uonekane kijana hata kama umri wako umeenda. 

(v) Maji ya madafu yana kiasi kidogo cha kalori.


(vi)  Maji ya madafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa usagaji chakula tumboni.


(vii) Maji ya madafu yanasaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya moyo pamoja na presha.


(viii)  Yanaimarisha ubongo na misuli.


"Maji ya nazi (dafu) husaidia kuongeza mbegu za kiume,mwendo kasi wa mbegu,homoni ya kiume na kuondoa mbegu zenye dosari kwa mwanaume,kutokana na uwepo wa madini na vitamini kwenye maji hayo,wanaume wanashauriwa kunywa kwa afya. Haya sababishi busha".


Asante kwa kusoma makala zetu na kuwa mwanafamilia wa blog hii Riyadibhai.blogspot.com

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa