Kwanini Keyboards Nyingi Zina Logo Ya Microsoft (Windows)?!


Hivi ushawahi kujiuliza kwanini keyboard nyingi za kompyuta zina alama ya Microsoft (windows)? ahaha! ni ka swali flani hivi kadogo sana ila kana maana sio?


Keyboard zipo za aina nyingi sana, kuna hizo ambazo zina alama hiyo ya windows na zingine zina alama zingine kabisa kwa mfano keyboard ya mac yenyewe ina alama ya command na zingine zikiwa na alama nyingine kabisa.


Ni wazi kwamba kwa namna moja au nyingine kitufe hicho kina kazi moja ambayo inafanana, hii ikiwa na maana kwamba kitufe hicho ukikobofya kitakueletea katika ‘start menu’ (kwa kompyuta nyingi).

Saa zingine ni kwamba kitufe hicho kikibofya na kitufe kingine inakua ni kama shortcut ya kufungua kitu. kwa mfano kama katika keyboard ya microsoft ukibofya alama ya windows + E itafunguka ‘Windows Explorer’.


Sasa sababu ni nini hasa ambayo inapelekea ‘keybaoard’ nyingi ziwe ni hiyo alama? kwa jibu la haraka haraka ni kwamba umiliki wa soko. Ni wazi kwamba katika kompyuta kwa ujumla ni Microsoft ndio wameliteka soko.

karibia ya asilimia 90 ya kompyuta zote zinakuja zikiwa na progamu endeshaji ya microsoft. Hii ikimaanisha kuwa asilimia 10 iliyobaki ndio wanayogawana makampuni mengine katika swala zima la programu endeshaji.


Hii inapelekea kwamba keyboard nyingi zije na kitufe hicho. Kwa kompyuta kama Mac na Chrome book zinyewe huwa haziji kabisa na kitufe hicho.. huwa zinakuja na vitufe vingine ambavyo kwa namna moja au nyingine vinakuwa na kazi sawa.

Sasa unajua alama ya ‘windows’ inapatikana maeneo gani katika ‘keyboard’?. alama hiyo ipo upande wa kulia na wa kushoto mwa ‘space bar’.



0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa