As salaam aleikum ndugu zangu Kutokana na ukosefu mkubwa wa ajira unaoikumba nchi yetu vijana wanaweza kutumia fursa zilizopo za kidigitali ili waweze kujikwamua kiuchumi kuliko kiuendelea kuisubiri serikali huku wakati ukiwatupa mkono. katika makala hii tutatalii ni kwavipi mwalimu au mtu mwenye ujuzi fulani anaweza kujiajiri kupitia kufundisha kupitia TEHAMA.
Ufundishaji wa mtandaoni Teaching Online, Ni mchakato mzima wa kuandaa na kutoa maudhui yenye lengo la kueneza maarifa kwa mtu au watu kwa njia ya mtandao.
Kufundisha mtandaoni ni miongoni mwa njia za kujiingizia kipato mtandaoni. Sio lazima uwe umesoma digrii ya ualimu ndipo ufundishe mtandaoni, bali pia unaweza kufundisha kile ulicho na ujuzi nacho kwamfano unaweza kufundisha lugha, mapishi, na mengineo mradi tu unauelewa nacho.
Mambo ambayo unaweza kufundisha mtandaoni
Lugha, biashara, muziki, mapishi, mazoezi, afya, Masuala ya kompyuta, na mengineo. Ufundishaji wa mtandaoni tunaweza kuugawa katika makundi mawili ambayo ni,
Kufungua darasa mtandaoni (online classes) hapa unaweza kumfundisha mwanafunzi mmoja mmoja au hata kikundi.
Kuanzisha kozi mtandaoni (online course), - kufundisha wanafunzi kama sehemu ya kozi mtandaoni.
Kuanzisha darasa mtandaoni. Kuanzisha darasa mtandaoni hauhitaji kuwa na vitu vingi hivi ni baadhi ya ambavyo unalazimika kuwa navyo,
Vifaa. Ili uweze kuanzisha darasa mtandaoni itakubidi kuwa na vifaa kama vile tarakilishi/ komyuta, mtandao wa internet ulio imara, phoni za masikioni na kamera ikibidi.
Software. Nilazima uchague software ambayo utafungulia darasa, hii itakuwezesha kufanya darasa, (web conferencing platiform) miongoni mwa software maarufu kwaajili ya kuanzisha darasa mtandaoni ni
Skype. Mtandao huu huruhusu mawasiliano ya mtu moja na mwingine kupitia video bila malipo na kwa urahisi hivyo unaweza kuutumia kufundishia. Vilevile skype huruhusu mikutano ya video pamoja na akaunti za malipo, unachopaswa kufanya ni kutafuta wanafunzi wa somo lako, kukusanya malipo na kuandaa darasa kwa kufungua akaunti ya skype
ZOOM
Huu ni miongoni mwa mitandao maarufu ya kuandaa mikutano mtandaoni kwa njia ya video, simu, na maandishi. Zoom huruhusu mawasiliano ya watu zaidi ya wawili, kwa dakika zaidi ya 40 bure. Kufungua akaunti ya zoom ni bure kwaajili ya mtu mmoja mmoja na ni malipo kwaajili ya biashara.
Je kuna faida na hasara gani unapofundisha mtandaoni?
Tukianza na upande wa faida ufundishaji wa mtandaoni, kwanza ni njia mojawapo ya kujiajiri kwa kufungungua darasa lako bila kuhitaji mtaji mkubwa, pili ni njia nzuri ya kukwepa maambukizi na majanga kwani haiwakutanishi mwalimu na mwanafunzi ana kwa ana, tatu unaweza kumfundisha mwanafunzi aliyesehemu yeyote na nne, haina ukomo wa mapato.
Pamoja na faida hizo ufundishaji wa mtandaoni huweza kukumbwa na changamoto kama, ugumu wa njia za malipo kwa baadhi ya nchi, ukosefu wa intarnet imara na ni njia ngumu kufundishia watu wenye matatizo ya uoni au kusikia. Muhimu, mwalimu hakikisha unajiandaa vyema, kutafuta mazingira yenye utulivu, intarneti imara pamoja na matumizi sahihi ya lugha ili darasa lako liweze kwenda sawa. Pia hakikisha hutozi kiwango kikubwa sana cha malipo kwaajili ya darasa lako.
Kuanzisha kozi ya mtandaoni.
Hii ni njia bora sana ya kufundisha mtandaoni kwani mwalimu huweza kuwa na wanafunzi wengi sana kwaajili ya kozi yake.
Kama ilivyo kwa uanzishaji wa darasa mtandaoni, uanzishaji wa kozi mtandaoni pia huhitaji vifaa kama vile, kompyuta, phoni, internet ya uhakika pamoja na malighafi ya ufundishaji. Kwa kutumia vifaa hivyo unaweza kutengeneza maudhui ya masomo mbalimbali katika maumbo ya video, maandishi au sauti. Kumbuka kuwa maudhui yaliyo katika mfumo wa video na sauti huwavutia wanafunzi zaidi.
Software, baada ya kuandaa maudhui yako yakufundisha unapaswa kutafuta software nzuri ya kufundishia, software nyingi zitakuruhusu kufungua akaunti, kupakia kozi yako pamoja na kupanga bei ya kozi yako, na baada ya hapo wao hukata asilimia fulani kama malipo ya mtandao huo. Baadhi ya software hizo ni;
Udemy, Hii ni miongoni mwa tovuti maarufu ya kuanzisha na kuuzia kozi mbalimbali mtandaoni, mtandao huu umeripoti kuwa na wanafunzi zaidi ya milioni 12. Vilevile Udemy hukata asilimia fulani kwa kila kozi yako iliyouzika kwaajili ya malipo. Malipo yaliyobaki ni kwaajili ya mwanzishaji wa kozi napengine wabia (affiliates).
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa